ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 16, 2015

KUMBUKUMBU

16-09-1964 16-09-1998
KUNDASAI ROBERT TERRY

Mume wangu mpendwa,leo umetimiza miaka 17 tangu ulipoitwa mbinguni kwa baba.
Hatuna cha kusema,tumebaki kushukuru tu maana imeandikwa,tushukuru kwa kila jambo.
Kweli ua zuri limerudi kwenye bustani ya Eden.
Tunakumbuka sana upendo wako na utanashati uliokuwa nao.
Kundasai,tupo kama ulivyotuacha kama familia,ni imani yetu kuwa ipo siku tutakutana Paradiso.
Unakumbukwa sana na mimi mkeo Elizabeth Terry,wanao Harrison na Diana Terry, familia nzima ya kwa Terry ya Arusha na Mamba Kiria,mashemeji zako wa ukoo wa Kweka,ndugu,jamaa na marafiki.

"Raha ya milele umpe ee bwana"

No comments: