Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Balozi Liu Songtian (hayupo pichani). Balozi Liu na ujumbe wake wapo nchini kwa ajili ya kufuatilia masuala ya uwekezaji na maendeleo ya viwanda Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi tatu za Afrika zilizochaguliwa na China kwa ajili ya kuwa mfano katika uwekezaji na maendeleo ya viwanda. Nchi zingine ni Ethiopia na Kenya. Wengine katika picha ni Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto kwa Bal. Gamaha), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Mhe. Abdulrahman Shimbo (mwenye tai nyekundu), Balozi wa Tanzania nchini China na Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa EPZA.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Balozi Liu Songtian akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Balozi Gamaha na ujumbe wake. Kulia ni Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Yoqing
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Maalum ya Uwekezaji (EPZA), Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akitoa mada kuhusu maeneo maalum ya uwekezaji yaliyopo nchini kwa ujumbe kutoka China unaoongozwa na Balozi Liu
Balozi Gamaha (katikati), akiwa pamoja na Balozi Shimbo (kushoto) na Balozi Kairuki (kulia) wakifuatilia mada iliyowasilishwa na Bw. Simbakalia (hayupo pichani)
Bw. Simbakalia akiendelea kutoa mada huku wajumbe kutoka China na Tanzania wakisikiliza
Balozi Liu akimkabidhi zawadi Balozi Gamaha
Balozi Mbelwa akimkabidhi Balozi Liu zawadi ya majani ya chai na kahawa ya Tanzania Picha na Reginald Philip
No comments:
Post a Comment