ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 6, 2015

BARUA NZITO WEMA KUNA KITU CHA KUJIFUNZA KWA‭ ‬ZARI‭!

‬Beutiful Onyinye‭, ‬Wema Sepetu‭ ‬‮!‬'Madam'.

Dhamuni la barua hii ni kutaka kukushauri kwamba unaweza kujifunza kitu kutoka kwa mpenzi wa sasa wa aliyekuwa mpenzi wako‭, ‬Nasibu Abdul‭ ‬‮!‬'Diamond‭, ‬Zarinah Hassan‭ ‬‮!‬'Zari!

Naomba usinielewe vibaya‭. ‬Sina nia ya kukupambanisha wala kutaka kukukejeli kwa namna yoyote‭. ‬Kuna kitu kidogo tu cha kujifunza‭ ‬kutoka kwa binti huyo wa Kiganda‭.‬
Achana na maneno yanayosemwa mtaani‭, ‬kila mmoja ana upungufu wake lakini binadamu tunashauriwa kuiga yale mazuri kutoka kwa wenzetu‭.‬

Iko hivi Wema‭, ‬wewe na yeye mna nafasi moja nzuri katika jamii‭. ‬Nyinyi ni maarufu‭. ‬Mnapendwa na watu kupita maelezo‭. ‬Mna ushawishi mkubwa sana katika jamii hivyo mnaweza kufanya jambo na likapata mafanikio makubwa sana‭.‬

Umaarufu wenu ni biashara‭. ‬Kwa nini uendelee kubaki chini wakati umezungukwa na fursa kibao‭? ‬Umaarufu wako ni biashara kama utaamua kuwa‭ ‬‮!‬٪serious‮!&‬‭ ‬na kila hatua unayoipiga‭.‬
Nikwambie ukweli bila unafiki‭, ‬unapaswa kuiga jambo moja tu la msingi kutoka kwa Zari‭, ‬kuwekeza na kuheshimu fedha‭.‬

Mwenzako anaijua fedha‭. ‬Anajua namna ya kuitafuta na namna ya kuiwekeza katika maeneo ambayo yatazidi kuzizalisha‭. ‬Akili yake inawaza pesa na si starehe zisizokuwa na msingi‭.‬
Mfano mdogo tu ni‭ ‬‮!‬٪idea‮!&‬‭ ‬kama ya All White Party aliyofanya Zari kule Uganda‭. ‬Alifanikiwa‭, ‬anaendelea kufanya na wiki iliyopita aliifanya pale Mlimani City jijini Dar na kupata mafanikio makubwa‭.‬

Kwangu mimi kile ni kitu kikubwa sana ambacho kinaingiza fedha nyingi kwa wakati mmoja‭. ‬Si vibaya kama utaiga vitu vya namna hiyo‭. ‬Nisikufiche‭, ‬nafasi ya umaarufu uliyonayo Kibongobongo‭, ‬unaweza kufanya zaidi ya shoo ile kama utaamua na kupata watu wazuri‭ ‬wa kufanya nao kazi‭.‬

Na unapofanya mambo makubwa kama hayo‭, ‬lazima pia udhibiti matumizi yako‭. ‬Starehe zipo lakini wakati mwingine unapaswa kuheshimu‭ ‬fedha‭. ‬Yale mambo ya kwenda kuzimwaga ukumbini eti kuwa kama kina pedeshee‭ ‬‮!‬٪nanilii‮!&‬‭, ‬si mazuri‭.‬

Jeuri ya fedha ifanye kwa kufungua miradi mikubwa ambayo hata utakapozeeka utainjoi matunda yake‭. ‬Kuigiza kuna mwisho‭, ‬huwezi kuwa mwigizaji milele‭, ‬kuna wakati utatakiwa kuwa msimamizi wa miradi yako tu binafsi na mkono uende kinywani kiulani tu‭.‬

Usikubali kushikiwa akili na wapambe‭, ‬unayoshauriwa na wapambe yachuje maana si yote yanakuwa na manufaa‭. ‬Tumia kipaji na jina lako vizuri‭, ‬una nyota ya kupendwa basi kupendwa huko kuwe na faida‭.‬
Natambua una idea zako ambazo tayari umeanzisha kama kipindi chako cha In My Shoes‭, ‬usiishie hapo fanya makubwa zaidi‭.‬
Kwa leo acha niishie hapo‭. ‬Ni matumaini umenielewa‭.‬
Wasalaam

GPL

No comments: