KAMPUNI ya Clouds Media Group imeendelea kuwa kinara kwa ubora wa SuperBrand kwa mara ya tatu katika nchi za Afrika Mashariki.
Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa Viwango Afrika Mashariki,Jawad Jaffer amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya watalaam wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ambao wanahaki ya kuamua aina ya haki ya viwango bora vya superbrands na kupongeza makampuni ambayo yamefanikiwa kuingia 20 bora.
Utafiti huo umefanywa na idara ya uchambuzi wa viwango makao makuu nchini Uingereza kutokana na kuzingatia ushauri wa wataalam wa masoko na maoni ya watumiaji bidhaa zaidi ya 600 wa huduma hizo.
Amesema kampuni nyingi zilizoingia katika ubora wa superbrands ni 1000 zikapambanishwa na kufanya kampuni 20 ziingie katika ubora superbrands na kufanya kampuni Clouds Media Group kuendelea kushikiria nafasi ya jsu kwa mwaka wa 2015 -2016.
Picha
ya pamoja ya baadhi ya makapuni binafsi waliopewa tuzo bora za
viwango,kutoka shoto ni Bi.Dorothy Mashamsham kutoka kampuni ya Mafuta
ya PetrolFuel,Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One Bi Joyce
Mhaville,Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group Bwa.Ruge
Mutahaba,Meneja Masoko Bwa. Elisa Ernest kutoka kampuni ya bima ya
Alliance Insurance.
Mkuu
wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana
Jawad Jaffer akiwa na baadhi ya viongozi wa juu wa kampuni ya Clouds
Media Group,kutoka kulia ni Mkuu vipindi wa Clouds FM Sebastian
Maganga,wa tatu ni Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji Ruge Mutahaba na
Mkuu wa kitengo cha huduma,Promosheni na Tamasha Clouds Media Group.Bi
Fauzia Kullane.
Mkuu
wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana
Jawad Jaffer akimkabidhi tuzo bora ya viwango Mkurugenzi wa Uzalishaji
na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba,kwenye hafla fupi ya
utoaji tuzo bora za viwango hizo
iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Mkurugenzi
wa Uzalishaji na Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza jambo na Mkuu
wa Kitengo cha Idara ya Uchambuzi wa viwango Afrika Mashariki,Bwana
Jawad Jaffer.
Mkurugenzi
wa Uzalishaji na vipindi wa Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba akiishukuru taasisi
ya SUPERBRAND East Africa mbele ya wageni waalikwa na waaandishi wa
habari kwa kutambua ubora wa kituo cha redio hiyo na kuipa tuzo bora za
viwango katika Afrika Mashariki kwenye hafla fupi ya utoaji tuzo hizo
iliyofanyika ndani ya hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Baadhi
ya Wageni waalikwa na wanahabari wakifuatilia jambo kabla ya utoaji
tuzo bora za viwanga a.k.a SUPERBRAND kwa makampuni binafis nchini
Tanzania.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akiwa amepozi na Mtangazaji wa ITV Bwa.Godwin Gondwe
No comments:
Post a Comment