ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 3, 2015

LOWASSA APATA MAPOKEZI YA KIHISTORIA KISIWANI PEMBA

- Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa akiwapungia mkono wananchi, wakati akiwa njiani kuelekea kwenye Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Tibirinzi, Kisiwani Pemba leo October 3, 2015.
- Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa akiwa ameusimamisha msafara wake kupisha watu wa huduma ya kwanza walikuwa wamembeba mama mmoja (jina lake halikupatikana kwa haraka) aliekuwa amepoteza fahamu kutokana na kukosa hewa katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Tibirinzi, Kisiwani Pemba leo October 3, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa akifurahi jambo na Mgombea Mwenza wake, Mh. Juma Duni Haji pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, walipokutana katika katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Tibirinzi, Kisiwani Pemba leo October 3, 2015.

10 comments:

Anonymous said...

Hivi kuna watu wangapi Pemba yote?
Nataka kujua tu ili nichambue mengine.

Anonymous said...

Unajua Lowasa na Ukawa wanamlipa fedha taslimu yeyote anayetaka kudhuria mikutano yao. Watu wanasafiri maili nyingi ilimradi wanajipatia vijisenti. Hii ni sawa na auditions za movies huku ughaibuni. Kwa wale waliopo Marekani, wanajua huu mchezo kama bwana Trump anavyoucheza. The bad part is that, the masses don't translate to actual votes, and therefore misleading!

Anonymous said...

Muulize Maalimu sefu

Anonymous said...

Zanzibar inaundwa na visiwa viwili na mgawanyo wa idadi wa watu ni kama ifuatvyo: Unguja - 622,459 na Pemba - 362,166.

Jumla ya watu wote Zanzibar kama nchi ni watu 984,625. Ujue pia kuwa Wazanzibari wengi wameweka maskani yao Bara.

Anonymous said...

Pemba kuna watu 330,000 kwa sense ya mwaka 2010, na asilimia 80% ni watoto chini ya miaka 10.

Anonymous said...

Swali la idadi ya watu wa pemba nenda Takwimu utapata jibu halisia. Ila unachotaka kuchambua ni pumba na huna kazi ya kufanya. Unashindwa kupaambanua kiongozi na mpiga dili! na pushh za juu!!

Anonymous said...

Uchambue nn mdau hapo juu, ukiambiwa zaidi ya laki saba hoja yako ndio itakuwa imetimiaa?? Hizo picha ndio halisia ya tukio.

Anonymous said...


Hello Dj. Luke, on several instances you have suppressed opinions submitted by some readers of your blog. P'se, allow their commentaries to be published no matter how unpalatable they sound, because it guarantee their First Amendment Right i.e. Freedom of Speech. Censorship violates Federal law, and of course, nobody is above the law.

Anonymous said...

Idadi ya watu wote Zanzibar mwaka 2012 ilikuwa kama ifuatavyo:
Unguja 896,721
Pemba 406,848
Jumla 1,303,569

Source: Population and Housing Censuses 2002/ 2012: National Bureau of Statistics (Tanzania)

Anonymous said...

Watu Pemba ni wachache mno kiasi kuwa hata wakiamua wote kuwapigia Ukawa hawawezi kuleteleza CCM ikashindwa. Ngome ya CCM iko Unguja ambako idadi ya watu ni kubwa zaidi.