picha ya juu ni redio national panasonic kablakampuni haijagawanyika kuwa national kwake na panasonic kwake, zilikuwa maarufu enzi hizo, zilikuwa redio madhubuti sana na ni watu wachache kwa wakati huo walioweza kumiliki vyombo kama redio na TV, kama utakumbuka kipindi cha pwagu na pwaguzi kikifika utakuta kundi la watu wanasikiliza vichekesho vyao, au wakati wa kipindi cha michezo ni hivyo hivyo, kubwa zaidi ni wakati wa vita vya kagera ni makundi ya watu yanakushanyika pale kwenye redio kila sehemu kujua nini kinaendela. huko ndiko tulikotokea
hicho kiatu kwa wakati huo kama wewe ni kijana hujavaa hiyo kitu na ni mtoto wa mjini basi unaonekana umechelewa, vijana wengi wa mijini ilikuwa ni ndio aina ya viatu wanavyovaa na suruali ambayo ilikuwa pana chini, ikijulikana kwa jina la buga shati iliyobana, (slim) rise on ni aina ya vitu vilivyotamba sana kwenye miaka ya mwishoni mwa sabini na mwanzoni mwa thamanini. munaikumbuka hiyo wale wa enzi hizo?Tujikumbushe tulikotoka, itakuwa inawajia kila jumamosi na jumapili, tutakuwa tunaweka picha na video za matokeo mbali mbali yaliopita,(zamzni) ikwa mashuleni, kijijini, kazini, michezoni, maghafali mbali mbali, maigizo, nyimbo na picha binafsi. tafadhali tutumie kupitia email tujikumbushetulikotoka@gmail.com vikiambatana na maelezo, ili wasomaji na wadau wa vijimambo tuweze kujikumbusha mambo tuliopitia.
No comments:
Post a Comment