Advertisements

Sunday, August 2, 2015

STARS UNITED YALAZIMISHWA SARE YA BAO 5-5 NA ALL AFRICAN STARS YA ATALANTA

 All African Stars wakipata picha ya pamoja.                       
Stars United wakipata  picha ya pamoja.


Na Mwandishi wetu Atlanta, GA
Timu Stars United inayoundwa na nyota kutoka majimbo mbalimbali nchini Marekani siku ya Jumamosi Aug 1, 2015 katika kiwanja cha nyasi za bandia cha Hammond Dr kilichopo mji wa Sandy Spring jijini Atlanta jimbo la Georgia, ililazimishwa sare ya bao 5-5 katika mchezo mkali na wa kusisimua  zidi ya timu mchanganyiko iliyoundwa na wachezaji wa mataifa ya Afrika yanayoshiriki mashindando mataifa ya Afrika.Jimbo la Georgia.

Katika mechi hiyo ambayo Stars United ilionyesha kama ingeibuka na ushindi mnono kwa jinsi ya uchezaji wake na kutawala mchezo huo karibu muda wote wa mchezo, tatizo kubwa lililoisumbua Stars United ni kucheza mchezo wa maonesho zaidi badala ya kutafuta ushindi.

Timu ya All African Stars iliyokua imechanganyika wachezaji wazoefu na vijana wanao chipukia ilisimama imara na kujikakamua na kukataa kipigo mbele ya mashabiki wake.


Mpaka mapumziko Stars United walikua wanaongoza kwa bao 2-1 huku ikikosa mabao ya wazi mengi kwa kutokua makini katika umaliziaji huku ikipiga mipira mingi iliyotoka nje au kudakwa na kipa wa All African Stars ambao ndio waliowaalika Stars United kucheza mechi ya kujipima nguvu.

Iliwachukua takribani dakika 20 ya mchezo kwa Stars United kuandika bao la kwanza kupitia mchezaji wake mwenye chenga za maudhi Dennis Geofrey baada ya kuambaa na mpira wingi ya kushoto na kuwapiga chenga mabeki wa All African Stars na kupiga shuti kali la kushutukiza na kumwacha mlinda mlango asijue la kufanya na kuandikia Stars United bao la kuongoza. 

Iliwachukua dakika 10 zingine kwa Stars United kuandika bao la pili kupitia mchezaji wake Eddy ambae jana alikua mwiba kwa mabeki wa All African Stars kwani alikua akabiki kwa kasi na chenga za kushutukiza.

All African Stars baada ya kufungwa goli la pili ilikuja juu na kuanza kuliandama lango la Stars United kama nyuki anayegemwa asali. Ukuta wa Stars United ulioongozawa na mchezaji mzoefu Malik ulikua mgumu kupenyeka muda mwingi wa mchezo kipa wa Stars United alikua likizo.

Kunako dakika ya 42 ya mchezo All African Stars walipata bao lao la kwanza kutokana na mabeki wa Stars United kujichanganya walipomrudishia mpira kipa wao Sean huku mshambuliaji wa All African Stars akiwa nyuma akiifukuzia pasi ile na kuwahi mpira na kuindikia timu yake bao la kwanza.

 Kipindi cha pili kilianza kwa Stars United kujipatia mabao mawili ya haraka haraka kupitia wachezaji wake Eddy na Balotelli aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mechezaji Mo Bilal kutoka New York. 

Stars United iliendelea kukosa nafasi nyingi za wazi huku mshambuliaji wake mwenye njaa na asietoka uwanjani bila kufunga, Dullah Makubeli akiwa anahemewa na mabeki wa All African Stars wakimkaba wawili wawili na kumsababishia kucheza chini ya kiwango na baadae kutoka kutokana na kustua kifundo cha mguu na nafasi yake kuchukuliwa na Hamfrey Owen.

Katika Dakika ya 67 beki ya kati ya Stars United Malik aliyekua kizingiti kwa washambuliaji wa All African Stars aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Dullah Riyami na kuumia kwake kuliwapa All African Stars fursa ya kurudisha mabao yake matatu ndani ya dakika 12 na kujipatia bao la tano kwenye dakika ya 97 ya mchezo na kuwafanya wachezaji wa All African Stars kupaki basi wakitegemea kulinda goli hilo moja walilokua wakiongoza nalo.

Magoli ya haraka haraka waliyofungwa Stars United yalitokana kwa kipa na mabeki kutokua na mawasiliano na timu kufungwa magoli ya kizembe wakati ilikua ikiongoza kwa mabao 4-1.

Baada ya All African Stars ya Atlanta kuwa mbele ya bao 5-4 wachezaji walirudi nyuma kujaribu kulinda goli na kujaribu kuwapa wakati mgumu Stars United isiweze kusawazisha bila kujua hilo liliku kosa na kuwafanya wachezaji wa Stars United kulishambulia goli la All African Stars kama mbogo aliyejeruhiwa anayetafuta kufanya kila awezalo kuokoa maisha yake. Katika dakika ya 90 mchezaji Eddy aliifungia Stars United bao la 5 na kufanya mchezo umalizike kwa timu zote kufungna bao 5-5 huku Stars United ikijilaumu kwa kutokushinda mchezo huo kwani ilikua na kila sababu ya kushinda.

Mchezaji wa zamani wa Ushirika Moshi Michael John ambaye pia ni kocha wa timu ya Watanzania Atlanta, Georgia alikua kivutio kikubwa kwenye mechi hiyo kwa jinsi alivyokua akicheza soka la kuvutia kushinda vijana wadogo.

Kikosi cha Stars United 1. Shabani, 2. Edgar, 3. Liga, 4. Dullah Riyami/ Evans, 5. Malik/ Dullah, 6. Elvis Mnyamuru, 7. Mundo/ Seif, 8. Mo Bilal/ Balotelli, 9. Eddy, 10. Dullah Makubeli/ Hamfrey Owen na 11. Dennis Geofrey/Hadji Helper

Kikosi cha All African Srars 1.Hart 2.Fubu 3.Dk 4.Fred (katakata) 5.Dr.Femi 6.Mike 7.Danis (Attorney) 8.Alhassan (Shaun write Phillips ) 9. Altidore (rashid yekin) 10. Ala (xavi) 11. Honest(muscle men ) reserves. 12.Chigo (Pastor),13. Richard 14.Okocha (mr.no break) 15.Tariq ( Roberto Carlos) 16.Moses (the dribbler) 17. Innocent (caterpillar).

1 comment:

Anonymous said...

Habari imependelea sana upande mmoja.
Hapa ni All African Stars ndio walilazimishwa sare maana Stars United ndio walisawazisha bao la tano Dkk ya 87 ya mchezo kutokana na beki wa All African Stars (Richard) kufanya makosa yaliyopelekea kufungwa kwa Goli hilo.
Mchezo ulibadilika baada ya Mshambuliaji hatari wa All African Stars Moses aka Mo The Dribbler kuingia na kufunga goli la pili baada ya sekunde chache tu za kuingia uwanjani. Goli hilo lilirudisha matumaini ya ushindi kwa All African Stars ambao walicheza mpira kwa kiwango ambacho Stars United waliishia kugombana wenyewe kwa wenyewe, chenga na pasi matata za All African Stars zilizaa magoli matatu ya haraka na kufanya All Afican Stars kuwa mbele kwa goli moja (5-4).