ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 28, 2015

WAKENYA NA MARAFIKI ZAO KUSHEHEREKEA TAMASHA MAALUM LONDON KESHO

Na Freddy Macha
Baada ya mwezi mzima wa kelele, vifijo na chereko- chereko, hatimaye siku mahsusi ya burudani na biashara itawadia kesho Jumamosi 29 Agosti, 2015. Huu ni wakati wanariadha wa Kenya wanaongoza "meza ya medali " mashindano yanayoendelea mjini Beijing, China. Bango la Kenya in the Park- Aug 2015 
Tamasha maalum la “Kenya in the Park” linaloongozwa na kikundi cha ngoma cha Malaika Dance na Taifa Radio FM chini ya msanii na mwanahabari, Lydia Olet, mkazi London, yatafanyika uwanja wa mpira wa Rugby na Soka kitongoji cha West Ham, London ya mashariki. Shughuli hii itakayoanza saa tano asubuhi hadi mbili usiku ni bure na kwa wananchi, wapenzi na marafiki wote wa Kenya. Fahari ya Afrika Mashariki. Habari zaidi pitia www.kenyainthepark.com

No comments: