ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 14, 2015

MH. STEPHEN WASIRA AJIVUNIA REKODI YA UADILIFU KATIKA MBIO ZA URAIS

Waziri wa kilimo, chakula na ushirika Mh. Stephen Wassira amesema kuwa rekodi yake ya uadilifu katika utumishi wa serikali, kutohusishwa na vitendo vya rushwa na ufisadi pamoja na malezi mema aliyolelewa na hayati baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere tangu akiwa kijana ni mambo yaliyomsukuma kutangaza nia ya kugombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi ili kuwatumikia wananchi ambao wanakabiliwa na changamoto za umaskini.
Mh.Wassira ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi – CCM na mmoja wa makada 31 ambao mpaka sasa wametangaza nia ya kuwania urais kupitia chama hicho ameyasema hayo mjini Bukoba mkoani Kagera wakati akizungumza na wana – CCM waliojitokeza kumdhamini katika kinyang’anyiro cha kusaka urais ambapo amesema ameamua kugombea nafasi hiyo kwa sababu anajua vizuri matatizo ya watanzania kutokana na kuwahudumia kwa muda mrefu tangu wakati wa rais wa kwanza mwalimu Julius Nyerere na kudai kuwa hana kashfa yoyote ya rushwa.

No comments: