ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 1, 2015

WANAWAKE NCHINI UGANDA WAANDAMANA WAKIWA UCHI

Wanawake wa jamii ya Ancholi 'wakigalagala' chini huku wakiwa uchi kama ishara ya kumlaani adui....Wakiendelea na maandamano huku wakiwa uchi.
Maandamano yakipamba moto.
Magdalena Alum, mkazi wa eneo hilo.
Karamela Anek, akisema wataendelea na maandamano kutetea haki yao.
John Makombo ambaye ni Mkurugenzi wa mamlaka ya wanyamapori nchini Uganda (UWA).

Jamii ya Apaa walisema, ikiwa mgogoro huo utaendelea, zaidi ya watu 21,000 watakumbwa na madhara ya mgogoro huo.
Sehemu ya eneo lililo katika mgogoro huo.

Wanawake wa kabila la Ancholi kijiji cha Apaa kilichopo Wilaya ya Amuru, Kazkazini mwa Uganda wamefanya maandamano jana wakiwa uchi kutokana na mgogoro wa ardhi kati yao jamii yao na utawala wa eneo hilo mgogoro ambao umeendelea kwa takriban miaka 10 sasa.

Siku chache kabla ya maandamano hayo, Mawaziri wa serikali na watafiti walifika eneo la kijiji hicho na kujadili wakipanga kukata sehemu ya ardhi katika kijiji hicho cha Apaa, kitendo hicho kilizua hisia tofauti kwa wakazi wa eneo hilo ndipo wakaamua kupanga maandamano hayo.

Wakati wa maandamano hayo, mbele ya maofisa wa serikali na jeshi la polisi, wanawake hao walianza kuvua nguo moja baada ya nyingine, huku wengine wakitoa machozi kuonesha hisia zao za kuteseka kwa muda mrefu kufuatia hisia hizo. Lengo ikiwa ni kufikisha ujumbe kwa wahusika ili walishughulikie suala hilo na jamii ya Ancholi ipate haki yake.

Walisikika wakilia kwa kusema, "Lobowa, Lobowa!" maana yake ‘ardhi yetu’ katika kabila lao.

Utawala wa wanyama pori nchini Uganda unaamini kwamba jamii ya Ancholi wamevamia ardhi ya uhifadhi wa wanyama pori huku wakazi hao (jamii ya Ancholi) wakidai kwamba ardhi hiyo ilikuwa ya mababu zao.

Taarifa zinadai kuwa watu wengi wa kijiji hicho wameuawa tangu mgogoro huo uanze hivyo kuisababishia jamii hiyo kukoswa nguvu kazi huku wakitetea ardhi yao ya urithi wa mababu zao.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa katika kabila la Acholi inaaminika kuwa, mwanamke anapovua nguo na kubaki ‘utupu’ ni zaidi ya kupigana kwa kuwa inatoa laana kwa mpinzani wake.
NA BBC

No comments: