Huu ndio Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, mahali ambapo mchana huu, Waziri Msitaafu Edward Lowassa atatangaza nia yake ya kuwania urais wa awamu ya tano.
Muonekano wa UWANJA wa Sheikh Amri Abeid, Arusha watu wamefurika kusikia atakachosema Edward Lowassa akitangaza nia ya kuwania urais mchana wa leo.
Wasanii watakao kuwepo katika safari ya matumaini leo Kadija Kopa, Ney wa Mitego na wengine wa mkoani hapo watakuwepo ili kuonyesha mshikamano .
Maandalizi yamefanyika vizuri na ulinzi umeimarishwa hivyo ni vyema. Kutangaza nia kwa Lowassa ni neema kwa wakazi wa Jiji la Arusha kwani hoteli karibu zote za Arusha zimejaa.
1 comment:
Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo mwanasiasa aliyejiuzulu kwa kashfa anaitwa aliyejiuzulu. Jamaa anaitaka Ikulu at any cost. Hizo pesa atazilipaje?
Post a Comment