Advertisements

Saturday, August 29, 2015

Lowassa kiboko yao, Jangwani yatapika

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa, Mh Edward Lowassa akiongea na wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani mapema leo.Mh Lowassa amesema kipaumbele chake kimoja wapo ni Elimu huku akisisitiza kuwa kampeni zao zitakuwa ni za busara na hekima bila kutumia matusi.
Mke wa Mgombea Urais kupitia Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Mama Regina Lowassa akitoa salamu kwa wakazi wa Jiji la Dar Waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani leo.
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Duni Haji akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa Kampeni za Ukawa leo katika viwanja vya Jangwani
Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar Waliojitokeza katika uzimduzi wa Kampeni za Ukawa zilizofanyika Jangwani leo.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mh Freeman Mbowe (wa kwanza kulia) akiwa na wagombea urais kwa Upande wa Zanzibar na Upande Wa Bara na mgombea mwenza bara wakionyesha Kitabu chao cha Ilani ya Uchaguzi mwaka 2015 katika uzinduzi wa kampeni za ukawa uliofanyika katika viwanja vya jangwani.
Halima Mdee akihutubia
 
 Wagombea Ubunge katika majimbo ya Dar Es Salaam wakitambulishwa mbele ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa leo zilizofanyika katika Uwanja wa Jangwani.
 Mgombea ubunge wa jimbo la Kisarawe kwa tiketi ya CUF Kingwendu akisikiliza hotuba ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema chini ya Mwamvuli ya Ukawa
 Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Mh James Mbatia akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar Waliojitokeza leo katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa jangwani jijini Dar
 Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Mh Fredrick Sumaye akihutubia wakazi wa jiji la Dar waliofika katika viwanja vya Jangwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ukawa
 Umati wa watu waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya jangwani leo
 Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema na Mgombea Mwenza wakiwaaga watanzania waliojitokeza katika viwanja vya jangwani katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa
Moja ya kifaa cha Kisasa kabisa aina ya Drone ambacho kilikua kikitumika kupiga picha kutoka anagani ambacho kimekuwa kivutio kikubwa kabisa kwa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam leo katika viwanja vya jangwani .Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

16 comments:

Anonymous said...

Nini sera za Ukawa?

James Bond said...

Nini Sera za CCM ?

Anonymous said...

Wewe inahuhusu nini
Yes in sera za ukawa
Ajira za magufuli kwa waliokosa kura za maoni zo kila kona
Tuwapuuze Kama mzee kipara aliyenyonyoka nywele hadi moyo
Mtu mzima hovyo
Tunamsubirikwa hamu aje mikoani kumpigia debe mwizi mwenzie magufuli atatujuwa sisi kina nani

Anonymous said...

Unauliza majibu kweli bado umelala. Hatutakuamsha hadi ndoto zako za mchana ziyeyuke.!!

Anonymous said...

Jua maana ya UKAWA,wacha uvivu wa Ku goggle neno UKAWA.Ukijua maana yake hutouliza hivyo.
Tupishe huko.

Anonymous said...

Sera zao nzuri sana lowasa atamtoa babu seya na mashehe walio fungwa gerezani!

Anonymous said...

Baada ya uchaguzi tutajua kama kiboko au kibogoyo wao.

Anonymous said...

mbona lowasa anaonekana hana furaha???? halafu hawa ukawa wanataka kumuua mzee wa watu wasingizie serikali ili wapate fursa. hii wamseti mzee wa watu

Unknown said...

nini sera za ccm??? nimezaliwa mpaka nazeeka umeme na maji shida, umasikini kama kawa, mabadiliko kwanza sera baadae, haijalishi tembo umemuuaje ili mradi afe!!

Anonymous said...

@anonymous #1. Acha uvivu wa kufikiri. Nenda mtandaoni utaona sera za ukawa. Watanzania acheni uvivu wa kusoma. Ndio maana mnaishia kuwa maskini wa kutupwa kwa vile hamna utamaduni wa kujifunza au kutafuta habari.

Kalubandika said...

Anonymous August 30, 2015 at 9:18 AM. Usitukane Watanzania. Hujui umuhimu wa mkutano wa hadhara wewe. Kulikuwa na maana gani kukusanya watu ili Lowasa ahutubie? Watanzania wangapi walioko Kijijini kwa baba /babu yako wenye uwezo wa kupata taarifa kwa mtandao? Inaonyesha wazi kuwa UKAWA ni wavivu zaidi kuliko Watanzania. Hamjui kuweka vipaumbele na hamna Mkakati wa kulihudumia Taifa. Ilikuwa ni siku ya EL kueleza at alifanyia nini Taifa. Badala yake ametoa HOMEWORK watu wakajisomee kwenye mitandao. You are doomed!

Anonymous said...

Nyie ndiyo mnatabiri ujinga huu....na ndiyo plan zenu.....nendeni mkaokote mikaa na vibuyu mpeleke kwa mganga wenu .....hamna jipya ...40 yrs nothing concrete zaidi ya ujinga na majungu

Anonymous said...

Good point na ndiyo maana Lowassa kasema elimu, elimu elimu...ujinga nj mwingi sana bongo ...yani ni aibu lowering pass mark iliwatu waonekane wamepass kumbe wamefeli.....where are we heading ...

Anonymous said...

Haya bwana tumezisikia sera za Ukawa ingawa kwa kifupi tu kwani Kiongozi aliongea dakika chache halafu kaishiwa pumzi (at time constraint!!!)na kuomba tunaopenda tuzisome kwenye website ya chama. (However, due to time constraint, Mr Lowassa could not present his speech in totality, but requested those in need of the details to visit Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) website - quoted from Daily News website dated 30/08/2015). Tunashukuru na hii ndio itakuwa changamoto na motisha yetu wavivu wa kusoma na kufikiri kwani tukitaka kujua kwa kinaga ubaga yasemwayo na viongozi ambao hawana muda majukwaani sasa itabidi kuingia kwenye mitandao ingawa sijui wasio na tekinolijia hii watasoma wapi!

Anonymous said...

Wewe unayependa kutumia neno "ujinga" kama huna hoja ya kuandika kaa pembeni wenzako waandike cha maana. Unatuchafulia hii blog kwani iko kwa ajili ya elimu ya Watanzania na wapenda Tanzania kwa ujumla. Matusi hayatusaidii chochote. Kuwa na fikra tofauti katika siasa ni jambo la kawaida na watu hawatukanani kwa ajili wametofautiana kimawazo. Mhusika wa blog hii hebu futa hiyo sentensi hapo juu inayosema "bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku yake" kama unataka lugha ya matusi ieendelee kwenye blog yako.

Unknown said...

Ahsante sana ukawa kwa kumtambulisha Dk slaa hapo jangwani nyie uwongo ndio kazi yenu mlijiapiza kwamba wanawowabeza kwamba dk slaa kaingia mitini kwa kumkimbia fisadi wasubiri kampeni zikianza dk slaa atakavyotema moto na moto wa dk slaa tumeona jangwani poleni sana mnaoendelea kudanganya na hao wababaishaji. Nimeziangalia hizo picha za lowasa kwa kweli anaokana mzaifu wa afya yake . Ule uso wake anaokena kabisa wa kukaribia kulia na atalia sana lol.