PONGEZI :
Tawi la CCM-New York linampongeza Mh. Dr. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa rahisi wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Vivyo hivyo Tawi linawapongeza wananchi wa tanzania kwa kufanikisha zoezi hilo kwa utulivu na amani na kukiamini Chama cha Mapinduzi kwa mara nyingine tena. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa.
IMETOLEWA NA UONGOZI WA TAWI.
8 comments:
Tanzania ina watu millioni ngapi kulinganisa na waliopiga kura na waliomchagua ni ndogo mno tunahitaji uchaguzi wa nguvu na haki zaidi. Pia wagombea wawe wana raise funds za kampeni sio kufuja mabenki, mishahara ya waalimu nakila kona. Nasi tulioko ughaibuni tusipongeze tu tutoe mawazo sio kukaa kula nyama choma kupongezana wakati ndg zetu wananunua sukari sh 3000 kilo moja. !! Adios.
Wanapongeza ni wasiolipa kodi wakipekeka mizigo Yao bongo, au unga
makabwela tu...kaibenkaibeni bongo hapa states mtabeba box tu. Hivyo vidola 300 vimeshakwisha
Wewe umechanganikiwa tu/ Pole sana. Hebu tuambie ni nchi gani hapa duniani ambayo wananchi wake wote hupiga kura! Swala la ndugu kununua sukari sh. 3000 kilo moja lina uhusiano gani na uchaguzi. Hivi bei za vitu zinapopanda hapa Marekani mshahara wa wafanyakazi nao hupandishwa? Swala la ufujaji pesa nakushauri umuulize mgombea wenu aliyeshindwa atakueleza kwani yaye anajulikana kwa shughuli zake za ufisadi.
Not very Tanzanian qualifies to vote, hivyo uwingi wa watu hauna effect on voting pattern.
Tunakuombeni sana kama mna mpango wa kufanya sherehe hizo fedha tuzichangeni ili ziwasaidie watoto mashuleni kupata walau dawati au blanketi kwa ajili ya baadhi ya hospitali zetu, sio hayo tu yako mengi. Hata DMV TUNAOMBA kuna katabia kakufungua matawi hiyo fedha ni ile ile iliyotolewa na kiongozi fulani huko Tanzania badala ya kuwasaidia ndugu zetu zinatumbuliwa US!! what is that!! Kuna mambo ambayo tunaweza kuyaacha au kupunguza munkari wake jamani!!
NI KWANINI BASI TUSIKAE KWA UPAMOHA STATE ZOTE TUONE JINSI GANI YA KUUSHAWISHI UONGOZI UNAOKUJA KURUHUSU URAIA PACHA KAMA ANAETOKA AMETUBEZA?? YOU GUYS BE SERIOUS.
Hongera magufuli,hongera big Apple. Ny inajulikana kuwa na ya watu werevu haiwezekani uwe unaishi ny city halafu ushindwe kuelewa ya kwamba Lowasa hawezi kuwa kiongozi atakae kizi matarajio ya watanzania bali alichokuwa anataka kufanya lowasa ni kukizi matarajio yake mwenyewe binafsi na kwa mtu yeyote anaeishi nje hasa marekani hawezi kumsapoti lowasa la sivyo huyo mtu anaabudu ukanda. Tumeshuhudia huku viongozi kama magavana na senators pamoja na mawaziri tena maarufu tu na wachapa kazi lakini once anapohusika na kashfa inayohusiana na maadili anakuwa ndio basi tena kisiasa it is over. Sasa leo lowasa anahusika na upotevu wa mabilioni ya pesa za umma bado watu wanamsherekea hee? Jamani tumejifunza nini kukaa kwetu huku nchi zilizoendelea?
tumewaona.mmenenepeana hadi meno,yale mafungu ya wizi yanayopitia ubalozini mnakaidhiwa nyinyi.kwa ujumla hamna ushirikiano wowote kwa sababu nyinyi wote mliletwa na mkapa, na kikwete marekani mkiwa hamna cv za kuwa majuu.mimi naishi new york nawajueni,unafiki tuu.
Post a Comment