Advertisements

Thursday, March 5, 2015

Urais wa Zanzibar wanukia Pemba

Raisi wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein.

Zanzibar. Wakati Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec), ikitangaza ratiba ya Uchaguzi Mkuu, wanasiasa wenye asili ya Pemba wameamua kudhibiti nafasi ya urais Zanzibar baada wagombea watano kutoka kisiwani humo kutajwa kuwa na mipango wa kugombea, akiwamo Rais Dk Ali Mohamed Shein .
Kama wanasiasa hao watasimama kwenye dhamira hiyo na mmoja kuibuka mshindi, kisiwa hicho kitaandika historia mpya ya kutoa Rais katika vipindi viwili tangu uhuru wa Zanzibar mwaka 1964.
Marais waliowahi kushika wadhifa huo kupitia Chama cha Afro Shiraz Part (ASP), kabla ya kuungana na Tanu mwaka 1977 na kuzaliwa CCM, ni Rais wa kwanza Sheikh Abeid Amani Karume, Aboud Jumbe Mwinyi, Idrisa Abdulwakili, Dk Salmin Amour Juma na Amani Abeid Karume.
Wagombea waliotangaza nia hadi sasa ni Makamu Mwenyekiti NCCR Mageuzi, Ambari Khamis Haji, Katibu Mkuu wa Tadea, Juma Ali Khatibu, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Hamad Rashid Mohamed (ADC) na Dk Ali Mohamed Shein anayetajwa kutaka kuendelea na wadhifa huo.
Mchuano mkali unatarajiwa kuonekana kati ya Mgombea wa CCM, Dk Shein na Maalim Seif wa CUF kutokana na vyama vyao kuwa na ushindani mkubwa kisiasa tangu.
Uchaguzi wa mwaka 2010, Dk Shein alishinda kwa asilimia 51, huku Maalim Seif akipata asilimia 49 na kulazimika kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Mwananchi

No comments: