Advertisements

Wednesday, July 29, 2015

DINA MARIOUS NA ZAMARADI MKETEMA WATUPIANA MANENO INSTAGRAM, KISA KIKO HAPA.

Kumekuwa hakuna maelewano mazuri katika ya watangazaji hawa wawili baada ya Dina Marious kusimamishwa kazi katika radio hiyo.


Katika Mtandao wa Instagram Dina Marious ameandika kwa kirefu kabisa kuhusu inshu hii, akiwa kama anamzungumzia Zamaradi, Dina ameandika “Leo nimeguswa kuongea na SNITCHES makazini na maofisini a.k.a boss little pet.

Kuna siku kuna dada alinipigia simu nimshauri namna ya kuishi na mtu ambae wako karibu kazini lakini amekuwa akimsitch kazini anapeleka maneno ya umbea kwa maboss juu yake.Tukaongea lakini hivi majuzi nimeongea nae tena ananiambia aliamua kuacha kazi kwa sababu boss mpelekewa maneno amekuwa mwiba kwake hana raha na kazi.


Jamani huko maofisini na makazini hata kwenye vibarua vya wenyewe kuna watu wambea jamani.Yaani ni wambea,waongo,wachochezi,wanakazi ya kuchukua habari za wafanyakazi wenzao na kuwapelekea maboss.Ili nini??ili iweje??kwamba wewe boss akupende sana??ni tabia mbaya na inatia kinyaaa yakhiii!! Na kwa uchunguzi wangu hawa watu utendaji wao kazini huwa mbovu,hawana lolote,hana cha ziada cha kumuweka kazini hivyo anatumia usnitch kupalilia kibarua chake kazini.

Sifa kubwa ya mtu huyu ni kujifanya anaupendo na kila mtu ofisini,ana ukaribu na kila mtu na maboss ni washikaji zake kinoma noma.So in btn anafanya umbea fulani hivi,kafanya hivi,kasema hivi yaani yeye ni reporter inshort.Na ofisini wanakujua ila wanakusikilizia wanachukua tahadhari juu yako japo wanacheka na wewe ila wanajua wewe ni bosses little pet….pyuuuuuu!

Hii ni tabia mbaya sana hivi huwezi kusimama wewe kama wewe na uwezo wako kazini mpaka uwe snitch kwa wenzako??usidhani maboss wanakupenda kwa wewe kuwa snitch wanakutumia tu na wanajua udhaifu wako na pia wanajua wewe sio mtu mzuri ila wafanyeje maadam ndio kazi unayoimudu hapo ofisini.
Eti kazini kwenu mnae huyu boss little pet?mnadeal nae vipi?je wewe unaesoma hapa ndio kazi hii unayoifanya kazini kwenu?shame on you.EMBU jitume kazini fanya kazi acha usnitch na kuwa kanyau ka maboss!!”.
Baada ya muda mfupi Zamari akawa kama kamjibu hivi! Zamaradi ameandika “This is SO SAD…. Nimekaa kimya muda mrefu sana.. Nafkiri ni MUDA wa kutoa tamko kuhusu hili… Hata UONGO unaponyamanziwa sana huonekana kuwa KWELI…. I AM SOOOOOOOOOO TIRED OF THIS kutoka moyoni….. nimechoka nimechoka nimechoka!!!! Binadamu anaweza kukupaka ubaya wa AJABU na dunia nzima ikaaminishwa tu kuwa ndio kilichopo… nilikaa kimya kwa sababu sikulichukulia kwa UZITO but mpaka inafikia napost vitu vyangu watu wananifata kunitukana bila sababu kwa kuona namjibu Dina kwa anayoyaandika KWELI!!!!!?????? AISEE.. naandika hapa huku mikono inatetemeka kwa Uchungu na Hasira!!! Hakuna kitu kibaya kama KUPAKWA UBAYA USIOKUWA NAO… muda si mrefu LEO HAITAISHA ntatoa yangu ya moyoni… NIMECHOKA KIUKWELI na naona KIMYA CHANGU KINATAFSIRIWA TOFAUTI.. SIWEZI TENA.”

2 comments:

Unknown said...

fanyeni kazi si kutafutana kati yenu kama kile alicho post mwenzako kinakugusa hacha ,umbea si mzuri hacheni kabisa ni sifa mbaya tena sana ,

Unknown said...

Enter your comment... pole sana dina