
Ni wazi kwamba ningependa siku moja watanzania waweze kujua ukweli
wa nini kinafanywa na matajiri wa nchi hii.Matajiri waliojaa ulafi wa kunufaika na rasilimali za nchi hii
kwa manufaa yao na familia zao ukijumlisha wapambe wao na washirika wa ndani na
nje ya nchi hii ya Tanzania. Ni katika vita hii ndio inayopelekea serekali yetu
kuyumba na kuyumbishwa (STATE TO BE CAPTURED) na hawa matajiri pale
wanapopigania maslahi yao na kudiriki kutumia utajiri wao na umiliki wao wa
vyombo kama vya Habari wanavyomiliki ili kuongeza kasi ya mapambano hayo ya
kudai maslahi yao . Ni kweli kabisa kwamba hawa matajiri wamejipanga kikamilifu
na kujipanga kwao kupo katika Nyanja tofauti sana lakini Nyanja zote
wanazotumia huwa wako makini sana na hivyo pia wanahitaji wananchi na serekali
makini kuweza kupambana na mipango yao hiyo michafu iliyogubikwa na hulka ya
ulafi na ubinafsi wa hali ya juu.Mipango hii ya matajiri katika kupambana
kuhakikisha wanapata maslahi yao inaanzia kwenye kutumia vyombo vya Habari
wanayomiliki wao wenyewe au washirika wao au zaidi ni vile wanavyovinunua ili
viweze kupeperusha ,kutetea na kuandika maslahi yao.Katika kufanya kwao hivi
huwa wanatumia vyombo vya Habari hivi kujaribu na kuhakikisha kwamba
wanaaminisha watanzania kwamba serekali inania ya kuwanyima kile wanachoomba na
kupendelewa watu wa nje au mashirika ya kiserekali. Wakiwa wanafanya hivyo pia
hujumuisha Habari na uzushi unaokuwa umelenga kutaka kupata huruma ya
watanzania kwamba hawa walafi waliojipa jina la wazawa wanaonewa na hivyo
watanzania wapaze sauti zao kuwatetea kwani watakapo pata kuvuna hizo
rasilimali manufaa yatakuwa kwa taifa lote .Loooo huu ndio uzandiki na unafiki
ambao wanawavika watanzania na kuwaaminisha na hii huwafanya kuwaaminisha
kwamba maslahi yao binafsi wanayopigania ni lazima watanzania wote washiriki
kuyapigania kwani ni maslahi ya taifa .Kumbe huu ni uuongo wa mchana kweupe kabisa
wa kusema maslahi yao yakitimia taifa nalo kwa ujumla litafaidika na hii
hupelekea watanzania kuanza kuwaona hawa matajiri kama watetezi wao kumbe
maskini watanzania hawajui kwamba ni bora shirika la serekali likahodhi uvunaji
wa rasilimali manufaa yatakuwa ya uma na sio kama wanavyoaminishwa na matajiri
walafi . Matajiri wanotumia vyombo vya habari vyao kugeuza maslahi yao kuwa
maslahi ya taifa.
Hii ndio hatari ya nchi yetu ilipofikia kwa hawa matajiri wa nchi
hii kujivika ngozi ya kondoo kumbe maskini wao ni chui . Nimependa sana
kuielezea hali hii nikuusisha na sakata la ugawaji wa vitalu vya gesi katika
nchi yetu.Ni wazi kwamba katika mchakato mzima wa kuomba vitalu hivyo vya gesi
katika maeneo ambayo gesi imegunduliwa katika mkoa wa Mtwara, tuliano
mashambulizi mengi ya hoja zilizokuwa zikiibuliwa na matajiri katika nchi hii
wakitaka serekali iweze kuwapa upendeleo. Ni katika vita hii ya kutaka
kupendelewa na serekali kwa wawekezaji wa ndani ndio iliyoweza kuibua mjadala
mrefu ,mjadala ulivikwa sifa ya kitaifa kumbe ulikuwa mjadala uliibuliwa na
matajiri wachache waliokuwa wakipigania maslahi yao lakini kwa ustadi wao na
utajiri wao wakaoufanya uwe ni mjadala wa kitaifa. Looo tukaona watanzania wanyonge
wakilalamika kwamba jamani mnaona serekali hii inawanyima wazawa fursa ya
kuchimba gesi na inawapendelea wageni .Huu ndio ulikuwa mwazo wa malumbano kati
ya serekali na watanzania matajiri na walalaahoi waliokuwa wamejazwa fikira
potofu kwamba watanzania matajiri wanabaguliwa na serekali hali yakuwa
wanauwezo.Nakumbuka hili jambo lilizuwa mjadala mrefu sana na midahalo mingi
iliyokuwa imesheheni kwenye majumba ,mashule ,maskani ya watanzania na hata
kwenye ofisi na taasisi mbalimbali .Ni kweli kwamba matajiri hawa waliokuwa na maslahi
yao binafsi waliweza kufanikiwa kuandaa safari hii ya mapambano kuona kwamba
rasimali iliyogunduliwa ya gesi inachangia katika kuongeza utajiri wao .
Kutokana na nia yao hii na uchu wao huo wa Kukuza pato lao lisilokuwa na
mahusiano yeyote ya kunyanyua hali ya maisha ya mtanzania wa kawaida aliyoko
kijijini anapambana na jembe la mkono alime kulilisha taifa hii na familia yake
. Kujipanga huko kwa matajiri kulianza kupanga safu ya waandishi wataokuwa
wakiandika Habari hizo za mapambano juu ya kufaidi hii rasimali iliyogunduliwa
na kupanga safu hata ya viongozi wa umma hususani wabunge kuweza kuwatetea na
kuwasemea. Mbali zaidi naweza kuongezea kwamba hii pia ilisaidwa na vyeo vyao
walivyonavyo katika taasisi ya Sekta Binafsi inayotetea maslahi ya tabaka
tajiri bila ya kuangalia maslahi ya kitaifa na maslahi ya mtanzania mnyonge au
mlalahoi.
Hii ndio ilikuwa pata shika nguo kuchanika katika taifa hili
matajiri wakiamini kwamba hapa bora punda afe mzigo ufike .Hii ni kiwa na maana
kwamba ata watu wakichukia serekali yao au amani ya nchi ikivurugika sawa
lakini wao lazima wahakikishe kwamba wanapata maslahi yao wanayopigania kwa
kutumia pesa zao nyingi na muda,ujuzi wao mwingi. Nakumbuka wazi kwamba mjadala
huu wa matajiri kutaka kupata upendeleo wa pekee kutoka serekalini
utakaowafanya wao kuvuna rasilimali hii ya nchi na kutajirika kutokana na
unyeti na umuhimu wa rasilimali hii ya gesi duniani na katika taifa letu hili.
Uchu huu ndio uliopelekea kuandikwa kwa taarifa za upotoshaji katika vyombo vya
Habari kama magazeti, mitandaoni na kutangazwa kwenye maredio na Televisheni. Taarifa
zilizokuwa zimejaa chuki na maneno ya kebehi kwa viongozi wa serekali na
mashirika ya serekali na serekali kwa ujumla.Yote haya yalikuwa hayafanywi kwa
bahati mbaya ila makusudi na yalifanywa
hivi ili kuona ni jinsi gani serekali itaweza kutishika na harakati hizi za
matajiri za kutaka maslahi yao yazingatiwe na yalindwe kwa njia yeyote ile.
Ukweli ni kwamba serekeli kwa ujumla ilitetereka nadiriki kusema ila jambo la
msingi ni kwamba mungu alitubariki sana kwa kutupatia kiongozi shupavu katika
serekali hususani katika sekta hii ya madini
na nishati naye si mwingine bali ni Profesa Sospeter Muhongo .
Ni wazi kwamba Profesa Sospeter Muhongo ndio kiongozi wa serekali
aliyekuwa akinyanyua mdomo wake mara kwa mara kupambana kwa dhati kabisa na
hawa matajri waliokuwa wanajaribu kutumia vyombo vya Habari na wabunge
kupigania maslahi yao,familia zao na washirika wao wa ndani na nje huku wakiwa
wamejivika sura na maneno ya kizalendo. Ukweli ni kwamba vita hivi vilikuwa
vikali sana kusema kweli kwasababu ni mtu mmoja ambaye alikuwa anapambana
kizalendo na jopo la mawakala wa rasilimali zetu na watanzania waliopotoshwa
kuhusu uvunwaji wa rasilimali ya gesi na hawa matajiri kupitia vyombo vya Habari
vyao na walivyovinunua pamoja na viongozi wa uma kama baadhi ya wabunge .
Nakumbuka mapambano haya ya matajiri wa ndani na mawakala wao yalifanyika huku
yakiwa yanajaribu kupandikiza chuki kwa watanzania kwa serekali yao na waziri
wao aliyekuwa amejaa hoja na uchambuzi
wa kizalendo . Hoja na uchambuzi wa maswala ya gesi uliokuwa umejaa uzalendo,
uwazi, uwajibikaji, utaalamu na uhalisia wa mambo yenyewe yanavyotaka na
ulivyo. Wapi bwana matajri walikuwa na kasi ya ajabu na maneno ya dhihaki na
kebehi huku yakiwa sambamba na hoja za kishabiki Mfano “Palizushwa maneno
kwamba waziri amesema mitaji ya matajiri ya watanzania ni ya kuwekeza kwenye
viwanda kama juisi tu ”. Haya yote
yalikuwa ni mapambano ya kuhakikisha kwamba matajiri wanapata maslahi yao waliojitoa
kwa hali na mali kuyapigania na wakiwa na imani na msimamo kwamba lolote na
liwe ila chetu kwanza taifa baadae. Mbali zaidi kwa lugha za mitaani vijana
wanasema “KAMA MBWAI MBWAI” .
Jambo pekee ambalo naishukuru sana taasisi ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam ni pale ilipoona kwamba kuna haja ya huu mjadala ukaja kujadiliwa
katika ukumbi wa chuo ukumbi wa Nkurumah. Huu ni ukumbi wenye sifa ya kitaaluma
ya kusheheni mijadala ya kitaifa inayosukumwa na utaalamu, uzalendo na ukweli. Ni
wazi kwamba jambo hili lilikuwa jema sana kwani iliweza kutoa fursa kwa
matajiri na upande wa serekali kutoa hoja zao na kuchambuliwa vizuri na wasomi
watanzania na watanzania wote kuona na kusikia na kuwezesha kuchambua ili
kuweza kupata muafaka .Nashukuru sana katika siku ile kwa upande matajiri
waliosimama kutetea upande wa matajiri waliojiita wazawa huku mimi nasema
matajiri wazawa wanaopigania maslahi yao ila wakajifanya wanapigania maslahi ya
taifa waliwakilishwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Dr. Regenald Mengi. Ni vema sana mana kwa
upande wa serekali uliwakilishwa na Waziri Mtaalamu wa Jiolojia,Profesa wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Sospeter
Muhongo ambaye kusema kweli kwake
ilikuwa yuko uwanja wa nyumbani waswahili wansema. Katika hali nzuri mjadala
uligubikwa na hoja zlizokuwa zimesheheni
utetezi wa maslahi ila maslahi tofauti.Lakini nipende kusema jambo moja ambalo
sikufurahishwa kabisa na kweli hii ilionesha kwamba matajiri wa nchi
wanapigania maslahi yao na sio maslahi ya taifa ni pale Mwenyekiti wa Sekta
Binafsi Tanzania Dr.Reginald Mengi pale alipotuambia watanzania na serekeali
kwamba katika kuhakikisha kwamba watanzania wanafaidika na rasilimali za nchi
yao na wanamiliki rasimali hizo na wanashiriki kikamilifu kuzivuna ili kuepuka
laana ya rasilimali . Alituasa na kusisitiza tuige mifano ya Nchi ya Nigeria na
Angola nchi ambazo uvunaji wake wa rasilimali unavunwa na matajiri wazawa.
Lakini huu ulikuwa mfano wa kusikitisha kabisa na waajabu ambao ulikuwa haupaswi
kutolewa na Mwenyekiti huyu tena ambaye ni Daktari kwa Elimu yake ikiwa na
maana kwamba amemaliza Shahada ya Tatu .Kusema kwangu kwamba ushauri wake ni
waajabu na sio sahihi hii ilithibitishwa na hoja zilizotolewa na waziri Profesa
Sospeter Muhongo, msomi aliyethibitisha utaalamu wake pale alipotoa hoja nzito
ambayo ni ya kweli naomba ni yaeleze kwa kuyasherehesha.
“Mwenyekiti wa TPSF anatwambia
watanzania na serekali yetu tuige mifano ya Nigeria na Angola kwenye
kumilikisha na kushirikisha wananchi wake (wazawa) kwenye uvunaji wa rasilamili
za nchi kwa manufaa lakini kwanini ametoa mifano ya nchi ambazo zinanuka rushwa
kwenye dunia ,na nikila mtu anajua kwamba nchi hizi zinanuka rushwa na hii
inadhihirika katika uvunaji wa rasimali zao kama mafuta .Mfano ANGOLA anayevuna rasimali ya mafuta na kuuza kwa
manufaa yao ni Rais Do Santos na mwanaye wa kike mwanamke tajiri Afrika
.Tukienda Nigeria ni familia za watu wachache wanaofaidika na uvunaji wa mafuta
.Ni wazi kwamba hatuwezi kuiga nchi hizi ambazo zinanuka rushwa na nchi ambazo
wananchi wake hawajafaidika na rasimali hizo .Ni wazi kwamba kama watanzania
tutaiga kwenye nchi hizo itakuwa ni maafa makubwa kwenye nchi yetu na balaa
kubwa ”
Hii ndio ilikuwa hoja ya
dhahiri kabisa iliyoonyesha kwamba hawa matajiri hawa katika swala hili la
kutaka fursa ya uvunaji wa rasilimali ya gesi katika nchi yetu ilikuwa ni
mapambano yalikuwa yamegubikwa maslahi binafsi ili ya yakavikwa ngozi ya uzalendo.
Yote haya yalifanyika wakijua kwamba matajiri watapata huruma ya watanzania
wanyonge kuwatetea wakiamini kwamba watanzania watawaona kama watetezi wao
kumbe ndio wadidimizaji kuliko serekali. Uthibitisho wa hilo ndio mana
Mwenyekiti wa sekta binafsi alidiriki kutuambia kwamba tuige nchi za Nigeria na
Angola ambazo zinanuka rushwa na ni matajiri ,familia zao na vibaraka wao wa ndani
na nje ndio wanaofaidika na uvunaji na biashara ya mafuta na kuwaacha wananchi
walalahoi katika lindi kubwa la umasikini na maisha magumu . Hii ikienda
sambamba na wao kula na kusaza na kufanya birthday party za wake zao kwa
kuwaita wasanii maarufu kama diamond Platinum ambaye amemlipa hela ambayo
angetumia kuwagaia watanzania walioshindwa kuwa na miatano ya kununua dawa au
hawajala au kufanya jambo lolote kwa watanzania maskini ,Umaskini unatokna na
utajiri wao hawa matajiri wanyonyaji wa wanyonge.
Kwa nyongeza niliguswa pia na hoja ya msingi na Waziri Profesa
Sospeter Muhongo kwamba huyu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi ni miongozi
mwa watanzania wanaomiliki migodi katika nchi hii ambayo wengi wao hawalipi
kodi katika nchi hii.Zaidi ya hapo ni kwamba anamiliki hekari za ardhi 5000
huku kuna watanzania wanalalamika kwamba hawana ardhi na yupo mtanzania
anayemiliki maekari mengi kama huyu ,huku bado akisema wazawa hawamiliki
rasimali .Kweli toka hapo nikaamini hakuna tajiri kwenye nchi hii anayepigania
maslahi ya taifa wala ya walalahoi kinachofanyika ni kujivika ngozi ya uzalendo
kumbe ni walafi wanaongozwa na kusukumwa na maslahi yao binafsi.
Naomba watanzania tujiulize hawa sekta binafsi wakiongozwa na
mwenyekiti wao ni kwanini walipigania wao wapewe upendeleo wa kupata vitalu
kwanini wasingesema vitalu hivyo lipewe shirika la serekali la TPDC ambalo
matunda yake yanarudi kwa umma wa watanzania. Hizo asilimia 10% wanazotaka
wapewe na wawekezaji wa nje katika asilimia 35% wanazochukua wawekezaji ni
kwanini kama ni kweli wazalendo ni kwanini hawakupiga kelele na kulia hizo
asilimia ziongezwe kwenye asilimia za TPDC ili kuongeza asilimia kutoka 65
watazochukua ziwe 75. Kwani naamini faida ya TPDC kama itasimamiwa vizuri
manufaa yatakuja kwa watanzania.Hata wakileta hoja kwamba serekali ya CCM haitoweza
kusimamia mbaka manufaa kuja kwa watanzania wote je ? wanataka kutuaminisha
kwamba wao hawaamini kwamba ipo siku nchi hii itashikwa na vyama va upinzani wanavyovisaidia kwa hali na mali ili
vije kulinda maslahi yao baada ya kuona CCM haiwapi.Kwa kumalizia zaidi kama
hawa matajiri wa ndani ni wazalendo na wanaoguswa na swala la ughali wa umeme
katika nchi yetu inayochochewa na kusababishwa na umeme unaozalishwa na mafuta
mazito ambayo ni ghali sana na yanaigharimu serekali mabilioni ya shilingi za
kitanzania kuwanunulia makampuni yanayozalisha umeme kama vile IPTL kwa sasa
PAP,SYMBION na AGRECO.Zaidi ya hayo makampuni yanayonunuliwa umeme pia serekali
inanua mafuta hayo mazito kwa baadhi ya mikoa ambayo haijaunganishwa kwenye
gridi ya taifa mikoa kama vile Kigoma na mingineyo.Ni wazi kwamba hawa matajiri
wangekuwa wazalendo wa kutosha ni kwanini wasingeishauri serekali iongeze
asilimia hizo kumi kufika 75 kitu ambacho kingeweza kutusaidia katika kupata
gesi nyingi ambayo ingeweza kutusaida kuzalisha umeme mwingi wa gesi na
kuepeuka gharama kubwa hii ya kununua mafuta mazito kwa mapesa mengi ya
kitanzania ambayo yangeenda kusaidia katika shughuli nyiongine za Maendeleo
kama afya,Elimu,miondominu ,kilimo na sekta nyingine yeyote nyeti kwa ajili ya
Maendeleo ya watanzania walalahoi na watanzania wote. Kwa mazingira hayo
inatuonyesha dhahiri kwamba hawa matajiri hawaguswi na uhaba wa umeme ambao kwa
sasa tunazalisha MG 841 kitu ambacho ni chache sana kwasababu kwa nchi tu kama
Norway yenye watu 4million wanazalisha MG 30000.Ni wazi kwamba kama matajiri
wangekuwa wazalendo na wapigania maslahi ya umma na sio yao wangeishauri
serekali iongee tena na wawekezaji waongeze asilimia kwenye zile 65 zitakazo
chukuliwa na TPDC shirika la umma kwa manufaa ya uma.Kumbe nilichokiona ndugu
zangu watanzania kwa hawa matajiri ni kwamba walitaka vitalu vya gesi wapate
(wapige) pesa nyingi kwa kuuza hiyo gesi kwa serekali na kwengineko wanapopajua
wao,familia zao na washirika wao wa ndani na nje ya nchi yetu inayotaka kuuliwa
kwa maslahi ya wachache hawa .Kiufupi hawa walitaka kuwa mawakala ila sio
wazalishaji na nashukuru Profesa Sospeter Muhongo aliwaambia ukweli bila ya
kungata maneno .Na kwenye hili kusema kweli tunahitaji kiongozi shupavu kama
yeye kwenye mazingira haya ambayo matajiri wa ndani na wa nje wanapambana
kupigania maslahi yao kwa njia mpaka za
haramu zilizojaa chuki,dharau,kebehi na dhihaka .
Nimalizie kwa kusema kwamba watanzania ni lazima tuwe makini sana
na hawa wanaojiita matajiri wazawa kumbe ni wasakatonge wazawa wenye kupigania
maslahi yao ili hujifanya na kujinadi wanapigania maslahi ya taifa na
watanzania wote kwa ujumla. Hawa ni
lazima tuwe nao makini sana kwani hawa ni hatari sana kwa mustakabali wa nchi
yetu na ustawi wa maisha ya watanzania wote kwasababu hawa wanaendeshwa na
falsafa ya “LIWALO NA LIWE ILA MASLAHI YETU NDIO KILA KITU” .Matajiri wa aina
hii ni hatari sana wanaweza kuingiza nchi kwenye misukosuko hata ya machafuko
ambayo yatasababisha maafa makubwa kwa walalahoi huku wao wakiwa wamepanda
ndege kwenda nchi za nje kunywa wiski na bia. Ni muhimu pia kwa serekali
kuchagua viongozi shupavu na wenye weledi wa hali ya juu wanaweza kupambana na
hawa matajiri wasiokuwa na uzalendo hata kidogo na wanaotumia mali zao
kupigania maslahi yao. Mfano wa viongozi wenye uwezo wa kupambana na hawa
matajiri walafi, wabinafsi na wasioitakia mema taifa letu na wananchi wake wote
tumeuona kwa Profesa Sospter Muhongo ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini
Mchapakazi na Mwaminifu na Mwenye kila sifa na uwezo wa kuingoza wizara ile
aliyokuwa anaiongoza na zaidi hata kuwa Rais wa nchi hii inayohitaji sayansi,
teknolojia na uvumbuzi wa hali ya juu kwa ajili ya kuchochea kasi ya Maendeleo
yetu yote.
Mwandishi wa Makala hii ni mimi Ismail Ramadhani .Muhitimu wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam shahada ya Sosholojia (Bachelor of Arts In Sociology
and specialized in Social Policy and Administration) mwaka 2014.
Nashukuru Mungu nimemaliza vizuri Profesa Wangu na nimeliza na
ufaulu wa G.P.A of 3.8 (Upper Second with Honours).
Ni miongoni mwa wachangiaji wa katika ule mjadala uliofanyika
Nkurumah Hall “Uliokuwa unajadili juu ya umiliki wa rasilimali kwa watanzania”
.Ni Yule kijana ninayeonekana nimevaa fulana ya nyeupe nikiwa nimeninginiza
kitambulisho shingoni.
Nashukuru sana nimeandika makala hii leo hii baada ya kusoma
makala yako ya “TANZANIA IJAYO: UFUGAJI WA KISASA NA BIASHARA KUBWA YA MAZAO YA
MIFUGO YETU” inayoonyesha kwamba wewe ni msomi ambae kama taifa litakutumia
vizuri hususani kwa ngazi kama ya Urais ukikosa kabisa uwaziri unaweza
kulivusha taifa hili mbali sana .Mbali sana ambako Watanzania wengi wanatarajia
kufika huko wakiamini kunaweza kunyanyua maisha yao yaliyoko kwenye lindi
maskini .
“Asante sana Mungu Mbariki Profesa Sospeter Muhongo , Mpe nguvu
,afya ,hekima ,busara ,ujasiri ,uzalendo ,ujuzi utakaomfanya aweze kugombani
urais wa nchi hii.Kama hatotaka Uraisi mpe moyo wa kugombania Ubunge hususani
wa Musoma na mjalie ushindi.Huku Mungu ukinajalia mimi kuwa katika timu yake
yakupigania na kushuhudia ushindi wake wa kishindo”.
Ameen
Asanteni Sana
Ismail Ramadhani
My Phone Number: o653 493732
Email: ramadhanimatemanga@yahoo.com
No comments:
Post a Comment