Advertisements

Wednesday, July 29, 2015

NAIBU SPIKA JOB NDUGAI AMPIGA MGOMBEA MWENZIE

Mbunge wa Kongwa aliyemaliza muda wake ambaye pia ni naibu spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amempiga mgombea mwenzie kwa nafasi ya ubunge, Dk. Joseph Chilongani kwa madai ya kumpiga picha wakati anafanya fujo
Tukio hilo limetokea jana jioni wakati wagombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM wakiwa kwenye mkutano na wanachama wa CCM kwa ajili ya kujinadi kwenye kata ya Ugogoni iliyopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni mdogo wa Dk. Chilongani, Michael Chilongani, Ndugai alichukua uamuzi huo baada ya mmoja wa wagombea anayeitwa Simon Ngatunga kusema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma na kuahidi kuwa kama atakuwa mbunge atahakikisha kuwa anaziba mianya yote ya ubadhirifu kauli iliyomkera Job Ndugai.
Ilipofika zamu ya Ndugai kujinadi kwa wanachama wa CCM alimtuhumu Ngatunga kwa kusema uongo na kwamba hakuna ubadhirifu wa aina yoyote ndani ya Halmashauri hiyo.

Amesema Ndugai aliposhuka jukwaani alianza kumtafuta Ngatunga ili ampige kwa fimbo ambayo huwa anatembea nayo kwenye kampeni hizo.
Wakati akifanya fujo za kumpiga mgombea huyo, Dk. Chilongani alikuwa anampiga picha kwa kutumia simu yake ya mkononi ambapo Ndugai alipomwona alianza kumshambulia kwa fimbo katika maeneo ya tumboni na kichwani hali iliyomfanya mgombea huyo kupoteza fahamu papo hapo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, David Misime alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema kuwa hana taarifa kuhusiana na tukio hilo ambapo Job Ndugai simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani.

3 comments:

Anonymous said...

HIYO NDIYO CCM NA SERIKALI YAKE, SIKUZOTE WANAJIONA WAPO JUU YA SHERIA, WOTE WALIOBAKIA CCM WANA MATATIZO KINA KIKWETE, MANGULA, NAPE, KINANA, MALECELA, LUSINDE N.K. HIVI KWELI UNA AKILI TIMAMU KUMPIGA MTU NA FIMBO NA KUMSABABISHIA MAJERAHA NA KUZIMIA HALAFU POLISI WANAULIZWA WANASEMA HAWAJUI KITU??? NINA IMANI POLISI WANAFAHAMU VIZURI SANA HILO TUKIO ILA WANAMLINDA HUYO NAIBU SPIKA....NDIYO TANZANIA ILIVYO, MASKINI HANA HAKI NA WATADANGANYIKA KUIPIGIA CCM TENA KWA KUPEWA KHANGA, KOFIA NA PILAU HALAFU NCHI ITAENDELEA HIVI HIVI KUENDESHWA KIHUNI HUNI . NAMPONGEZA SANA LOWASSA KUONDOKA CCM....CHAMA CHENYE VISASI NA KISICHOWAJALI WATANZANIA.

Unknown said...

Dah

Anonymous said...

Nakubaliana na wewe kwamba tanzania, na hasa ccm, wanajifanya nchi ni ya kwao. Mambo yao ni hivi: utanijua mimi ni nani mbele ya sheria. Arobaini ya ccm imekariboa, tafuteni pilau na nazi