Friday, March 13, 2015

WAZIRI CHIKAWE AKABIDHI PIKIPIKI 35 KWA MAKATIBU KATA WA CCM WILAYA YA NACHINGWEA LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya pikipiki Mwenyekiti wa Makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Nachingwea, Ally Napepa. Waziri Chikawe alikabidhi pikipiki 35 kwa makatibu kata wilayani humo kwa ajili kazi ya uendeshaji wa shughuli za chama ikiwemo kuwahamasisha wananchi katika kata zao kujiandisha ili kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekwa na Bunge, pamoja na kujiandaa na uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za CCM wilayani humo. Kulia ni Katibu wa CCM wilaya hiyo, Mussa Liliyo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kulia) akiwasisitiza Makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Nachingwea, kuzitumia kwa uangalifu pikipiki 35 alizowakabidhi kwa ajili ya kazi za uendeshaji wa shughuli za chama ikiwemo kuwahamasisha wananchi katika kata zao kujiandisha ili kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekwa na Bunge, pamoja na kujiandaa na uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za CCM wilayani humo. Picha zote na Felix Mwagara.

3 comments:

Anonymous said...

Asante. Wapenda Amani Tanzania tunaweza kuona matunda ya fedha iliyyochotea na wajanja ESCROW account! Mtandao ni mkubwa ndio maana Rugemalila hajaulizwa wala kukamatwa. Mpango mzito huu! Hiyo kura ya ndio ni wapi wananchi wameipotia katiba hiyo au ni ile iliyopitishwa na Sitta na kundi lake!!!

Anonymous said...

CHADEMA hakuna kampeni au kina Mbowe washakatiwa zao

Jay said...

Hiki chama kimelaaniwa kweli....yaani watu wanagawa pikipiki huu mwaka wa uchaguzi, je siku zote hizo walikuwa wapi? Maendeleo Tanzania hayataweza kuletwa na CCM hata iweje.