Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akifungua Mkutano wa viongozi wa dini mkoani Dodoma uliojadili masuala ya amani na utulivu wakati wa uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.Picha na John Banda
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SACP David Misime akifafanua jinsi jeshi la polisi Dodoma lilivyojipanga kusimamia amani na utulivu wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25 mwaka huu kwenye kikao cha viongozi wa dini kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Viongozi wa dini wakiendelea kufuatilia kwa umakini kinachoendelea kwenye mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mapema leo kujadili masuala ya amani na utulivu wakati wa uchaguzi mkuu oktoba 25.
Kaimu sheikh wa Mkoa wa Dodoma Ahmed Said Ahmed akiomba Dua ya shukrani kwa majadiliano na makubaliano ya kulinda amani na utulivu wakati wa uchaguzi Mkuu Oktoba 25 yaliyofikiwa wakati wa kikao cha viongozi wa dini kilichoitishwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya viongozi wa dini Mkoa wa Dodoma wakiomba Dua ya shukrani kwa majadiliano na makubaliano ya kulinda amani na utulivu wakati wa uchaguzi Mkuu Oktoba 25 yaliyofikiwa wakati wa kikao cha viongozi wa dini kilichoitishwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria Mkutano uliojadili masuala ya amani na utulivu wakati wa Uchaguzi Mkuu ifikapo Oktoba 25.
3 comments:
PAIR YA HAWA WATU WAWILI BALAA. MKUU WA MKOA WA DODOMA CHIKU GALAWA ANAAMURU KUVUNJA MIKUTANO HALALI YA KAMPENI ZA CHADEMA KUWAWEKA NDANI WAGOMBEA NA WAFUASI WA CHADEMA.AKIAMBATANA NA RPC DAVID MISIME WANAKAGUA NYUMBA ZA KULALA WAGENI NA HOSTELI MBALI MBALI WAKIWASAKA WANAFUNZI WAVYUO VYA ELIMU YA JUU[ADUI MKUBWA WA CCM].NA HUYU KAMANDA DAVID MISIME NDIYE ALIYEKUA MSIMAMIAJI MKUU WA POLISI KUWAPIGA WANA CCM WAFUASI A MHESHIMIWA LOWASSA MWEZI JULY 215 WAKATI WA MCHAKATO WA CCM KUMPATA MGOMBEA WAKE.KWA MIKONO YAKE MISIME ALIWAPIGA SANA WALE WAANDAMANAJI,ALIWAMWAGIA MAJI YA UPUPU.JUZI TENA KATILI HUYU KATAMKA TENA HADHARANI,"SIKU YA UCHAGUZI WATU WAKITURUSHIA MAWE,NA SISI TUTAWARUSHIA MAWE LAKINI YA KWETU SIO YA KUOKOTA[AKIWA NA MAANA YA RISASI ZA MOTO]HUKU CHIKU GALAWA ALIYEKUA AKIMSIKILIZA AKIANGUA KICHEKO CHA NGUVU.KWA UJUMLA HAWA WAWILI HAWATAKWENDA THE HAGUE,WATASHUGHULIKIWA NA VYOMBO VYA DOLA VYA HAPA HAPA NDANI YA TANZANIA.TUNAO POLISI,MAHAKIMU NA MAJAJI, WENYE WELEDI MKUBWA,HESHIMA NA NIDHAMU YA HALI YA JUU YA KAZI NA WAJIBU WAO,HAO NDIYO WATAKAYOITUMIKIA SERIKALI MPYA YA AWAMU YA TANO INAYOKUJA JUMAPILI TAREHE 25 OCTOBA 2015 BAADA YA UCHAGUZI MKUU UTAKAOMPA MHESHIMIWA LOWASSA USHINDI MKUBWA SANA.
Uongo mtupu.
mkuu wa mkoa wa dodoma,chiku galawa hatufai kabisa hapa dodoma.ukatili wake unasambaa hata vijijini.sasa hivi mkoa wa dodoma umekumbwa na njaa kubwa.wana vijiji kwenye jimbo langu waliwahi kumuomba msaada sio wa yeye kutupatia chakula,tunajua hana ila atoe taarifa sahihi ofisi ya waziri mkuu tusaidiwe.taarifa ile aliogopa kuipeleka eti wakubwa zake wataona hakutimiza wajibu wake wa kuhimiza kilimo cha mazao yanayostahili ukame.galawa zaidi ya dodoma mjini ni nyumbani kwake dar-es-salaam.kiongozi gani huyu.au kwa kua ni uteuzi.hatufai,hafai ni garasa.
Post a Comment