Advertisements

Saturday, February 28, 2015

RUBANI APATA MAJERAHA BAADA YA NDEGEVITA YA JWTZ KUANGUKA MWANZA


 Ndege hiyo kabla ya kuruka.
Moto mkubwa ukiwaka baada ya Ndege Vita ya Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) kuanguka katika uwanja wa jeshi Mwanza baada ya kupata hitilafu.

Rubani wa ndgevita hiyo Meja Peter Lyamunda  alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa.
 Picha Juu ni Mabaki ya ndege hiyo baada ya moto kuzimwa. Rubani wa Ndege hiyo 
  Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa eneo la tukio kuangalia mabaki ya ndegevita hiyo iliyopata ajali leo.
----
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea jana tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.

Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita,  Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto. 

Hata hivyo, rubani wa ndegevita hiyo Meja Peter Lyamunda  alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .

Wananchi wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundo mbinu. 


Imetolewa na

Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano
Makao Makuu ya Jeshi ,UPANGA
S.L.P 9203,Dar es Salaam,Tanzania
Kwa Masiliano  Zaidi -0783-309963

2 comments:

Anonymous said...

Yaani hata sitaki kuamini kama ndege ndiye aliyesababisha hili balaa tena ni baada ya Ndegevita kuruka angani.!!!! Haiwezekani hata kidogo kuna wanachoficha hawa watu maana helikopta za jeshi zinaanguka sana tu na hata juzi juzi kuna helikopta ya Maliasili na Utalii ilianguka pale Kipunguni-Ukonga na kuua watu wote waliomo ndani.
Tunahitaji uchunguzi wa maana sana ufanyike,

Anonymous said...

Uchunguzi kwa faida gani wewe,kweni hapo wakudanganye ili wapate nini