ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 13, 2015

Ukawa waizungumzia afya ya Lowassa


KUFUATIA kuwepo kwa minong’ono juu ya afya ya mgombea urais wa Tanzania kupitia umoja wa vyama unaounda Ukawa, Edward Lowassa, umoja huo umetoa ufafanuzi na kusema kiongozi huyo yupo fiti kiafya.
Jumanne wiki hii baada ya waandishi wa habari kuzuiwa kuingia katika chumba cha kuchukua fomu kwenye Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dar kwa kile ambacho viongozi wa Ukawa walisema ni ukosefu wa hewa kutokana na udogo wa chumba, ilianza minong’ono kuwa afya ya Lowassa labda siyo.

Lakini Ofisa Habari wa Chama cha Wananchi (Cuf), Silas Bwire alipoulizwa juu ya hilo alisema madai hayo ni propaganda za wapinzani wao kisiasa kwani afya ya kiongozi huyo iko vizuri.

“Kwanza watu wanatakiwa wajue afya si mali ya mwanadamu, ni mali ya Mungu, binadamu haupaswi kumhukumu mwenzako kuhusu afya yake, wakati wewe mwenyewe hujajua kitu gani kinatokota tumboni mwako,” alisema Bwire.

Alisema Lowassa ana afya nzuri ndiyo maana anaendelea na mapambano ya kwenda ikulu.
Wakati huohuo, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Salum Mwalimu alisema hali ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe aliyefikishwa hospitali hapo Jumatatu ya wiki hii imeimarika na kwamba tatizo lake lilisababishwa na uchovu tu.
Credit:GPL

5 comments:

Anonymous said...


Daktari wa Lowassa atoe ripoti ya afya yake kwa kutumia vyombo vya habari, na sio riport yake ya afaya itolewe na vijana au wapenzi wake.

Anonymous said...

Kwani Magufuli au jk. Madktari
Wametoa taarifa za afya zao kwa vyombo vya habari

Anonymous said...

Kijamba kazi wa ccm angalia mbele wewe. Huyo swahiba wako wakati anazimia majukwaani mbona mlikuwa mnachekelea wakati sheikh yahaya anamtolea ripoti.

Anonymous said...

HERI YAKE HUYU ANAYESHUTUMIWA KUUMWA KULIKO ALIYEANGUKA JUKWAANI AKIHUTUBIA SIO MARA MOJA BALI MARA MBILI.

Anonymous said...

Hata awe mgonjwa Ikulu ataingia tu!! Hofu imewajaa ccm. Ila mabaya wanayomwombea kamwe hayatampata.