Advertisements

Wednesday, June 3, 2015

MWILI WA MAREHEMU EUGEN ELISHIRINGA MWAIPOSA KUAGWA LEO KATIKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA

 

Marehemu EUGEN ELISHIRINGA  MWAIPOSA

TANZIA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Mhe. EUGEN ELISHIRINGA  MWAIPOSA  kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 2 June 2015 nyumbani kwake Dodoma ambako amekuwepo kushiriki Mkutano wa Bunge la Bajeti.

Mwili wa Marehemu unaagwa leo tarehe 3 Juni 2015 kuanzia saa 4 asubuhi katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, na baadaye mwili kupelekwa nyumbani kwake Ukonga, Dar es Salaam.

BWANA alitoa, BWANA ametwaa. Jina la BWANA  lihimidiwe. Amina!

No comments: