ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 30, 2015

MPENZI WA MR NICE AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE, NICE ASEMA NDO MTOTO WAKE WA MWISHO

Mpenzi wa mwanzilishi wa style ya ‘Takeu’ Lucas Mkenda aka Mr Nice, amejifungua mtoto wa kike na kupewa jina la Nicole.

Mr Nice ambaye ni baba wa watoto wawili kwa sasa, Collin na Nicole, ameiambia Bongo5 kuwa Nicole ni mtoto wake wa mwisho ili aweze kuwatengezea maisha mazuri.
“Sasa hivi ni uzazi wa mpango, huyu kwangu ndo mtoto wa mwisho, kuzaa tu kama mbwa itakuwaje? mwishowe utashindwa kuwatengenezea maisha mazuri,” alisema Nice.

1 comment:

Anonymous said...

wewe usijifanye mpangaji wa maisha wewe,wewe zaa tu bwana mungu ndo mpangaji,kama hayo maisha hujajalia kuwatengenezea utasemaje?we zaa tu acha mchongo. kwani wewe ndo umewauba muumbaji si yupo.zaa wewe.acha hizo.