ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 21, 2015

MAMA MWANAMWEMA SHEIN AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA UWT WILAYA YA MJINI UNGUJA

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Mjini Bi Waridi Juma akisoma risala ya Wanawake wa Mkoa wa Mjini wakati wa mkutano na Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, Mama Mwanamwema Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar.
Viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati wa mkutano wake na Viongozi hao uliofanyika Afisi ya CCM Mkoa Amani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Salama Aboud Talib akizungumza wakati wa mkutano huo na kuwakaribisha Viongozi wa Ujumbe wa Kampeni ya Mama Mwanamwema Shein, kuzungumza na Viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja. 
Makamu Mwenyekiti wa UWT Mstaaf Balozi Amina Salum Ali akiwasalimia Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Mkoa wa Mjini katika mkutano na Mama Mwanamwema  kuwahamasisha Viongozi wa UWT Zanzibar katika kupiga kura kwa Wagombea wa CCM.  
Makamu Mwenyekiti wa Mstaaf wa UWT Zanzibar Balozi Amina Salum Ali, akitowa nasaha zake kwa Viongozi wa UWT kutumia nafasi zao kuwahamasisha Wanawake kukipigia kura Chama cha Mapinduzi kwa Wagombea wao wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na Wagombea wote wa CCM. 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja Silima Borafya akizungumza na Viongozi wa UWT katika mkutano wao na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati wa kumuombea Kura Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.
Muasisi wa Umoja wa Wanawake Tanzania Bi Asha Simba akiwasalimia Viongozi wa UWT na kuwaomba kukipigia kura Chama cha Mapinduzi na Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, mkutanom uliofanyika katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar. 
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akitowa nasaha zake kwa Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania kukipigia kura ya Ndio Chama cha Mapinduzi na Wagombea wao wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.   
Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Mjini Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akizungumza wakati wa mkutano huo wa kuwaombea kura Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli. na Wagombea wote wa CCM.
Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania wakionesha mikono juu kuashiria kuwapigia Wagombea wa CCM Kura ya Ndio kwa Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli. 


Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Viongozi wa Umoja wa Wanawake wa Mkoa wa Mjini Unguja na kuwaomba kumpigia Kura ya Ndio Mgombea wa Urais wa CCM Dk Ali Mohamed Shein na Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na Wagombea wote wa CCM.
Mke wa Rais wa Zanzibar akiwahutubia Viongozi wa UWT wa Mkoa wa Mjini Unguja wakati wa mkutano wake wa kampeni ya kumuombea Kura ya Ndio Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein. 
Viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini wakifuatilia hutuba ya Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimuombea kura Dk Shein.
Umoja wa Wake wa Viongozi wa CCM Wabunge na Wawakilishi wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar  wakijumuika na Mke wa Rais wa Zanzibar kumuombea Kura Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. 
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com
Mob. 0777424152 or 0715424152.
Email. othmanmaulid@gmail.com 

No comments: