ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 21, 2015

TFDA NA TAASISI YA TRADEMARK EAST AFRICA (TMEA) WAZINDUA MFUMO WA UTOAJI VIBALI KWA MFUMO WA KIELEKITRONIKI

 Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi (kulia), akibonyeza kituvye Dar es Salaam leo asubuhi, kuashiria uzinduzi wa mfumo wa utoaji vibali kwa njia ya kielekitroniki (e-portal) ambao utawezesha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kuhudumia wateja wake kwa kutumia mtandao wa intaneti. Mpango huo unaendeshwa kwa ushirikiano wa TFDA na Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA)
 Viongozi wakiwa meza kuu wakifuatilia uzinduzi huo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo ya uzinduzi.
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Viongozi wakiwa tayari kuzungumza na wanahabari. Kutoka kulia ni Meneja wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA), Josephat Kweka,  Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo.
 Maofisa Habari kutoka Kampuni ya PR ya  PPR, wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo (kushoto), akizungumza na wanahabari.


Na Dotto Mwaibale


MAMLAKA ya Chakula na dawa nchini (TFDA), imezindua mfumo mpya wa utoaji vibali kwa mfumo wa kielektroniki ujulikanao kama 'e-portal'.

Mfumo huo uliogharimu kiasi cha sh. milioni 300 kwa ushirikiano wa taasisi ya Trademark East Afrika(TMEA) kwa kutoa dola za marekani 250,000 lengo ikiwa ni kuboresha mfumo wa utoaji huduma kwa njia ya mtandao.

Akizungumza Dar es Salaam leo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando, Dk.Mkuu wa Serikali Muhammad Kambi alisema mfumo huo uliozinduliwa umekuja wakati muafaka kwani utasaiduia kuboresha huduma katika sekta ya afya kwa kuongeza uwazi, ukweli na kwa uharaka zaidi.

"Mfumo huu uliozinduliwa leo utarahisisha katika kufanya maamuzi ya kudhibiti katika utoaji wa vibali vya kuingiza bidhaa nchini na kutoa bidhaa nje ya nchi kwa kuwa wa kuandaa vibali utafupishwa na utaongeza faida katika mamlaka hiyo,"alisema.

Alisema mfumo huo utasaidia kuhudumia wateja na katika kusajili na kufuatilia ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za chakula,dawa, vipodozi na vifaa tiba sokoni sanjari na kuongeza kiwango cha wateja katika kuzingatia matakwa ya kisheria.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo alisema mfumo huo mpya unatumiwa na watu takribani 300 ambao wamethibitisha kuwa hauna matatizo yeyote kwani lengo la mamlaka hiyo ni kuhakikisha wanapunguza muda wa wateja wao katika kuomba vibali ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za huduma hiyo.

"TFDA inatambua mchango wa TMEA katika kuendeleza mfumo wa e-portal ambao utarahisha ukusanyaji wa takwimu, uchambuzi na uhifadhi wa taarifa za usajili, uratibu na ufuatiliaji wa taarifa za ubora na usalama wa vyakula dawa, vipodozi, vifaa tiba nchini,"alisema.  

Mkurugenzi wa TradeMark East Afrika Tawi la Tanzania, Dk. Josephat Kweka alisema mfumo huo utasaidia kuweka mazingira mazuri ya kibiashara hasa katika kuingiza na kutoa bidhaa katika soko la ushindani.

"Portal inatarajia kuongeza kasi ya usajili, kupunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi na muda wa kusafirisha bidhaa nje ya nchi. Tumewawezesha portal hiyo ili kukuza biashara ya kikanda na ushirikiano wa kiuchumi kwa nchi za jumuia za Afrika Mashariki,"alisema.


Aidha uzinduzi huo ni hitimisho la maboresho ya mfumo huo ulioanza mwaka 2011 ambapo utawawezesha wafanya biashara kuomba na kupata vibali vyote muhimu kwa njia ya mtandao bila kulazimika kufika ofisi za mamlaka hiyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments: