
Mmoja wa watoa maoni anadai hana imani tena na mwanamke kwa sababu aliwahi kutendwa vibaya na msichana aliyempenda kwa dhati.Kwako mtoa maoni na wengine, kuumia na kuumizwa katika uhusiano ni jambo la kawaida sana, sema inakuwa ngumu kuukubali ukweli.
Dickson Julius wa ‘Wasafi Classic’ Sengerema, Mwanza:
Ninashukuru sana kwa mada zenu zinatufundisha mengi kuhusu uhusinao.
Simwamini mwanamke yeyote hata kidogo kwa sababu nilishawahi kuumizwa na msichana ambaye nilimpenda ambaye alikuwa mchepuko ile mbaya, mpenda fedha, hatazami sura wala tabia na hakuwa na mapenzi ya dhati.
Alipenda sana kusema ‘mapenzi pesa maua mpelekee nyuki’. Nashukuru niliachana naye na kwa sasa nimempata msichana mwingine ila nahisi hata yeye atabadilika kama wa mwanzoni.
INA KAPUNI
Nimeachwa na mume wangu kwa sababu ya kumkanya asitumie vilevi kama vile bangi, mirungi na pombe, hiyo ndiyo sababu iliyonitoa kwenye ndoa yangu, niko njia panda naombeni msaada wenu.
JINA KAPUNI
Wakati sijawa na msichana ninayempenda, wasichana wengine walikuwa hawanifuatifuati na kunitamani ila kwa sasa nimempata mmoja ninayempenda lakini kila siku wasichana wananisumbua.
Nawapongeza sana kwa ushauri wenu kwa sababu nimepata mafundisho, nimejifunza mengi kutoka kwenye safu hii.
FRANK WA KITUNDA, DAR
Mungu awabariki kwa mada zenu zenye mafunzo ndani yake.
Mtazamo wangu, hakuna mtu asiye na kasoro na ninavyojua kasoro zinarekebika, sema tu wengi tunakuwa na tamaa, lakini upendo wa kweli ni kutoka moyoni, kama hautakuwa na imani utakuwa kila siku ni mtu wa kutamani tu kila mpenzi mpya. Kwa mfano mimi mwenyewe mpaka sasa hivi nimeona bora niishi bila mpenzi maana kila ninayempata hana imani na penzi la dhati.
LUCY EMMANUEL WA MWANZA
Niliipenda sana mada ya wiki iliyopita. Kabla ya kuachwa unapaswa ujiulize kwanza, wengine wanakuwa na viherehere na kukurupuka kutafuta mpenzi mpya ili kumuumiza roho aliyemuacha ndiyo maana wengine wanaangukia pua.
DONATILLA AU TILLA WA MBEYA
Nafurahishwa sana na mada zetu za XXlove, tafadhali endeleeni kutuelimisha.
Hii ni sehemu ndogo tu ya maoni hayo lakini tunasema asanteni kwa maoni yenu. Tukutane wiki ijayo kwenye mada nyingine murua.
GPL
No comments:
Post a Comment