
Waziri Nyalandu(kushoto) akiwa na Aunt Ezekiel Marekani.
Hatimaye Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye ni Mbunge wa Singida Kaskazini kwa leseni ya CCM, Lazaro Samwel Nyalandu na mkewe Faraja Kotta wamejibu tetesi kuwa mheshimiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson.
Awali tetesi hizo zilieleza kwamba Nyalandu na Aunt walikutana nchini Marekani kwenye hafla ya ubalozi wa Tanzania nchini humo.
Kwa mujibu wa Nyalandu ambaye ni miongoni mwa waliotangaza nia ya kugombea urais mwaka huu, hilo ni jambo ambalo alipenda mno kulitolea ufafanuzi kwa kuwa lilipoandikwa watu wake wa karibu walimuuliza pia kutaka kufahamu kama kuna ukweli wowote.
“Unajua mpaka nikaanza kucheka,” alisema Nyalandu.
“Unajua watu wana midomo, watu wanaweza wakachonga lakini michongo mingine inaweza ikawa haina dili kabisa.
“Hata anayechonga pia anajua anasababisha zogo ambalo anataka lizae matunda na wanajaribu kuliendeleza.
“Nilifika kama mgeni rasmi kwenye tukio ukiwa mwaliko wa ubalozi na tukio lile lilichukua saa moja na huyo dada anayeitwa Aunt Ezekiel katika maisha yangu nimemuona siku moja, ndiyo hiyohiyo siku nimemuona, nilikuwa sijawahi kumuona tangu nizaliwe.
“Tumekutana naye akiwa mwalikwa pamoja na maDJ wengine wa Bongo Fleva katika tukio lenye watu wengi ambao ni Watanzania waishio Marekani.
“Nikiwa mgeni rasmi nikatoa vyeti, nikatoa hotuba wakanisindikiza nikaondoka. Kwa hiyo kwanza katika hali hiyo ya kuwa Amerika (Marekani) atakuwa aliniona kwa saa moja kwenye ule mkutano.
“Lakini pia nilikuwa sijawahi kumuona katika maisha yangu na sijawahi kumuona tena, yaani ni mtu ambaye sifahamiani naye,” alisema Nyalandu pembeni akiwa na mkewe.
GPL
3 comments:
Waziri usipate tabu huyo aliyeanzisha hii story yupo bongo sisi tuliokuwa hapa tunajua ukweli. Dada Ezekiel tulikuwa naye hapa Maryland kwa muda na tulichill naye sehemu nyingi wakati wewe uliishajiondokea kwenda California kwa shughuli zako binafsi na kurudi nyumbani. Na dada huyu alikuwa na wenyeji wake waliomwalika 24/7. WABONGO TUACHE UZUSHI. Mheshimiwa we love you and you inspire us the young generation since you were here in USA kama wengi wetu tulivyo na mpaka sasa unaendelea kufanya mambo mazuri...
GOOD JOB STAY FOCUSED NA WAACHE WASEME..
kimewaka kimawaka mtanatafuta maji ya kuuzima moto hamtoupata.
wana wana kissiwa mpaka kwenye pua te te teeeeee.
na nyinyi wa marekani ndo mliomlo chomo siri mpala ikafika bongo msiwasingiziye wa bongo,watu wa Maryland kwa unafiki ndo wenyewe tena wanaume ndo wamewazidi wanawake huko kwa uongo na umbe wao.
nimeishi huku na najua tabia zenu huko.
ndo imeshachotoka hiyo ikirudi pancha na hii comment ibaniye pia kama hamtaki watu wato comment si mzibe kama mlivyo fanya kwenye valentine day.
huu si uzushi ungekuwa uzushi usingetangazo bungeni na nyinyi mnasomaga ka blog hiki tu mliopo huku marekani njoeni nyumbani muone habari hizi zilivyo eneea.
pigeni miboksi yenu mkichoka nendeni kwenye party za minuso yenu haafu pumuliyeni kwenye blog ya lucas.
but mkitaka ukweli njoeni nyumbani mtajujua ukweli.
na usituite wabongo wazushi,kwani wewe si mzushi? umejuaje wenzako wazushi kama wewe si mzushi na mfagiliaji msafishaji wakuu? au si mbongo wewe? mwaaafyuuuuu!!!
Post a Comment