ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 14, 2015

SUMAYE-SIRUDI NYUMA MPAKA NIHAKIKISHE CCM IMENG'OKA!


Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amesema pamoja na vitisho ambavyo amevipata kutoka kwa mahasimu wake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hatarudi nyuma mpaka atakapohakikisha chama hicho kimeng’oka madarakani.
Kadhalika, amesema mwisho wa CCM kukaa madarakani ni mwaka huu kwa kuwa wananchi wameamua kufanya mabadiliko wenyewe. 
Aliyasema hayo jana wakati akizindua kampeni za ubunge Jimbo la Ubungo za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Alisema ukiwa ndani ya CCM, ni vigumu kufanya mabadiliko kutokana na mfumo uliopo, lakini hata mtu akiamua kwenda chama kingine kutokana na ukiritimba wa CCM, anakuchukiwa.
Alisema kwa ambavyo ametembea katika mikoa mbalimbali kwa kampeni za kitaifa za mgombea urais waChama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayeungwa mkono vyama shirika vya Ukawa, Edward Lowassa, CCM mwaka huu ni lazima iondoke madarakani.
Alitaja mambo manne ambayo yatachangia CCM kuondoka madarakani kuwa ni pamoja na ukosefu wa Katiba ya Wananchi ya kudhibiti utawala mbovu ambayo alisema Ukawa wakichukua dola, litakuwa jambo la kwanza kuanza nalo na itawapa wananchi mamlaka ya kuwa watawala wa viongozi. 
Nyingine ambayo alisema imewafikisha Watanzania katika hali hiyo ya umaskini kuwa ni kukosekana kwa umoja, uzalendo, uadilifu wa utawala ambao umesababisha kutowajibika kwa viongozi na hata kuacha mianya ya rushwa. 
Sumaye alisema yeye hajaenda upinzani kwa ajili ya uroho wa madaraka kama wengine wanavyodai, kwa kuwa hagombei nafasi yoyote.
Kwa upande wake, mgombea wa ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Ukawa, Saed Kubenea, alisema endapo wananchi wa Ubungo watamchagua, hawatajuta kamwe kwa kuwa amejipanga vya kutosha kuwasaidia.
Kubenea alisema akiingia madarakani, atashughulikia tatizo la usafiri katika jimbo hilo, tatizo la maji, afya na matatizo mengine.

7 comments:

Anonymous said...

Hana effect yoyote.Kwa miaka 10 CCM haikukuitaji kwa namna yoyote, sio ubunge, wenyekiti wa kamati,hata kwa ushauri! Don't you get it!

Anonymous said...

Kama kuna ushahidi wa vitisho kwa nini asiripoti kwenye vyombo vya usalama na NEC ili wahusika washughulikiwe? Uongo kuwa ndani ya CCM mtu hawezi kuleta mabadiliko tumeusikia sana, tatizo ni kuwa Sumaye na wenzake wa aina yake hawakuwa na mawazo yoyote ya kupendekeza na hivyo kutaka kukibadilisha chama hicho zaidi ya kuwa bendera tu zinazofuata upepo. Ni sababu kama hii ya kuwa "ndiyo bwana" wakati wote hata huko kwenye upinzani wameshindwa kuvisaidia vyama vyao vipya ili viweze kujenga sera na hoja za maana badala yake wamebaki kulalamika tu. CCM haing'oki badala yake tutaona mwisho wa Ukawa baada ya waroho kama Sumaye na mwenzake Lowassa kwenda kuvuruga vyama hivi vya upinzani. Ni majonzi na masikitiko makubwa kwani Tanzania tulianza kujivunia kuwa upinzani umeanza kushamili nchini na hivyo kuleta msisimko mkubwa katika duru la siasa!

Anonymous said...

Mimi ni mtanzania tena mtanzania kama leo ikitokea taifa lolote lijitoe fahamu liseme linakwenda kuivamia Tanzania kwa msingi ya dhuluma ya aina yeyote basi maisha yangu kwa asilimia 100% nipo tayari yaishie hapo kwa kulipigania taifa. Hapa sizungumzii ukawa, chadema au CCM nazungumzia utaifa kwa roho safi. Kwa upande wa vyama vya siasa na mabadiliko ya siasa nchini basi CCM licha ya udhaifu wake na to be honest CCM sio dhaifu ni udhaifu wa baadhi ya watumishi wake sio CCM. Watu kama kina mzee msumaye anachokifanya sasa hivi ni kuwadanganya watanzania kuwa chama cha mapinduzi ni kichafu sio yeye wakati yeye ndie aliekuwa mtendaji mkuu wa serikali ya CCM sasa kiufasaha kabisa uchafu uliokuwanao CCM basi mzee sumaye na ndugu yake lowasa ni miongoni mwa watumishi wa CCM waliowasababishia watanzania adha kubwa katika maisha yao na la kushangaza ati leo wanazunguka Tanzania zima kuwadanganya watanzania kuwa CCM haifai wao ndio wanafaa. Hivyo mtu akipewa zamana ya duka likiwa na kila Kitu ndani lakini mara baada ya mpewa zamana huyo wa duka kuondoka au kuachiswa akiliacha duka likiwa na hali mbaya anatoa shutuma kuwa duka lilikuwa baya na sio yeye kwa hivyo anaomba zamana ya kupewa duka jengine atafanya vizuri ?Sasa jamani kama huo si utapeli ni kitu gani? Na kama kweli watanzania wanawaamini hawa wazee wanayoyasema kuhusu CCM basi mimi si mtanzania tena nipo serious sio kama naipenda CCM hapana nimeshaitembea dunia vya kutisha na nimekutana na wadanyifu wengi kiasi kwamba kwangu inakuwa rahisi kuwapambanua na sina shaka kabisa kuwa lowasa na sumaye ni miongoni mwa hao wadanganyifu . Vilevile CCM inamising imara ya muundo wake, katika CCM hakuna dhambi ya ukanda au ukoo au ukabila tujitahidi kuilinda misingi ya aina hii si kwa CCM tu hata kwa vyama vingine vya siasa kwani ni misingi mizuri kwa amani ya nchi na maendeleo ya watu wake kwani umoja ni nguvu. CCM ni ya watanzania wote uwe unatoka kusini au mashariki. Kaskazini au kusini ilimradi imekusanya watanzania wake wote katika nyazifa mbalimbali ya chama hicho kwa kweli inavutia sana. Hata leo tumejionea magufuli alipotokea hajulikani sasa anakaribia kuwa kiongozi wa juu kabisa wa CCM . Tumeona jinsi dk slaa alivyo fukuzwa kama paka licha ya jitahada zake zote za kukiimarisha chadema tatizo kile chama sio cha wananchi ni chama cha watu binafsi ndio wanaoamua nani ashike nafasi gani sio wananchi. Kama chadema na ukawa ni taasisi ya wananchi basi dk slaa na lowasa chaguo la wananchi kamwe isingekuwa lowasa hata siku moja.

Anonymous said...

hii ntu wala msiiamini mzinifu mkubwa nakumbuka alipokuwa amekuja kusoma hapa usa alikuwa anazini sana na dada temina jeuri wa pale boston na kuwa karibu sana na feruzi nduguye temina na kumuahidi mengi kumbe kamba tu haya na huyo anaempigia debe bwana lowasa ana kabint kadogo kamezaliwa mwaka 1995 na wakati anazini nae ni miaka mitatu iliyopita kabint kana kaa kinondoni na jina lake linaanzia na H na mshenga mkubwa alikuwa dereva wake na siku ya kwanza kukutana ilikuwa pale muslim na wakampa lifti na ndipo uhusiano wao ulipoanza sasa edo huyu cmjukuu wako halafu alimuomba mpk picha za uchi ushahidi nnao mpk leo kwa ataetaka niweke hadharani na ieleweke kuwa mi cmwana siasa na huyo bint ni ndugu yng na aliniomba ushauri wkt edo anataka picha hizo na nikamfahamisha jinsi gani afanye sasa kweli atatufaa kuwa rais huyu

Anonymous said...

Miaka 50 ya sera za ufisadi na umaskini kazi ni mmoja kuingoa CCM. Tumechoka na umaskini

Anonymous said...

You're one of those who can pause and their brains! There are a bunch of mentally challenged folks out there who, take irreconcilable positions all the time. They would tell you they're sick and tired of corruption but at the same time they're determined to throw their wholesale support to the most corrupt candidate. It's odd!

Anonymous said...

It's odd, indeed.