Advertisements

Saturday, August 29, 2015

MAGUFULI ATINGA MKOANI NJOMBE LEO

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kampeni kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula akihutubia kwa kumnadi Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli  katika mkutano wa hadhara wa kampeni kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe


 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimtambulisha Naibu Waziri wa Ujenzi, ambaye anagombea ubunge Jimbo la Njombe Kaskazini, Gerson Lwenge katika mkutano wa hadhara wa kampeni wilayani Wanging'ombe, mkoani Njombe
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya  Shilole akitumbuiza leo kwenye mkutano wa kumnadi Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Dk Magufuli akitoa shukrani kwa viongozi wa CCM Mkoa wa Mbeya baada ya kumaliza ziara mkoani humo  na kuanza kampeni katika Mkoa wa Njombe
  Dk.Magufuli akijinadi kwa wananchi na kutoa ahadi  katika nKijiji cha Igoma, Mbeya Vijijini aliposimama kwa muda akielekea Makete mkoani Njombe kuendelea na kampeni.  Akichaguliwa ameahidi kujenga barabara  ya lami ya Njombe hadi Mbeya kuptia Makete na kijijini hapo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wananchi wakishangilia baada ya kuelezwa na Dk Magufuli kuhusu ijenzi wa barabara ya lami itakayopita kijijini hapo
 Wananchi wakimshangilia Dk Magufuli kijijini hapo
 Dk Magufuli akijinadi katika Kijiji cha Ilungu Mbeya Vijijini mpakani na Mkoa wa Njombe
 Wananchi wakishangilia huku wakiwa na vipeperushi vyenye picha za Dk Magufuli
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), ambaye pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Makete,  Binilith Mahenge akimpigia debe Dk Magufuli pamoja na Mgombea ubunge wa Jimbo la Makete, Norman Sigalla.
 Dk. Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano uliofanyika Iwawa wilayani Makete
 Dk Magufuli akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la Makete, Dk Norman Sigalla katika mkutano wa kampeni uliofanyika Iwawa Makete
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu nchini, Amon Mpanju akimpigia debe Dk Magufuli eneo la Iwawa wilayani Makete
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini Dk Magufuli mjini Makete
 Dk Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafuasi wa vyama vya upinzania waliovihama vyama vyao na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika  Iwawa, Makete leo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Mmoja wa wafuasi wa Chadema akiwa amesamama karibu na pikipiki yenye bendera ya chama hicho huku akimsikiliza kwa makini Dk Magufuli akijinadi katika Kijiji cha Kenja, wilayani Makete leo.
 Mfuasi wa Chadema (kulia) akishangilia baada ya kumsikia Dk Magufuli akitangaza kwamba akichaguliwa kuwa urais watoto watakuwa nasoma bure kuanzia darasa  la kwanza hadi kidato cha nne. Kutano huo ulifanyika katika Kijiji cha Kenja wilayani Makete baada ya msafara kuzuiwa wananchi katika eneo hilo wakiwa na hamu ya kusikiliza sera zake.
 Baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Kenja wakimsikiliza Dk Magufuli huku wakiwa na mabango yenye picha za mgombea huyo wa urais wa CCM
 Dk Magufuli akisisitiza jambo katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Kenja wilayani Makete
 Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM,  William Lukuvi akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula katika mkutano wa kampeni wilayani Wangi ng'ombe, Mkoa wa Njombe leo
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana akihutubia katika kutano wa kampeni wa kumnadi Dk Magufuli wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe leo

 Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, Philip Mangula akisalimiana na Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli katika mkutano wa hadhara wa kampeni wilayani Wanging'ombe, mkoani Njombe
 Wananchi wa Kijiji cha Igagala wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali walipokuwa wakimlaki Dk Magufuli, wilayani Wanging'ombe, Njombe
 Dk Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Igagala, wilayani Wanging'ombe
 Wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa CCM mjini Njombe
Msanii Cgegge akitumbuiza katika mkutano wa kampeni za CCM kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe leo

10 comments:

James Bond said...

Huyu Shilole si tumesoma amefungiwa au kwa chama tawala sheria za nchi hazina anafasi?..binafsi sikufurahishwa na kifungo chake ila nahoji utawala wa sheria

Anonymous said...

Mazingaumbwe picha za mwanza Mbeya ndio zinatinga za awali tusidanganyane. Hatukubaliki.. Mkeo Samia yuko wapi mbona huandamani nae??

Anonymous said...

Nonsense! Hakuna atakayekuadhibu kwa kutokuweka andiko kwenye hii blog kama huna cha maana cha kusema. Mpiga kura mwenye akili kama hii hawezi kutuchagulia kiongozi bora bali atatumia haki yake ya kupiga kura kutuchagulia bora kiongozi.

Anonymous said...

Nininkipya zaidi yaani mnatuambia kuwa mtaleta mabadiliko hiyo haipo katika ilani za CCM ila zinabakia kuwa CHukua chako Mapema na ndio kinachoendelela kwa kilamkiongozi anayeingia ukiondoa mwalimu Julous. Nyerere. Hebu tuambizane. Mh. Mkapa kaenda kuhodhi ardhi kule Lushoto kwani kule alikozaliwa hakikuona na kutaka alete maendeleo ya wana Kusini?? Iweje?? Hawapendi alikozaliwa?? Au ni wapumbavu na malofa?? External Dat kajiwekea kijiwe chake anazalisha wakati walioko mtaani kwake wanaumia ile mbaya.!! Tuache kudanganyana na maahadi kibao yasiyotekelezeka. Ukweli unabakia palepale ahadi wanazotoanwagombea wa CCM hazitekelezeki hatabasilimia 40 tuendako sasa hatuna sababu ya kuyaamini hayo. Samia Kaskazini unetembea na ahadi kibao zote ni kitendawili tumekusikiliza sana lakini mhh. Sisi kina mama tunaumia sana umepita na u ii shapata basi utakuja tena baadabya miaka 5. Kwaheri hatuna muda wa kupoteza Mabadiliko. Ndio sasa wewe hutayamudu ndani ya ilani chukua chako.mapema. CCM!!!!???#

Anonymous said...

Ukawa nawapendea hicho tu kwa kashfa Samia kawa mkewe na Halima mdee mke wa mboe, ,,, mwaga sera zenu si msha fungua campen mkajaza nyomi Jagwani mbona hamcoment,,,, ukitukana mwenyewe,,,,,,

Anonymous said...

Siyo Ukawa wala nini....sema ukweli 40 yrs chama tawala kimefanya nini zaidi ya kuangusha wananchi.....magari mengi nchini siyo maendeleo.....Shule nchini ni lower standard na Hospitali jamani ni aibu viwanda tulivyo rithi vyote vimefungwa ...jamani vyakujitegemea vinakufa daily and bado mnaimani things will chamge under the same principles and leadership.
i know watu kibao wanadanganywa .
We need to.change but mnaopenda mambo ya ahadi ...mpigieni kura Pombe na mtajua hali ya Muhimbili baada ya mwezi.

Anonymous said...

Jamani sisi wote ni Watanzania hebu tuandike hoja za maana na tuache matusi. Tujue tu kuwa haya yote tunayoyaandika nia yake ni kuvutia na kushawishi wapiga kura wenzetu kupigia upande mmoja au mwingine tokana na jinsi hoja ya upande gani itakuwa na ushawishi wa busara zaidi. Sasa kama tutaishia kutoa lugha ya matusi hatuwasaidii wenzetu ambao kwa sababu moja au nyingine wanapenda kupata mawaidha yao kutoka kwenye mitandao. Tupende au tusipende kuna kiongozi mmoja wapo kati ya wagombea wote atapewa kura nyingi zaidi na wapiga kura na hivyo kutwaa madaraka ya kuiongoza nchi. Kama leo tutakuwa tunamkashifu kiongozi huyo, akiichukua nchi tutashirikiana naye vipi?

Anonymous said...

Anonymous wa August 30, 2015 at 10:57am u need to wake up!! Nothing will change if the person running for the UKAWA ticket is among those who like u said messed up the country for over 40years...if he really wanted to bring change he should have joined UKAWA long time ago and with a legitimate reason na siyo Eti Miezi michache iliyopita and the reason being he didn't secure CCM nomination....he is still one of them.....wote tunadanganywa siyo CCM peke Yao huyu mtu Ana agenda Yake akiingia Ikulu so do not expect change....WAKE UP PEOPLE !!!!
UKAWA wangemteua one of their pioneers to run and not one of until recently CCM's own....CCM siyo jina CCM ni watu na watu wenyewe ndiyo hao kina Lowassa


Maisha bila unafki hayaendi.


Dr.Slaa:
Lowassa tumemtaja kwny orodha ya watu wanaolitia hasara taifa (List of Shame.)

Mbowe:
Nawashangaa wanaowachoma moto vibaka na kumuacha Lowassa akikamua mitaani.

Mch. Msigwa:
Anayemuunga mkono Lowassa apimwe akili haraka.

Mnyika:
" Nina ushahidi wa kutosha kuhusiana na wizi na ufisadi wa Lowassa na Rostam.

Lissu:
CCM wamempatia Fisadi Lowassa Fomu ya kugombea Urais ni hatari.

Lema:
Ni heshima kwa Mungu kumzomea na kumtukana mtu Fisadi kama Lowasa.

Anonymous said...

Kati ya Magufuli anayehutubia mpaka liamba na yule anayehutubia dakika 10 tu halafu anaishiwa pumzi ni nani atakeyeiona Muhimbili mapema zaidi?

Anonymous said...

Kuna watu respectable wenye CV zao za maana duniani…lakini walivyojihusisha na CCM wamechafua CV zao;
Mfano;
Getruda Mongela mwanamama aiyeongoza mkutano wa Beijing unajua kashfa za rushwa zilizokuja kumkumba
Sospeter Muhongo-A respectable Journalist unajua Amefanya nini kwenye ESCROW
Omar Nundu mtaalamu wa dunia wa usafiri wa anga unajua ni nini kimemtokea
Prof Anna Tibaijuka mama aliyeongoza shirika la Umoja wa mataifa unajua nini kimemtokea
Daudi Balali a respectable IMF and World Bank Economist unajua nini kimemtokea baada ya kujihusisha na CCM.
Ukiachana na hao…Jakaya Kikwete wakati anaingia madarakani alikuwa mtu mchapa kazi…Katika wizara alizopita kabla ya hapo alikuwa mwadilifu na Mchapa kazi…alichaguliwa kwa 80% kumbuka….Nini kimetokea baada ya kuwa Ikulu?
Benjamin Mkapa..Jembe la Nyerere aliingia kama mzee wa kazi ameondoka na kujimilikisha mgodi wa Kiwira.
Magufuli anayegombea urais wa CCM Alishiriki kikamilifu katika kuuza nyumba za serikali….Ameshiriki kuiingiza hasara serikali majuzi kwenye kivuko ca kigamboni shs Bilioni 8…Kivuko hakina muda wa miezi mitano lakini hakifanyi kazi ….ameiingiza hasara serikali kwa maamuzi mabovu mengi aliyofanya.
Ndio maana kwa tunaotazama mambo kwa umbali ni bora CCM ikakaa pembeni tuanze upya (Sio kwamba wapinzani ni wazuri sana)…Kutakuwa na maumivu ya miaka 5 lakini baada ya hapo tuta endelea kama taifa.
Kama taifa inabidi tuweze kufanya maamuzi magumu kwa mustakabali wa vizazi vyetu vijavyo.
Mfano kulikua na haja gani ya kumilikisha kampuni za wazungu gesi yetu kwa miaka 99…tena kwa mikataba ya siri…….
Utakuwa kichaa kudahani magufuli ataipitia hio mikataba na kuifumua…You must be mad
8
5