Advertisements

Saturday, March 28, 2015

KASEJA KIVUTIO SIMBA


Kaseja kivutio Simba

Mara baada ya kocha Goran Kopunovic kumaliza mazoezi ya asubuhi wachezaji wa Simba walimvamia kipa huyo na kuanza kumsalimia huku wengine wakimtania

KIPA Juma Kaseja, leo amekuwa kivutio kikubwa kwa wachezaji wa Simba waliokuwa wakifanya mazoezi kwenye uwanja wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam UDSM.
Mara baada ya kocha Goran Kopunovic kumaliza mazoezi ya asubuhi wachezaji wa Simba walimvamia kipa huyo na kuanza kumsalimia huku wengine wakimtania.

Kaseja ameiambia Goal yeye ni mchezaji huru kwa sasa na alifika uwanjani hapo kwa ajili ya kufanya mazoezi lakini imemlazimu kusalimiana na wachezaji wenzake wa zamani kabla ya kuanza kijifua peke yake.

Licha ya kuondoka kwake lakini bado anamkataba na Yanga na timu hiyo tayari imeshamfungulia kesi kwenye mahakama ya kazi ikimlalamikia mchezaji huyo kuvunja mkataba na kutoroka kwenye klabu hiyo bila taarifa rasmi wakati anajua yeye ni mchezaji halali wa klabu hiyo.

No comments: