Advertisements

Tuesday, October 6, 2015

PICHA: MH. MWANG'OMBE AENDELEA KUCHANJA MBUGA MBIO ZA UBUNGE

Ni mwana Diaspora Liberatus Mwang'ombe anaye onekana kuwa na mvuto wa kipekee kwenye mbioza kuelekea Dodoma. Mwang'ombe amekuwa akikusanya watu wengi sana hata akisimama kwenye vijiji vidogo ambavyo havina watu wengi. Pichani akiwa kwenye vijiji viwili vidogo ambavyo havina historia ya watu kuhudhuria mikutano ya kisiasa; lakini ilikuwa tofauti kwa Mh. Mwang'ombe

Libe anawaomba wana diaspora na waTanzania wote kumuunga mkono kwa kumchangia fedha ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mtunga sheria Tanzania. Msaada wa fedha anaomba utumwe kupitia;

M-PESA- WAVE App number +255 752 494 409

Au, wasiliana na: 
Rehema Sarmet 301 367 9711
Lukresia  240 593 5973
Jabil  240 604 0574 
Juu na chini: Wananchi wakiomba Ukodaki moment na Mh. Mwang'ombe, Igunda, Mbarali


 Swaga imekulea Igava, Mbarali





Hapa ni kijiji cha Igunda, Mbarali

2 comments:

Anonymous said...

sielewi kumuita mheshimiwa!!! mheshimiwa wa nini kwani ana cheo gani mpaka kuitwa mheshimiwa. wewe luka hebu jifunze Kiswahili, ibanie basi na hii sababu huyo jamaa ni rafiki yako. kama kweli anavutia watu mbona hatumi picha zake michuzi. anatumia blog yetu ya jamii kwa propaganda. luka kuwa fair, mbona comment zake huweki unaminyia, demokrasia ya kweli waache watu washuke comment tuone kama kweli kama anavyoandika ni ya kweli. ni kuelimisha tu dj kama kawaida usiipost basi na hii maana hutaki kumuudhi jamaa yako.

Seba said...

Kwanini asiitwe mweshimiwa kuna watu wana hate hata wale wanataka kusaidia jamii! Mtu anayeacha kazi yake kwenda nyumbani kwa siasa kusaidia watu ni muheshimiwa mkubwa kuliko wapiga porojo wa kila siku