
Mbunge
mteule wa Jimbo la Mtama, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape akisaini
mkataba wa kupata vifaa vya huduma za afya mbele ya Mwambata wa Siasa wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Mis Song Rui katika ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China.
Mbunge
Mteule wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye ameanza kazi ya kuwatumikia
wakazi wa jimbo hilo baada ya kusaini mkataba maalum na Ubalozi wa China
nchini wa kusaidia vifaa vya huduma ya Afya kwa jimbo la Mtama.
Ikumbukwe
katika kampeni zake Nape aliahidi kulifanya jimbo kuwa la mfano kwa
kuboresha huduma mbali mbali za kijamii ikiwemo afya na elimu.
Akiongea
na mwandishi wa habari hizi Nape alisema " Wakati nimeamua kugombea
ubunge nilisema nataka kuwafanyia kazi watu wa Mtama nataka niwe mbunge
wa mfano na niliwaahidi nitatatua kero zao mbali mbali na leo nimeanza
kwa upande wa huduma za afya ambapo vituo na zahanati kadhaa vitapata
vifaa vya matibabu alivitaja baadhi ya vituo ni Mtama, Nyangamala,
Chiponda, Namupa, Chiuta,Luo, Nyengedi,Kiwalala na kwengineko."
No comments:
Post a Comment