ILANI YA CHADEMA / UKAWA
Kuhusu katiba mpya kuna nukuu kadhaa kutoka kwenye Ilani ya uchaguzi
ya Chadema/UKAWA
Mosi, maelezo ya Mkt wa CHADEMA yanasema kuwa..."UKAWA inajengwa katika msingi mkuu wa kubadilisha katiba iliyopo ili kuweka katiba ya wananchi kwa ajili ya maendeleo yao. Katika kipindi hiki ambacho hali ya maisha ya Watanzania imeendelea kuwa duni, uchumi wa nchi yetu umeyumba, ubora wa elimu ni wa mashaka, ajira kwa vijana ni za kubahatisha na ukiukwaji na uvunjifu wa haki za binadamu umekithiri; uongozi thabiti wenye uadilifu na uzalendo unahitajika kuivusha nchi yetu ili tufike salama”.
Pili, ...... “CHADEMA na UKAWA tunatambua sababu kuu nne zilizosabisha nchi yetu ifike katika umaskini uliokithiri wakati inazo rasilimali za kutosha. Sababu kubwa ni: 1. Ukosefu wa katiba ya wananchi ambayo ingewapa mamlaka ya kuwadhibiti watawala”.

Tatu, wanasema.....”Lengo kuu kwa ujumla katika ilani hii, ni kuhuisha uzalendo, uadilifu na uwajibikaji katika uongozi wa nchi ambao ndio msingi mama wa kuleta maendeleo ya jamii ya Watanzania. Ili tuweze kutoka hapa tulipo tunahitaji uongozi utakaozingatia.”
Yafuatayo ambayo ndiyo msingi wa ilani hii:
Kuimarisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa Kuleta Katiba ya Wananchi inayosimamia haki na usawa
Pia kuna maelezo mengine yafuatayo kuhusu Katiba.
Katiba ya wananchi
• Kutokuwa na katiba bora kumewanyima Watanzania mamlaka ya kuwajibisha viongozi wao, kukosekana kwa dira, tunu za Taifa, maadili na miiko ya uongozi; na kukosa Muungano ulio imara kimuundo.
• Pia kukosekana kwa katiba ya wananchi kumepelekea mfumo wa serikali kiutendaji kuwa mbovu kwani hakuna vyombo huru kama Taasisi ya kupambana na rushwa, ofisi ya mkaguzi mkuu wa serikali, mahakama na vyombo vya dola.
• Kutokuwepo kwa ugatuzi wa kweli wa mamlaka ya serikali kuu kwenda karibu na wananchi kumepelekea watanzania kutoshiriki katika maamuzi ya vipaumbele vyao na kutoshirikishwa katika kupanga na kuisimamia bajeti za maendeleo yao kikamifu na hivyo kuzorotesha maendeleo.
Fursa iliyopo
• UKAWA iliyoanzishwa kutetea katiba ya wananchi ilisusia Bunge la Katiba lililokuwa chini ya wingi wa CCM ambalo lilitupa maoni ya wananchi. Sasa umoja huu umeimarika na sasa unaingia katika uchaguzi ukiwa kitu kimoja na lengo kuu likiwa ni kushinda uchaguzi
ili kuwaletea Watanzania katiba bora. Upinzani unaunganishwa na kutaka kupitishwa katiba mpya ya mabadiliko ya jinsi tunavyoongozana kama vile kuwa na muundo wa serikali tatu yaani serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanganyika na Serikali ya Muungano yenye usawa ambayo itaimarisha muungano, bunge na baraza dogo la mawaziri la serikali ya Muungano.
Nini kitafanywa na CHADEMA/UKAWA

• Katiba ya wananchi ni kipaumbele namba moja, hivyo serikali ya CHADEMA/UKAWA tutaanzisha tena mchakato wa katiba uliozingatia maoni ya wananchi.
Lengo ni kuhakikisha kwamba vifungu vinavyohusu tunu, maadili na miiko ya uongozi vinakuwa kwenye katiba mpya ili sheria na kanuni mpya ziweze kutungwa na kudhibitiwa
• Swala la maadili ya viongozi na watendaji wa Umma litawekwa kwenye katiba na kuanzisha chombo huru na imara cha kusimamia maadili ya viongozi na watendaji serikalini.
Matokeo tarajiwa
• Nchi kupata katiba ya wananchi itakayoharakisha maendeleo yao na kuwa na Muundo wa Muungano unaozingatia haki kwa Tanganyika na Zanzibar
Fursa
Mabadiliko ya Katiba kuelekea katika uundwaji wa katiba ya wananchi, yatahakikisha haki na utu wa binadamu unalindwa.
ILANI YA CCM
Kwa upande wa Ilani ya CCM
Kwa upande wa Katiba, Ilani inazungumzia mafanikio yaliyopatikana kwenye utekelezaji shughuli za Serikali kwa kipindi cha 2010-2015

Mafanikio ni pamoja
(e) Mchakato wa kutungwa kwa Katiba mpya umeendeshwa na umefikia hatua ya Katiba Inayopendekezwa iliyopitishwa na Bunge Maalumu la Katiba ambayo itapigiwa Kura ya Maoni na wananchi;
Ibara ya 145. Ili kuendeleza Utawala Bora, Demokrasia na Uwajibikaji, katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM itahakikisha kuwa, Serikali inatekeleza yafuatayo:-
(g) Kukamilisha mchakato wa kutunga Katiba mpya na kuanza kuitekeleza kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba; na
Maazimio ya Mkutano Mkuu wa Nane
Ibara ya 183. Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM wa Taifa uliofanyika mjini Dodoma tarehe 11-13 Novemba, mwaka 2012 ulipitisha maazimio mengi yenye umuhimu mkubwa katika kudumisha uhai wa Chama chetu ili kiendelee kuwa na nguvu, uhai na uhalali wa kushika dola. Baadhi ya maazimio hayo ni kama ifuatavyo:-
(a) Kudumisha Muungano Mkutano Mkuu wa Taifa ulielekeza kuwa hatua ziendelee kuchukuliwa za kuuenzi na kuuimarisha Muungano wetu wa kihisitoria wa Tanganyika na Zanzibar, wenye muundo wa Serikali mbili. Aidha, changamoto za Muungano huu zitafutiwe majawabu kila zinapojitokeza ili kuimarisha, kudumisha na kuendeleza udugu, umoja na mshikamano uliopo baina ya pande mbili za Muungano.
Katika kutelekeza azimio hili, CCM imeridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali zote mbili katika kusimamia mchakato wa kupata Katiba Inayopendekezwa na ambayo hatimaye itazaa Katiba mpya ya nchi yetu.
Aidha, Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba ndani ya Katiba Inayopendekezwa, kero nyingi za Muungano zimepatiwa majawabu ya kuridhisha. Hivyo, iwapo Katiba Inayopendekezwa itapitishwa hapana shaka itaimarisha Muungano wetu.

6 comments:
nina imani waTANZANIA na wapenda amani na maendeleo watakubaliana kwamba hapa kuna tofauti kubwa sana za HIZI ILANI!! Nasema hivyo kwa sababu gani, ukisoma au ukitafakari sana hapa chama tawala CCM wao wanalenga zaidi chama kuendelea kuimarika, kuendelea kutawala na sio kuleta maendeleo au manufaa kwa wananchi walio wengi, wametizama zaidi upande wao na kunufaika wao, Swala la muungano lisiwe zaidi kisingizio, Zanzibar ina Rais wake, ina maamuzi yake umoja uwepo ndilo muhimu. Katiba ilipokelewa vizuri kabisa lakini ikachakachuliwa vibaya mno kiasi kwamba haikuweza kupitishwa na ndiyo iliyozaa UKAWA unaowasumbua sasa hivi!!
Upande mwingine wa sarafu unalenga kuleta maendeleo na kuwa na katiba iliyopendekezwa na wananchi chini ya mkurugenzi Warioba! kuwawezesha wananchi wanufaike na uchumi, Elimu, Biashara, maendeleo kwa jamii, uongozi unaowajibika na kuondoa tatizo la rushwa lililoota mizizi ndani ya CCM, na hatimaye kurejesha uchumi wa nchi ulioyumba!
Hapa kuna tatizo moja linaloonekana kwamba kwa kuwa lengo la upande mmoja ni kujinufaisha wao tuu, kwenye kampeni kumeonekana kuwa na hasira na chuki za kutoa lawama na kuchochea ubaya kwa upande usiopenda kushindwa (unajulikana)
!! vyama viko vingi vinavyoingia kwenye uchaguzi lakini hapa tumewekewa ilani za vyama viwili, Laengo kubw ahapa ni kupambanisha wawili hawa ambao mmoja anaonekana kuwa ni bora na hviyo kwamba anayetaka kuhodhi madaraka analeta kila mbinu na kutumia fedha kwa kiwango chochote kile ili mradi uongo uendelee kuwekwa ukweli mbele ya macho ya walio wengi wanaoona bila hata ya kuongozwa!! Hapa ni wazi kuna siasa za kutafutana ubaya badala ya kutizama WATANZANIA (TAIFA) kwanza kabla yakushambuliana. Mara tunasoma habari za kashfa sasa hizo kashfsa zimeanza leo!! tukiweka wazi kashfa kweli serikali na viongozi wengi walioko madarakani kitaeleweka hapa si itakuw hadhithi. kwa amani iliyopo Tanzania bazi tunawaombeni wana Kampeni, vyma, tume ya uchaguzi NEC na wapiga kura kwa ujumla bila kusahau jeshi letu la ulinzi litakalokuwepo na walinzi kila kona ya Tanzania. Hebu tuweni na uono wa kile tunachokiita amani kwanza na haki itendeke pale palipo na haki bila kupendelea chama wala upande wowote, tusianzishe vurugu kwa jambo dogo kulinda upande mmoja!! Amani,.. Amani ... Amani.. Mungu ibariki Tanzania na watu wake watulivu..
Mbona mwandishi kaandika mengi upande mmoja tu! Ninavyofahamu hata ilani ya CCM inazungumzia mambo mengi na siyo swala la muungano peke yake. Kama mwandishi hataki tuelewe kuwa anapendelea upande mmoja basi aandike pia zaidi ya maswala ya muungano yalioyoko kwenye ilani ya CCM.
Sasa hao ukawa wanasema wao wataleta serikali yenye kusimamia utawala bora wakati mgombea wao ni kigogo wa mafisadi hii imekuwaje?
Na suala la serikali tatu za muunganoTanzania ni kusema kila mtu achukuwe chake kwa maana halisi ni kuvunja muungano kwa nini tu wasiseme kuwa ilani ya ukawa ni kuvunja muungano? Lowasa na serikali ya uadilifu sawa sawa na kumkabidhi gari mlevi alipitishe mlima wa kitonga . Na hii imekuwaje jamani tutafika kweli?
Hii taarifa ya ilani ya uchaguzi kati ya CCM na ukawa imeletwa kwenu na idara ya uenezi ya siasa kampeni na propaganda ya ukawa ili kupotosha umma kwa ajili ya kulega uchaguzi zaidi kuliko ukweli halisi wa ilani zilizomo ndani ya vyama hivyo hasa CCM. Makala hii imeandaliwa kwa ajili ya kuipamba ilani ya ukawa kikampeni na sio kiuhalisia wa ilani hizo. Na ndio maana haraka haraka mtoaji maoni wa kwanza kaja na maoni ya kuisapoti hii makala na hiyo yote ni mipango ya ukawa na chadema kuupotosha umma.
Inatakiwa tuone mbali zaidi ya maandishi haya yanayoweza kupotosha. Watanzania tunajua kusema na kuandika sana lakini utekelezaji ndio unatakiwa. Tuangalie historia nzima ya miaka 50 tunakwenda mbele au nyuma, kasi ikoje ya huko tunakoelekea? Chama tawala kimejisahau sana na kufikia mahali hawasikilizi wananchi waliowaweka madarakani. Wote tunaowaona tumechoka na ahadi tu, wanaonufaika ni wachache na wamejihalalishia maisha hayo. Tunaposema Lowassa ni fisadi tuangalie baada ya yeye kutoka mangapi ya ufisadi yametendeka? Ukweli ni mengi mno na pengine ya kuzidi, hao wako wapi? Wengi ni viongozi mpaka sasa. Ukweli ni kuwa viongozi wetu ni wachache sana ambao hawana damu ya ufisadi mikononi mwao. Kwa hiyo hii kudai mmoja ndio fisadi sio haki, chama tawala kinao wengi, na hawakufanywa chochote angalau Lowassa aliwajibika. Tunachotaka ni mabadiliko na hayataletwa na wale waliokuwepo miaka 50 wakashindwa kuyaleta inabaki ahadi tu. Timu nyingine Inatakiwa itakayowasikiliza wananchi .
Ananymous wa September 22, 2015 at 8:27 PM
Siyo kweli ilani ya CCM na chama tawala kwa ujumla inalenga kutawala tu bila kutaka kuleta maendeleo au manufaa kwa wananchi wengi. Hizi zote ni fikra duni ambazo Ukawa wamekuwa wakizitoa kuwakejeli wananchi na hivyo kuwafanya wakichukie chama hiki. Katika kufanya hivyo Ukawa wamefumbia macho na kuamua kwa makusudi kutowaelezea wananchi programu ambazo CCM imezifanya na maendeleo ambayo nchi na wananchi wengi kwa ujumla wamenufaika kutokana na programu hizi. Angalia barabara mpya zilizojengwa na za zamani kukarabatiwa. Angalia shughuli za viwanda, madini, gasi, mafuta zilivyoanzishwa, wawekezaji vitega uchumi wa ndani na nje ya nchi kuongezeka, uchumi wa nchi ukiendelea kukua kwa asilia 7 kwa mwaka ni baadhi tu ya maendeleo ya nchi yanayotokana na uendeshaji na usimamizi madhubuti wa CCM. Hivi wewe kama Mtanzania msema ukweli utakanusha kuwa haya yote sio maendeleo na kwamba CCM haipendi kuleta maendeleo nchini na kwa Watanzania wengi?
Najua kila mmoja anataka maendeleo zaidi ya hapa lakini lazima tukubali pia kuwa maendeleo hayapatikani kwa kipindi kifupi wala masaa 48 kama viongozi wenu wanavyowadanganya wananchi. Maendeleo ya nchi ni swala la muda mrefu ndio maana hata nchi zilizoendelea imewachukua muda mrefu sana kupata hayo maendeleo waliyo nayo. Marekani wana miaka zaidi ya 200 ya uhuru lakini pamoja na maendeleo waliyoyapata kuna wananchi wao wengi tu ambao wanataka maendeleo zaidi. Hivyo ni vizuri kutambua hata yale maendeleo kidogo ambayo nchi na CCM kwa ujumla imeweza kutupatia badala ya kukaa tunalalamika na kulaumu vyama na viongozi wetu tu kila wakati.
Post a Comment