
Hatimaye
mgogoro wa ardhi wa zaidi hekta 200 baina ya wananchi wa chasimba na uongozi wa
kiwanda cha saruji cha Twiga umemalizwa na waziri wa nyumba na maendeleo ya
makazi Mhe.Wiliam Lukuvi akitangaza kubadili matumizi ya ardhi hiyo kuwa ya
makazi yao kutoka mikononi kiwanda kama eneo la kuchimba madini.
Waziri
Lukuvi ambaye ameandika historia katika mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka
15 alifuatana na uongozi wa kiwanda,manispaa Kinondoni,Tanesco,mbunge wa kawe
idara ya maji,piolisi na timu yake ya wizara akigiza eneo hilo kupangwa kama
makazi ya wanachasimba ikiwemo miundombibnu ya maji barabara, shule,zahanati na
huduma nyinginezo za kijamii.
Aidha
Mhe.Lukuvui aliyeahidi kumaliza migogoro sugu nane katika jiji la Dar es Salaam
pamoja kueleza kuutambua mgogoro huo tangu akiwa mkuu wa mkoa alikiri kushindwa
kuingilia kati kutokana na sabambu mbalimbali na hatimaye kufikia nafasi ya
dhamana ya wizara hiyo na kuamua kutimiza adhima ya serikali ya kuhudumia
wananchi huku mbunge wakawe Mhe.Halima Mdee akikiri hatua iliyochukuliwa kuwa
muafaka kwa serikali yoyote inayojali watu wake.
Kwa upande
wake mkurugenzi wa kiwanda cha saruji cha Twiga Bw. Alfonso Rodrigoz pamoja na
kukiri mgogoro huo kuwanyima usingizi kwa kipindi kirefu amempongweza waziri
lukuvi na kuwataka wananchi kuanza ujirani mwema kwa maendeleo akiahidi
kusaidia katika ujenzi wa miundombinu.
CHANZO: ITV TANZANIA
No comments:
Post a Comment