Advertisements

Sunday, September 20, 2015

KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA CHATOA MAFUNZO YA HAKI ZA BINAADAMU KWA VIKOSI VYA SMZ

Kamanda wa Polisi mkoa wa kusini Pemba ‘RPC’ Juma Yussuf Ali, akifungua mafunzo ya siku mbili yaliowahusisha Polisi jamii na Vikosi na Idara maalumu ya ‘SMZ’ Pemba, juu ya haki za binadamu, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba, kulia ni Mratibu wa mfaunzo hayo, Khalfan Amour Mohamed, na kushoto ni mtoa mada kutoka afisi ya ‘DPP ‘Pemba Mohamed Ali Juma
Mratibu wa mafunzo ya haki za binadamu kwa Vikosi na Idara maalumu za SMZ, Khalfan Amour Mohamed akielezea namna Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba, kinavyofanya kazi na makundi mbali mbali, kwenye mafunzo hayo yaliofanyika afisini kwao Chake chake Pemba, kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa kusini Pemba RPC, Juma Yussf Ali.

 Mtoa mada kutoka afisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Pemba Mohamed Ali Juma, akito akwenye mafunzo yalioandaliwa na ‘ZLSC’ kwa ajili ya Polisi jamii na Vikosi na Idara Maalum za ‘SMZ’ yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ na kufanyika afisini kwao Chake chake Pemba,
Askari wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji ‘KZU’ Ndg.Mohamed Fadhil Abass akiuliza suali kwenye mafunzo ya siku mbili juu ya haki za binadamu, yaliowahusisha vikosi hivyo vya SMZ na Polisi jamii wa Mkoa wa kusini Pemba,
Washiriki wa mafunzo ambao ni Vikosi na Idara Maalumu za ‘SMZ’ Pemba pamoja na Pilisi jamii, wakimsikiliza mtoa mada Suleiman Ame, kutoka Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi ‘ZAECA’ hayupo pichani, mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba, na kufanyika afisini kwao Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments: