ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 27, 2015

TASWIRA ZA ZARI NA DIAMOND WALIVYOJIACHIA VISIWANI ZANZIBAR

Diamond akilibusu tumbo la mpenzi wake Zari ambaye ni mjamzito.


Mwanamuziki Nasibu Abdul 'Diamond' akijiachia na mpenzi wake Zarinah Hassan 'The Boss Lady' Visiwani Zanzibar.
Zari na Diamond wakizidi kula maisha huko Zanzibar walipokwenda kwa ajili ya shoo iliyofanyika Juni 25, mwaka huu.

STAA wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul 'Diamond' na mpenzi wake Zarinah Hassan 'The Boss Lady' wamezidi kuonyesha kuwa penzi lao linazidi kuimarika baada ya Zari kuachia picha Instagram wakiwa 'close' walipokwenda Visiwani Zanzibar juzi.

Wapenzi hao walikuwa Zanzibar kwa ajili ya shoo ya Diamond iliyofanyika Jumamosi (Aprili 25, mwaka huu) usiku huko Ngome Kongwe.
Mojawapo ya picha za wapendanao hao imbayo imeenea mitandaoni ni ile ambayo Diamond analibusu tumbo la Zari mwenye ujauzito unaodaiwa kuwa wa staa huyo.
CREDIT:GPL

1 comment:

Anonymous said...

haya haya kumekucha mmependeza wapendanao tunakutakieni mtotoo mwema mwenye kheir na mfunze dini yenu na adabu na mila za kinyumbani msimfanye aje kupotoka kama watoto wa mastar.