Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Mavanga wilayani Ludewa muda mfupi baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya Tsh milioni 40 katika kijiji hicho.
Viongozi wa Kijiji cha Mavanga akiwemo mwenyekiti wa kijiji, Bw. Hilmar Mpambichaka (Chadema) kulia wakipokea misaada ya vifaa vya ujenzi toka kwa mbunge Filikunjombe kushoto.
Mbunge Filikunjombe akifurahia jambo wakati mkazi wa Mavanga akimtaka kuwa mbunge hadi atakapochoka yeye.
Mwanahabari wa kituo cha Radio Best Ludewa Deo Nyoni akiwa makini kufuatilia matukio
Wananchi wa Mavanga wakiwa wamebeba kitanda cha kujifungulia wanawake wajawazito kilichotolewa na mbunge Filikunjombe kitanda chenye thamani ya Tsh milioni 5.2
Mwenyekiti wa kijiji Cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akimpongeza mbunge Filikunjombe kwa misaada yake
Paroko wa kanisa la Anglicana kushoto akipokea msaada wa bati 300 kutoka kwa mbunge Deo Filikunjombe
Mwenyekiti wa kijiji cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema )akiwa amepokea msaada wa Darubini toka kwa mbunge Deo Filikunjombe
Mbunge Filikunjombe akipokea zawadi ya mbuzi toka kwa vingozi wa kanisa la Anglicana baada ya kuwasaidia bati 300 za ujenzi wa kanisa
Mbunge Filikunjombe akicheza mpira na wanafunzi hao baada ya kuwapa msaada wa mpira na sukari kwa mwaka mzima
Wasanii wa ngoma katika kijiji cha Mavanga wakishiriki kupiga ngoma na mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kushoto
Mbunge Filikunnjombe na katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw Mgaya wakicheza ngoma Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe asema baadhi ya wabunge ,mawaziri na watendaji wabovu serikalini wanakichafua chama cha mapinduzi ( CCM )Filikunjombe alisema kuwa Ccm ni chama makini na kinachopendwa sana ila shida ipo kwa baadhi ya watu waliopo ndani ya Ccm na serikali ni bomu
mbunge huyo alitoa kauli hiyo leo katika kijiji cha Mavanga wakati akijibu maswali ya wananchi na viongozi wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi ( Ukawa) kuhusiana na Ccm kuwateulia wananchi viongozi wasio na sifa kugombea nafasi mbali mbali.
Alisema kama kila mmoja angetimiza wajibu wake katika nafasi yake hakuna mpinzani ambae angechaguliwa ila kuchaguliwa kwa wapinzani ni kushindwa kwa wale waliowaamini kutoka Ccm kushindwa kuwajibika kwa wananchi waliowaamini
Filikunjombe alisema atakuwa mbunge wa mwisho kunyoshewa kidole na watanzania wakiwemo wananchi wake wa Ludewa kwa kushindwa kuwatumikia wananchi na chama chake cha Ccm .
Kwani alisema hakuomba ubunge kwa ajili ya kujinufaisha binafsi ila aliamua kugombea ili kuwatumikia wana Ludewa kwa kuwapelekea maendeleo hivyo Kazi Yake kwa sasa hadi mwisho wa ubunge wake ni kuleta maendeleo kwa wananchi wake na kuona ahadi zake zinatimia kwa muda uliopangwa na si kujinufaisha kwa wakati.
" Naomba kwanza mtambue kuwa wabunge wote tulipo fika bungeni kwa mara ya kwanza tulikopeshwa Tsh milioni 90 kwa ajili ya kununua gari la kutembelea na Mimi kwa kuwa nilikuwa na gari pesa hizo niliamua kununua gari la wagonjwa Mlangali ambao hawakuwa na gari la wagonjwa ....lengo langu kutumikia wananchi na kuwatatulia kero zao si vinginevyo"
Akielezea msaada huo wa vitu mbali mbali vyenye thamani ya Tsh milioni 40 alivyotoa alisema ni pamoja na kitanda cha kujifungulia wajawazito chenye thamani ya Tsh milioni 5.2,Darubini ,pesa ya taslimu Tsh milioni 1 bati zaidi ya 500 ,rangi debe 20 ,saruji zaidi 525 na vifaa vingine vingi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa miradi mbali mbali ya kijiji na ujenzi wa makanisa,shule na wodi la wazazi
Awali viongozi ukawa wa kijiji cha Mavanga kata kata ya Mavanga walimpingeza mbunge Filikunjombe kwa kuwa mbunge wa mfano Ludewa japo wapo viongozi wengi ndani ya chama chake ni wabovu.
Mwenyekiti wa Ukawa Mavanga John Mligo akishukuru kwa msaada huo wa vifaa na fedha toka kwa mbunge Filikunjombe alisema kama wabunge na viongozi wote wangefanya kama Filikunjombe kamwe wananchi wasingechukia chama hicho.
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti huyo wa Ukawa na mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Mavanga Bw Hilmar Mpambichaka ( Chadema ) walisema wao kama viongozi wa upinzani hawana shaka na uwakilishi wa mbunge Filikunjombe ndani ya jimbo hilo na nje ya jimbo hilo
" Tumekuwa na wabunge 7 ambao wametangulia kabla ya Filikunjombe ila uwakilishi wake umekuwa wa kuigwa na wabunge wengine na kama wabunge kote nchini wangekuwa watendaji hivyo huenda upinzani nchini usingekuwepo"alisema Mligo
Kwani alisema kuwa Chanzo cha kijiji hicho kuchagua mwenyekiti wa Serikali ya kijiji kutoka Chadema ni baada ya viongozi wa ccm kuonyesha kuwa mbali na wananchi na baadhi Yao kutafuna pesa za michango ya wananchi .
Bw Mligo alisema shida ndani ya Ccm ni vita ya wenyewe kwa wenyewe ndio ambayo imekuwa ikiwachanganya wananchi na kujikuta wananchi wanaingia katika mgawanyiko na kuchagua wapinzani
Alisema wakati wa kampeni hata wasio na sifa wanataka kuchaguliwa kwa kutumia rushwa ,hivyo kutaka kwa Ludewa kutambua wazi mbunge anayekubalika ni Filikunjombe pekee na kuwa hawahitaji mtu zaidi ya mbunge wao aliyewavusha katika maendeleo
Huku mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bw Mpambichaka akiwataka wananchi wa Ludewa kuacha kuonja sumu kwa kubadili wabunge na kuwa utendaji wa Filikunjombe hakuna wa kumfananisha nae
Alisema kuwa wamepata kushuhudia utendaji wake ndani ya bunge kupitia kamati ya PAC kwa kupambana na ufisadi kupitia Escrow na kuwafanya mawaziri zaidi ya watatu kujiuzulu
Pia kupitia utendaji wake ndani ya jimbo amefanikiwa kuwavuta wana Ludewa ambao siku zote walikuwa wakiona aibu kuweka wazi kuwa ni wakazi wa Ludewa na badala Yake kudanganya kuwa wao ni wazaliwa wa Mkoa wa Ruvuma kutokana na awali Ludewa kuwa nyuma kwa maendeleo .
" Toka Filikunjombe ameingia madarakani mwaka 2010 na kuwepo kwa kasi ya maendeleo ndio tunashuhudia wana Ludewa wakirejea Nyumbani na kujitangaza kuwa wao ni wakazi wa Ludewa tofauti na zamani wengi walikuwa wakijificha kwa aibu "
Hata hivyo alisema wapo wabunge ambao wamekaa majimboni muda mwingi kama akina Mzindakaya huko Sumbawanga ila siku zote ni mtu wa kueleza jinsi alivyofanya Kazi na Mwl Julius Nyerere ila si kujipambanua namna gani alivyoleta maendeleo jimboni
Kuhusu misaada mbali mbali iliyotolewa na mbunge huyo kijijini hapo mwenyekiti huyo alisema kwa mara ya kwanza toka wabunge 7 waliopita kijiji hicho kimepata kupata misaada mingi kutoka kwa mbunge
1 comment:
Eti wabaya watu sasa chama si kina watu na ndio hao wanachama, bila watu chama kitatokea wapi?
Post a Comment