ZITTO AVULIWA RASMI UANACHAMA CHADEMA
Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa CHADEMA. Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama wa mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto baada ya mahakama kuu ya Tanzania kutupilia mbali shauri lake.
Katika maamuzi hayo ya Mahakama kuu ya Tanzania leo imetupilia mbali shauri lililofunguliwa na Mh Zitto Kabwe mwaka jana akipinga kikao cha kamati kuu ya CHADEMA kumjadili akikitaka chombo hicho cha sheria kukielekeza chama chake kusubiri kwanza rufaa yake aliyokua amekata Baraza kuu.
10 comments:
Nafikiri Chadema wanahitaji kufikiria kwa makini kuhusu maamuzi yao ya kumfukuza Zitto. Vipi Kama ni mbinu endeleza ya Ccm kuisambaratisha Chadema? Mind you, suala la Zito limekuwapo kwa muda Sasa kama nyote mnakumbuka Ccm waliitumia hii issue kushinda Viti vingi sana ktk uchaguzi mdogo wa wabunge na madiwani kama sikosei. Ni issue ambayo imeonekana kuwa na mafanikio makubwa kukigawa Chadema. Ninaelewa mambo yaliyokwisha semwa kuhusu huyu bwana kuwa ni msaliti, pengine ni kweli au la! Pia naunga msimamo wa chama kuwajibisha watu kama hao. Lakini nakataa notion ya kufukuzana ktk chama kwani it weakens chama(inadhoofisha). Hebu tuwe wepesi kujifunza kutokana na makosa rather than kurudia makosa. Demokrasia ya kweli inaruhusu rivaries ndani ya chama, kwani huo sio uadui. After all no body is perfect, we all make mistakes. So kwa mtazamo wangu, Chadema kitafute solution kumsamehe Zitto japo kwa adhabu nyingine sio kumfukuza. Make a reconciliation to bring him back for the sake of movement, sio tu mtaonekana kuwa nyie ni human but also mna lengo la pamoja kuikomboa Tanzania kotoka ktk rushwa na dhuluma iliyokithiri. Please don't buy on CCM propaganda, kwani ni Neema kwao kwenda Ikulu again!
Kama reconciliation itashindikana kwa namna yoyote ile, then let him decide kuondoka mwenyewe kulikoni kumfukuza. Kwa kufanya hivyo umma utamwona kuwa kweli hakuwa mwaminifu. Then Chadema wataweza kuwakeep most of his followers. Why I'm saying that??? Ni kwasababu ya "TIMING". In politics there is something called timing, kwanini jiulize huu uamuzi wa mahakama kwanini uje sasa hivi? Ambapo Ccm inaonekana kubanwa ktk masuala mengi yanayohusu jamii? Miezi Saba tu kabla ya uchaguzi mkuu? Kama majaji hao hao wanaweza kuchukua rushwa kwanini msifikirie kuwa huu ni mpango mahususi kuwamaliza opposition? Let's be critical thinkers instead of kukurupuka na maamuzi. Kwa mtazamo wangu, this is the time to raise above politics kwa kuongeza nguvu ya opposition badala ya kuendeleza mgogoro. For Mr Mbowe, this is your time to shine sir, be unpredictable leader, raise above politics by thinking of Tanzania future. Imagine the crowds when you announce bringing Mr Zitto back, it will be the end of Ccm and beginning of new chapter of our beloved country! Show that the opposition can by embracing one another!
Nawakilisha!
Well said.
Mdau hapa juu asante sana kwa kuliona hilo. Naimani kabisa hapa kuna mkono wa wahasimu wakubwa. na Chadema ni vyema kukaa chini na kuliona hili na kukaa meza moja na Zitto kuwela mkakati mpya kwa uchaguzi ujao?\!
Kwa heshima na taadhima CCM wasubiri 2035! 2015 hadi 2035 CHADEMA. Nchi itakuwa na watu wenye maendeleo, furaha, na amani. Ni ustarabu kuachiana hivo. Yapo mambo mengine ya kujenga taifa zaidi ya kuwania viti na madaraka katika vyama kisiasa au serikali.Uongozi bora ni nguzo lakini haina maana watu mkose usingizi kwa kukosa vyeo.Kuwa mjenzi wa Taifa si lazima uwe Waziri fulani su Rais fulani kutoka chama fulani.
You don't have to be in politics of power struggles in order to contribute effectively to your country.
bora kafukuzwa bana alikuwa anapiga deal na ma ccm na akapewa pesa nyingi sana na ccm ili akidhoofishe chama,walivyomshtukizia akakibilia mahakamani ndo wakamuokoa hao ma ccm but I reality katika chama alikuwa hayupo kabisa hawajamtaka kabisa ni nyoka hatari sana kama yule nyoka makengeza.
bora amefukuzwa ni msaka tonge ande akasaka tonge huko ccm. na mgao wa escrow yumo na yeye pia.
cha kushangaza watanzania sijui kwa nini tupo hivi ni nchi hii ya kipekea inayo wakumbatia mafisadi.
kiini macho eti tunapigiwa nyimbo za ngonjera za escrow wakati aliyegawa hizo pesa kapooo. anaulizi wakutoshaa hawezi kuguswa ask your self why?
na jiulize ndani ya chama huyu zitto hawamtaki kwa sababu hana uaminifu ni fisadi nyoka hatari ndumi la kuwili nyoka wa mdimuni.jeulize kwa nini mahakama imembeba na kumuweka kwenye chama bado?
this happens only in Tanzania.
na asepe na akisanzuwe na akitoe huko aende sasa kwa mafisadi wenzake wakale pesa za umma kwa raha zao bila kuguswa.
but ole wao hawana mkataba wa kudumu na mungu kuna siku watarudi kwa mungu wao na kuulizwa huu ufisadi walio wafanyia watanzania tena maskini za mungu wasio jiweza walala hoi mloo mmoja tu ni shidaaaa na wao leo wanawazulumu na kula mali zao.
Hivi kila kitu ni CCM???? Khaaaaaaaaaaaa THIS CLAIM DOES NOT MAKE SENSE AT ALL. Huko CHADEMA is the same story kila mtu anataka kuwa kiongozi
sisi m ni shidaaaaaaaaaaaaaaaaa.chezea ccm wewe.unajifanya mjuaji na msemaji wa wananji inakula kwako sasa.
pig deal,shiba na familia yako kwisha kazi wananchi wajitafutiye wenyewe kama sisi wapiga mabox huku ughaibuni.
aisee pole sana zitto wamekutosa kama walivyomtosa marehemu komba angalia sana wasiku dedishe tu.
Hivi nimegunduwa ni chama cha udini na ukabila siyo kama ccm Angalia jinsi mbowe anakula ajsfukuzwa zityo amekuwa staa sasa wamemfukuza mweeh hiki ni chama cha wenyewe siyo wanyonge kabisa chadema ni people power tena ya one person mr mbowe .Pole zitto but usijali chadema siyo tulivyofikiri ni chama cha wanyonge no ni chama cha mbowe na wengine sisi wanyonge siyo chama chetu .na huu ni wito kwa wote kwamba chadema ni chama cha upendeleo
Post a Comment