ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 15, 2015

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI ENEO LA CHAKECHAKE, PEMBA

 Wananchi mbali mbali wa mji wa Chake Chake wakiangalia fusi lililomfunika marehemu Seif Kibishi (33) mkazi wa Tibirinzi, baada ya kufunikwa na fusi la mawe baada ya kuporomoka wakati walipokuwa wakichimba msingi wa nyumba ya Ghorofa katika soko la Katari Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
Kifusi cha mawe kilichoporomoka na kusababisha kifo cha kijana Seif Kibishi (33) mkazi wa Tibirinzi Chake Chake, katika eneo la soko la Katari.
 Askari wa kikosi cha zimamoto na uwokozi Chake Chake Pemba, wakivunja mawe kwa kutumia nyundo, ili kufukuwa kifusi kilichomfunika kijana Seif Kibishi(33)na kupelekea kupoteza maisha, baada ya kifusi hicho cha mawe wa fondesheni ya jingo la ghorofa, kumwangukia wakati alipokuwa akichimba msingi yeye na wenzake wanne katika soko katari.
 Askari wa Polisi Mkoa wa kusini Pemba wakiweka ulinzi katika eneo lililoporomoka kifusi cha mawe na kusababisha kifo cha kijana Seif Kibishi (33) mkazi wa Tibirinzi Chake Chake, huku vikosi vya uokozi vilipokuwa vikifanya kazi ya kufukuwa kifusi hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdalla mwenye baibui, akiangalia kazi ya ufukuaji wa mwili wa kijana Seif Kibishi (33) mkazi wa kibirinzi Chake Chake, iliyokuwa ikifanywa na vikosi mbali mbali vya ulinzi na usalama mkoa huo huko katika soko la katari.
 Wananchi mbali mbali wakishuhudia kazi ya uokoji wa mwili wa kijana Seif Kibishi (33) mkazi wa Tibirinzi Chake Chake, aliyefunikwa na fusi.
 Vikosi mbali mbali vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kusini Pemba, wakiutoa mwili wa kijana Seif Kibishi (33) mkazi wa Tibirinzi Chake Chake, mara baada ya kufukiwa na fusi la mawe huko katika soko la katari, wakati alipokuwa akichimba msingi wa nyumba ya ghorofa.
 Vikosi vya ulinzi na Usalama Mkoa wa kusini Pemba, wakiubeba mwili wa marehemu Seif Kibishi(33)mkazi wa Tibirinzi Chake Chake, mara baada ya kuufukuwa katika kifusi na kupeleka katika gari ya wagonjwa kwa kupelekwa spitali.
 Kikosi Cha Huduma ya kwanza Red Cross Kisiwani Pemba, wakiongozwa na Dk Suleima Ali wa kwanza kushoto wakiwa wameubeba mwili wa marehemu Seif Kibishi (33) aliyefukiwa na kifusi na kupeleka katika chumba maalumu cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Chake Chake kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
 Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza na waandishi wa habari mbali mbali kisiwani Pemba, mara baada ya kukabidhiwa kwa mwili wa marehemu Seif Kibishi aliyepoteza maisha baada ya kufunikwa na kifusi.
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mhe. Hanuna Ibrahim Masoud akiwa na katibu tawala wake Rashid Khadid wakijadiliana na ndugu na jamaa wa marehemu kijana Seif Kibishi aliyepoteza maisha baada ya kufunikwa na fusi, juu ya maandalizi ya mazishi ya marehemu huyo.

No comments: