Advertisements

Saturday, February 28, 2015

NDOA YA TEMBA YAPUMULIA MASHINE


Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amani James ‘Temba’ akiwa na mke wake siku ya ndoa yao.

Habari kutoka kwa chanzo kilicho karibu na wanandoa hao wanaoishi wilayani Temeke, kinasema kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu baina ya watu hao, kila mmoja akimtuhumu mwenzake kusaliti, jambo linaloonyesha wakati wowote ndoa yao inaweza kusambaratika.

“Jamaa hayuko ‘peace’ kabisa na ndoa yake, yaani kila siku ni mgogoro, wife wake anamshutumu mshkaji kuwa msaliti kwa wanawake wengine na mke naye anatuhumiwa hivyohivyo ili mradi hakuna amani kabisa.

Inaonekana kuna tatizo kubwa,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Gazeti hili halikuweza kuwapata wanandoa hao kutokana na simu zao kutopatikana, lakini wakati linakwenda mitamboni, lilipata taarifa za kufikishwa mahakamani kwa Mheshimiwa Temba, ambaye anashtakiwa kwa kosa la kutishia kuua, kitendo alichokifanya kwa Godfrey Deogratius anayemtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe. GPL

1 comment:

Anonymous said...

"habari kutoka chanzo kilicho karibu"- hii habari ni feki kwa sababu familia ya huyu bwana inaonyesha upendo jinsi walivyoshikana mikono wakiwa na familia zao na marafiki.

"Jamaa huyuko "peace" kabisa na Ndoa yake": malalamiko yako wapi na mwawadikaji wa hii habari unao ushahidi?

mwandishi kaandika: "Mheshiniwa Temba, amabye anashitaiwa kwa kosa la kutishia kuua, kitendo alichokifanya kwa Geofrey Deogratius anayemhutumu kwa uhusiano wa kimapenzi na mkewe"

hapa mwadikaji wa hii habari amepotosha sana: Kwanza, Masliti hafanyi mapenzi. Huyu "jamaa" na Mheshimiwa temba ni watu wawili tofauti kwa sababu Temba ni ukoo mkubwa sana unaonza South africa, mpaka Kenya na nchi nyingine.

Waandishi wa habari, na watangazaji wawe waangalifu wanavyoandika habari ammbazo hazina ukweli au uchnguzi wa kikamilifu