Advertisements

Thursday, March 5, 2015

B Fasso:Mwili wa Sankara kufukuliwa



Mwili wa aliyekuwa rais wa Burkina fasso marehemu Thomas Sankara kufukuliwa

Serikali Burkina Fasso imeagiza kufukuliwa kwa mwili wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Thomas Sankara .
Watu wa familia ya rais huyo wamekuwa na wasiwasi kuhusu utambuzi wa maiti ya kiongozi huyo wa zamani.

Mjane wa marehemu Miriam,akizungumza kupitia njia ya simu kutoka Paris amesema, kuwa ufukuaji wa mwili huo utafanywa kulingana na agizo la mahakama ili kusaidia katika kuwatafuta waliotekeleza mauaji yake.

Bwana Sankara aliuawa mnamo mwaka wa 1987 katika mapinduzi yaliomfanya aliyekuwa rafikiye na mshirika wake mkuu Blaise Campaore kuchukua mamlaka.

Blaise Campaore aliondolewa mamlakani katika mapinduzi ya kiraia mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita.

Serikali mpya inayoongozwa na Michael Kafando ,ilisema kuwa italiangazia suala hilo wakati ilipochukua madaraka.

Mwili wa Sankara ulizikwa katika kaburi lisilotambulika miongoni mwa makaburi yaliopo mashariki mwa mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

No comments: