Advertisements

Friday, October 23, 2015

Lowassa: Nikishindwa urais nakwenda kuchunga ng’ombe

Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na
By Julius Mathias, Mwananchi

Dar es Salaam. Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa amesema akishindwa kupata ridhaa ya wananchi kuwa rais wa awamu ya tano ataenda kijijini kwake kuchunga ng’ombe.

Lowassa, kada wa muda mrefu wa chama tawala aliyetimkia upinzani na kufanikiwa kupitishwa kugombea akiviwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ameyasema hayo alipofanya mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili) na kubainisha matokeo ya ushindani wowote lazima yawe na mshindi pamoja na aliyeshindwa.

"Nina ng’ombe wangu kijijini nitakwenda niwachunge na kuendelea na maisha," amesema Lowassa kwa kifupi alipoulizwa nini hatma yake endapo atashindwa kuukwaa urais kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumapili hii na kumpata kiongozi wa awamu ya tano.

Waziri huyo wa zamani, ameitumia nafasi hiyo kufafanua namna atakavyotekeleza sera ya elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu na kubainisha vyanzo vya mapato atakavyovitumia.

Amezitolea mfano nchi za Ulaya ambazo zimefikia hatua hiyo kwa wananchi wake na kulinganisha na rasilimali ambazo Tanzania inazo kwamba zinatosha kufanya kile kinachofanywa na mataifa hayo ya magharibi na kuwapunguzia gharama Watanzania.

"Ulaya hakuna malipo yoyote yanayotozwa kwa wanafunzi. Tunazo rasilimali nyingi zinazotuwezesha kununua magari makubwa kama Range (Rovers) kwanini fedha hizo zisitumike kugharamia elimu? Tunayo hifadhi ya gesi iliyogundulika kusini nayo ni muhimu kwa uchumi. Watanzania wanipe ridhaa waone jinsi nitakavyotekeleza," amesema Lowassa.

Tofauti na chaguzi zilizopita, mwaka huu kumekuwa na mwamko mkubwa miongoni mwa wananchi hasa vijana ambao wamejitokeza na kushiriki kwa hatua zote za maandalizi yake kuanzia uandikishaji mpaka mikutano ya kampeni.

Kwa mujibu wa takwimu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), wapigakura waliojiandikisha na kuthibitishwa ni 22.75 milioni na miongoni mwao, katika kila watu 10 sita ni vijana hivyo kutoa changamoto kwa wagombea na vyama vya siasa kuweka mipango imara ya kulishawishi kundi hilo.

16 comments:

Anonymous said...

SAWA MKUU.UMEWAJIBU VEMA.LAKINI CCM WASINGETHUBUTU KULIJIBU HILO.MIMI NI MFUASI WA MABADIRIKO NA,NINAZO SABABU 75 ZINAZONIONGOZA NIMCHAGUE MHE.EDWARD LOWASSA AWE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. MNIVUMILIE NAZITAJA ZOTE NAZO NI:-1.NI MCHA MUNGU 2.ANAWAPENDA WATANZANIA 3.ANAYE MKE MWAMINIFU 4.ANA UWEZO MKUBWA 5.NI MWADILIFU-KIMATENDO ANAICHUKIA NA KUIKEMEA RUSHWA 6.MTETEZI WA ELIMU BURE 7.NI MKWELI 8.MFALME WA MAAMUZI MAGUMU 9.ANA MVUTO WA KIPEKEE 10.KIPENZI CHA WATANZANIA 11.ANAOGOPWA NA MAHASIDI 12.ANATISHA KWA WAVIVU 13.KIBOKO CHA WATORO 14.KIBOKO CHA WALEGEVU 15.MFALME WA HARAMBEE TANZANIA 16.MPENDA KAZI MKUU 17.HAVUMILII UZEMBE 18.MTU WA MALENGO 19.ANAUCHUKIA UMASKINI 20.ANAWACHUKIA WEZI 21.ANAWACHUKIA VIOGOZI WAONGO 22.NI MTANASHATI WA DARAJA 23.ANAUNGA MKONO SERIKALI TATU 24.ATAIFUMUA BAJETI-KANJANJA 25.BWANA KILIMO 26.MTAALAM BIASHARA-ANAWAPENDA WAFANYA BIASHARA 27.BWANA MIFUGO 28.ANAKUBALIKA KIMATAIFA 29.ANAKUBALIKA MAREKANI 30.ANAKUBALIKA CHINA 31.ANAKUBALIKA ULAYA 32.ANAWAJALI WAFUNGWA 33.ANAJALI MISIBA NA VIFO 34.ANA MPANGO MZIMA KWA WASANII WOTE 35.ANAWAJALI MAMA LISHE 36.ANAWAJALI BABA LISHE 37.RAIS WA BODABODA 38.RAIS WA BAJAJ 39.ANAWAJALI MADEREVA 40.ANAWAJALI ABIRIA 41.ANAKATAZA MANYANYASO 42.ANAWAJALI ALBINO 43.BWANA"FAIDI MAJI YA ZIWA VICTORIA" 44.BWANA MAKAO MAKUU-DODOMA 45.ANAWAJALI WAZANZIBARI 46.ANA UTU NA HESHIMA 47.ANALICHUKIA NENO "HAPA KAZI TUU" 48.ANAWAPENDA MAJIRANI ZETU 49.ANAUPENDA USAWA WA KIBIASHARA 50.ANAWAPENDA WANAMICHEZO 51.ANAPENDA UKOMAVU WA KIUCHUMI 52.MTAALAMU KILIMO CHA UMWAGILIAJI 53.ANAIPENDA DAR-ES-SALAAM 54.ANAIPENDA MBEYA 55.ANAIPENDA MTWARA 56.ANAIPENDA MWANZA 57.ANAIPENDA MIJI YOTE TANZANIA 58.ANAVIPENDA VIJIJI VYOTE TANZANIA 59.ANAPIGANIA KUKUA KWA PATO LA UTALII 60.ANACHUKIA BARABARA FINYU NA MBOVU 61.ANAWACHUKIA MAJANGILI 62.ANALIPENDA SHIRIKA LETU LA NDEGE-AIR TANZANIA 63.ANAPENDA KUANZISHA VIWANDA-MALIGHAFI 64.ANAICHUKIA NJAA 65.HAIPENDI NA ANAILAANI "MV BAGAMOYO" KANJANJA 66.HAPENDI KUPANDISHWA KWA NAULI 67.KATANGAZA VIVUKO VYOTE BURE 68.ANAWAPENDA WAFANYAKAZI 69.RAFIKI MKUU WA MACHINGA 70.ANA TIMU IMARA MNO ILIYOMZUNGUKA 71.ANA USONGO NA MAENDELEO YA HARAKA 72.ANAIJUA TANZANIA 73.ANA WEPESI WA KUELEWA NA KUKUBALI 74.NI MVUMILIVU WA KUPINDUKIA NA,75.NI MWANA SIASA GWIJI,MKOMAVU,MNO. KWA SABABU HIZI 75 LOWASSA ANASTAHILI KUPEWA DHAMANA YA KULIONGOZA TAIFA LA TANZANIA KUPITIA KURA ZETU HAPO KESHOKUTWA JUMAPILI TAREHE 25 OCTOBA 2015.ASALAAM ALEYKHOUM,BWANA YESU APEWE SIFA. JINA LANGU ANGOMWILE MALOFU MWALUBALA

Anonymous said...

You're EITHER a mentally-challenged dude in urgent need of a psychiatrist OR a corrupt person who resembles Lowasa in all material respects!

Anonymous said...

Kwann asikiimarishe Chama ili 2020 alete hayo mabadiliko.

Anonymous said...

asante angomwile sikujui ijui wewe ni profesa wa maprofesa.elimu unayo angomwile.sijawahi kuona upembuzi wa kina na yakinifu amna hii katika historia ya siasa za tanzania.hongera sana.umetufumbua akili za ziada.mimi kwa upannde wangu nimevutika kumchagua mhe.lowassa kupitia vigezo vvya angomwile namba moja hadi kumi tuu[1-10] yaani ucha Mungu,kuwapenda watanzania,mke mwaminifu,uwezo mkubwa,uadilifu-kivitendo,mtetezi wa elimu bure,mkweli,mfalme wa maamuzi magumu,mvuto wa kipekee na kumi kipenzi cha watanzania naongezea walio wengi.hizo sababu 65 zilizobaki nazihifadhi akiba. jumapili tarehe 25 octoba 2015 nitampigia kura mheshimiwa lowassa.

Anonymous said...

Ngojea tarehe 25/10/2015 ukamsaidie kuchunga ng'ombe.

Anonymous said...

mkuu una uhakika na yote hayo uliyoandika au umeshakula cha juu.mmh misifa mingine hata mtu mkewe hawezi kumsifia hivyo. na mimi wala sina chama ila misifa yote hii mtu mmoja hawezi kuwa nayo kwani yeye malaika.
na sina ubaya wowote na lowassa ila nakata sifa zote hana hizi.na wala ccm hayupo mwenye sifa zote hizi.

maendele ya kweli ni wewe na juhudi yako hakuna raisi yeyote atakaye kupa hayo maendeleo.

ushabiki maandazi tuuache.tupige kazi na elimu that is it.

mungu ibariki Tanzania yenu wafanye uchaguzi wa amani mungu wabariki watanzania wote wawe na ummoja na upendo wa kudumu bila kubagua dini wala kabila wala rangi.Amen.

wadau wote mungu akubarikini amen.tuisadiye nchi yetu popote pale tulipo na tuache ushabiki maandazi.tuwe wazalendo wa kweli bila kujali kupokea cha juu ndo tuwe wafuasi wa chama.tuipende kweli kwa dhati nchi yetu na watu wetu amen.

Anonymous said...

Mdau wa 75 REASONS popote ulipo agiza kinywaji na chips kuku nitalipa bill yako.
MAMA MABADILIKO HAPA.
Napatikana 7542078.

Anonymous said...

Anonymous wa saa 9:40am. Umetaja sifa nyingi za lowasa unaempendekeza awe raisi ila hukumtendea haki kwa kutoainisha sifa yake kuu ya ufisadi katika utumishi wake. Katika CV ya Lowasa ukiacha kuiainisha taaluma yake ya ufisadi itakuwa haijakamilika . Lowasa mgonjwa amepoteza hata uwezo wa kumbukumbu tumeshuhudia katika interview aliofanya na shirika la BBC la uengereza huvi karibuni yaani katika interview hiyo hatukumshudia lowasa bali tulishuhudia mtu mfano wa zombie asiekuwa na hata na uwezo wa kupumua. Kila wakati lowasa anapoulizwa suala la ufisadi anonekana kuwa hayupo comfortable kabisa katika kulitolea ufafanuzi wake kwanini ? Tunasema tena Lowasa kutamka wazi yakuwa atakwenda kuchunga ng'ombe wake baada ya kushindwa uchaguzi inaonesha ni jinsi gani lowasa alivyo kuwa hana malengo na chadema kwake yeye anachojali ni kuingia ikulu tu . Ni hasara kubwa na pigo kwa wapinzani kumpoteza mtu kama dk Slaa kwa sababu ya mpita njia mwenye uchu wa kuwa raisi kama lowasa.Chadema na ukawa wataisoma namba baada ya uchaguzi kwa kosa la kumpokea lowasa.

Anonymous said...

KAJIBU NINI SASA HATA SWALI MOJA HAJIBU,,,, USHABIKI WA SIASA KAMA WA TEAM ZA MPIRA,,,, KWELI PEOPLE Z POWER,,, HATAKAMA KUSOMA HUJUI ANGALIA PICHA, ,, LOWASA IKULU ATAISIKIA TU HATAKAMA ANAJAZA MAFURIKO SWALI WATAENDA KUPIGA KURA? HAMKA WII KUSEMA MMEIBIWA KURA.

Anonymous said...

In short, hujielewi..

Anonymous said...

Na wewe ndio walex2 ambao akili zenu mmehifadhiwa na Mbowe mpaka baada ya uchaguzi. .

Anonymous said...

NAITWA ANGOMWILE, NAWASHUKURU SANA VIJIMAMBO UJUMBE WANGU UMEFIKA,TENA KWA KISHINDO.HAKUNA SWALI LOLOTE LA KIPUUZI KUTOKA NYINYI WAFUASI DIE-HARDS WA CCM LILILOKOSA JIBU KATIKA 75 BORA ZA LOWASSA.WEWE FANYA CORRESPONDING ENTRIES KWA SIFA HIZO ZOTE UKIMLINGANISHA MGOMBEA MAGUFULI WA CCM.MFANO SIFA NAMBA MOJA MCHA MUNGU.LOWASSA AMESAIDIA KUPITIA HARAMBEE ZAKE KUKUSANYA MABILLION KUIMARISHA MISIKITI,MAKANISA NA TAASISI ZAKE MBALI MBALI,GEUKIA KWA MAGUFULI KUNA NINI KWAKE?IPO HATA SENTI TANO ALIYOKWISHACHANGIA HADI LEO JUMAMOSI TAREHE 24 OCTOBA 2015?UPUUZI WEKENI KANDO.UJINGA MUUMEZE MIOYONI MWENU.KARAMA YA LOWASSA IPO WAZI.NENDA POINT KWA POINT,PATAKAPOKUKWAZA KWA UFEDHULI WAKO NIULIZE.MAJIBU YOTE NINAYO,NA PIA NINALIHIFADHI KAPO LA MAJIBU YA ZIADA.

Anonymous said...

Suala la Ccm kuiba kura,halizuiliki,narudia halizuiliki.wamejiandaa kweli kweli, KUFA KUPONA.wanawatumia polisi kikamilifu,wanavitumia vyombo vingine vya dola kikamilifu.uliona wapi unaambiwa ukishapiga kura rudi nyumbani [NIKIWA NYUMBANI NIFANYE NINI? NILALE? NIFUMBE MACHO? NICHUNGULIE DIRISHANI? TUONGEE KWA SAUTI NDOGO YA KUNONG'ONA?.hii ni kali,tena ya karne.Ni heri Wangesema ukishapiga kura,endelea na ratiba yako nyingine ya maisha.kuna kwenda kanisani,misikitini,masokoni,hospital,safari,kazini na shughuli nyingi nyingi za kimaisha.lakini Tume,Polisi,na Mahakama wanasema UKISHAPIGA KURA URUDI NYUMBANI.HII NI KARI YA KARNE.MIMI NIKALALE NA WEWE UKAYACHEZEE MASANDUKU YA KURA.MUNGU YUPO,MTAIBA SANA,LAKINI TSUNAMI YA LOWASSA IPO PALE PALE.

Anonymous said...

Malafyale Ango, acha ulimbukeni na makelele yasio na mshiko.

Ukiangalia vizuri mahojiano kati ya Lowassa na Zuhra wa BBC, ni dhahiri kuwa Magufuli ndiye Rais wa awamu ya tano. Wewe na mimi ni wabongo, kwa uelewa wangu mdogo nilionao hakuna mtu mwenye akili timamu atakayepoteza haki yake ya msingi kwa kumchagua fisadi papa Lowassa.

Katika misifa yakijinga yote uliyompa Lowassa, umeweza kaielezea moja tu ya harambee.

Kwa taarifa yako hizo hela zote alizokuwa anachangia kwenye misikiti na makanisa, ndio hizo za kifisadi zilizochotwa kupitia mahasimu wake akina Rostam, na zilipangwa makusudi kabisa kwa ajili ya kampeni. Hiyo ilikuwa ni kampeni kabisa.

Magufuli ni mzalendo, vilevile watu walikuwa hawamualiki kwenye harambee.

Anonymous said...

Nonsense; you're a brainless human being! Hivi wewe unapoambiwa piga kura urudi nyumbani unadhani unaambiwa uende ukajifungie kwenye banda lako? Unachoambiwa baada ya kupiga kura endelea na shughuli zako za kila siku. Kwa akili yako ndogo na uzoefu wako mdogo, ni nchi gani duniani umeshawahi kuona wapiga kura wake wanabaki kulinda kura zao baada ya kupiga kura?

Anonymous said...

Dk. Magufuli amekwishafaulu interview ya kazi anayotafuta hivyo tunangojea tu waajiri wake (Watanzania) kupma baura ya ajira. Hongera sana Dk. Magufuli na tunakuomba uje kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu.