Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Gymkhana mjini Bukoba tayari kuhutubia wakazi wa Manispaa ya Bukoba.
Umati wa wakazi wa manispaa ya Bukoba wakiwa wamefurika katika viwanja vya Gymkhana kumsikiliza mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli .
Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa manispaa ya mji wa Bukoba ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania atahakikisha bei ya Kahawa inapanda, ujenzi wa viwanda mbali mbali katika kukuza uchumi na ajira.
Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia wakazi wa Bukoba mjini.
Wakazi wa Bukoba mjini wakimsikiliza Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Huo ndio umati ukimsikiliza Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukoba mjini Ndugu Hamis Kagasheki akihutubia kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambazo mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alihutubia.
Msanii Bushoke akitumbuiza wakazi wa manispaa ya Bukoba kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambao mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alihutubia.
Yamoto Band wakishambulia Jukwaa kwenye mkutano wa kampeni za CCM Bukoba.
Fid Q akishambulia jukwaa na nyimbo za hiphop wakati wa mkutano wa kampeni za CCM Bukoba mjini.
Diomond Platnumz akishambulia jukwaa kwenye kampeni za CCM Bukoba mjini.
Halima Bulembo Mbunge mteule kupitia vijana akihutubia wakazi wa Bukoba kwenye mkutano wa kampeni kulia kwake ni mbunge mteule anayewakilisha wazazi kutoka mkoa wa Bukoba Oliva Semguruka.
Mr.Blue akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM Bukoba.
Wanaume TMK wakishambulia jukwaa kwenye kampeni za CCM Bukoba mjini.
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, akijinadi kwa wananchi kwenye mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Gymkhana mjini Bukoba/Dk Magufuli amesema kuwa yeye alipoamua kugombea urais hakufuata fedha bali kufanya kazi tu.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Wananchi wakishangilia hotuba ya Dk Magufuli mjini Bukoba leo
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli, akiwapungia mikono kuwaaga wananchi baada ya kujinadi katika mkutano wa kampeni katika Jimbo la Muleba Kusini
Dk Magufuli akiwapungia mkono wananchi akiwemo Kamanda wa Poilis wa zamani wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana katika Kijiji cha Buganguzi, Muleba Kusini
Dk Magufuli akiomba kupigiwa kura Muleba Kusini katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu.
Mtoto akipeperusha bendera ya Taifa katika mkutano wa kampeni za DK Magufuli Muleba Kusini
Dk Magufuli akiifariji familia ya aliyekuwa mgombea udiwani Kata ya Muleba, Oswald ambaye aloifariki dunia katika ajali ya pikipiki
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimfariji mjane wa aliyekuwa mgombea udiwani Kata ya Muleba, Oswaid Rwakabwa, Georgia alifariki dunia kwa ajali ya pikipiki mjini Muleba, Mkoa wa Kagera. Dk Magufuli aliifariji familia hiyo kabla ya kwenda kwenye kampeni katika Jimbo la Muleba Kusini
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimfariji mjane wa aliyekuwa mgombea udiwani Kata ya Muleba, Oswaid Rwakabwa, Georgia alifariki dunia kwa ajali ya pikipiki mjini Muleba, Mkoa wa Kagera. Dk Magufuli aliifariji familia hiyo kabla ya kwenda kwenye kampeni katika Jimbo la Muleba Kusini
Wananchi wakishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli akiwasili katika mji wa Kamachumu Muleba Kaskazini kuendelea na kampeni
Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Mji wa Kamachumu Muleba Kaskazini
Mmoja wa wanachama wa upinzania akijitangaza kujiunga na CCM KATIKA MKUTANO WA KAMPENI ZA ccm
Dk Magufuli akiomba kura kwa wananchi katika Kata ya Nshamba Muleba Kusini
Wananchi wakifurahishwa na ujio wa Dk Magufuli katika Kata ya Kamachumu, Muleba Kaskazini
Mgombea ubunge Jimbo la Muleba Kaskazini kijinadi kwa wananchi
Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi Muleba Kaskazini
Mmoja wa wakazi wa Kamachumu akisikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli akihutubia na kujinadi kuomba kura kwa wananchi
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi eneo la Kemondo
Ni furaha iliyoje kwa wananchi hawa baada ya kumuona Dk Magufuli alipowasili katika mkutano wa kampeni katika Kata ya Marukucha MaBukoba Vijijini
Mwakilishi wa watu wenye ulemavu kwenye kampeni za CCM, Amon Mpanju akielezea wasifu wa Dk Magufuli
Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Kata ya Maruku, Bukoba Vijijini
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli akielezea sera za CCM
Wananchi wakishangilia hotuba ya Dk Magufuli
Dk.Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza wakati wa mkutano wa kampeni katika Jimbo hilo
Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akiingia kwenye Uwanja wa Gymkhana mjini
Chege na Temba wakitumbuiza katika mkutano huo
Yamoto Bandi ikitumbuiza
FD Q akitumbuiza
Mgombea ubunge jimbo la Muleba Kaskazini, Charles Mwijage akielezea umuhimu wa wananchi kumpigia kuraDk Magufuli. Wengine ni wagombea ubunge viti maalumu kupitia Mkoa wa Kagera. Kulia ni Halima Bulembo
Kundi la Diamond likitumbuiza wakati wa mkutano huo
Dk Magufuli akisalimiana na msanii wa muziki wa kizazi kipya Abdul Naseeb Diamond Platnumz
Mgombea ubunge Jimbo la Bukoba Mjini, Khamis Kagasheki akijinadi kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni mjini Bukoba
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM akijinadi kwa wananchi, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Gymkhana mjini Bukoba
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI














9 comments:
Kwani nani anayeomba urais kwa kutafuta pesa?? Labda Kikwete, Mkapa na Mwinyi.....Wengine wanatafuta titles na wana visababu vingine. Unataka kuwasaidia watanzania wakati uliuza nyumba za umma kwa bei ya kutupa, ukawagawia nyumba nyingine marafiki zako? Umebebwa na Kikwete kama msindikizaji wa Membe bahati mbaya au nzuri kwako walivyomuondoa Lowassa kwa hofu ya kumshinda Membe ndiyo waliopanga kumpigia Lowassa wakakupigia wewe. Inabidi umshukuru Lowassa kwa kukufanya angalau ujulikane na watanzania(Ingawa najua huwezi kushinda kama uchaguzi utakuwa huru na wa haki)Kuna mambo mengi umechemsha Bw. Magufuli.
it seems there is nothing to do in Bongo, I can't believe people would go and listen to any crap from these politicians. God bless them. I sincerely wouldn't handle it even for one second
Yaani watu wanavyomkubali huyu magufuli hadi aibu. Na cha kushangaza zaidi ni uwezo wake wa kupiga kampeni kijiji kwa kijiji bila kuchoka huyu jamaa jembe hasa si mchezo. Ule ushabiki wa kipuuzi tuache kiukweli huyu jamaa kazi, kazi kweli. Alafu mgombea anakwenda na helikopta anatua mjini watu wanamiminika kuja kumshangaa mtu alikuwemo ndani ya helikopta iliokuwa ikizurura angani muda si mchache uliopita picha zinapigwa za mkutano tena za kweli na za kutengeneza kuwaaminisha watu kuwa huyu mgombea anakubalika lakini jitahada anazozifanya magufuli za kukanyaga kila tarafa, kata na vijiji ni maandalizi tosha yatakayo mrahasishia ushindi wa kishindo. Unaona kabisa huyu jamaa hana kabisa mpango wa goli la mkono. Tulikuwa tunawaona simba walivyokuwa wanahangaika na usaili na kambi zao zisokwisha hadi watu wanawacheka. Mara lushoto, mara Zanzibar kwenda rudi. Mara Dar. sasa leo wanaowashangaa simba kushinda gemu zao tena kwa kujiamini basi watakuwa hawana tofauti na watakaokuja kumshangalia magufuli na ushindi wake wa kishindo katika uchaguzi mkuu hili halihitaji hata kumaliza shule ya msingi kuona kitakachotokea .Nanakuhakikishia mnyama atammeza yanga jumamosi na ngoma yao hadi aibu :)
Yaani naifananisha stamina na pumzi ya yanga mbele ya simba sawa na mzee lowasa kwa magufuli kwakwakwa lol.
TUNAMUULIZA SWALI MGOMBEA KWANI MTAGULIZI WAKE ANAYEMALIZA MUDA WA UONGOZI HAKULIONA HILI YAANI JEE NI JIPYA KWA CCM?
Huyu ni J P Magufuli na yule ni J Kikwete. Uadilifu, uwezo wao ni tofauti.Kikwete alichaguliwa kwakua ni handsome, lakini ttuampa nchi Magufuli on 25/10/2015 kwakuwa ni mwadilifu na mchapakazi.
Punguzo munkari na chuki binafsi.Ukitaka jibu la uuzaji nyumba za serikali muulize msemaji wenu mkuu Sumaye na infact alikwisha litolea maeelezo.
Dalili za mvua ni mawingu na hii ni dalili moja wapo kuwa neema ya Mwenyezi Mungu iko njiani inakuja. Wasio amini tafuteni mianvuli na sehemu ya kujibanza kwani bado siku 32 tu mvua ya masika itaunguruma.
Kuhusu magufuli kuuza nyumba za serikali naona mshauri mkuu wa kampeni wa lowasa ndugu Fredrik Sumaye ameshalijibu na kulitolea jambo hilo ufafanuzi wa kutosha ningeomuomba Dj Luke atuwekee tena ile clip ya mzee sumaye wakati akilitolea ufafanuzi hilo jambo kwa kweli utakuwa umesaidia kuelimisha wengi katika upotoshaji wa hilo jambo.
You, September 21, 2015 at 11:48 PM, by contributing here, you have spent more than a second!
Post a Comment