Advertisements

Saturday, November 28, 2015

CHAMPIONI YATUNUKU TUZO KWA WAANDISHI NA WAHARIRI WAKE

MC wa hafla ya ugawaji tuzo, ambaye pia ni Mhariri wa Gazeti la Championi Jumamosi, Elius Kambili akitoa neno la utangulizi wakati wa shughuli hiyo.
Mwenyekiti wa shughuli hiyo ambaye pia ni Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally akifungua rasmi hafla fupi ya utoaji tuzo kwa waandishi na wahariri wa Championi.Mhariri wa Gazeti la Amani, Andrew Carlos (kushoto) akikabidhi tuzo ya Mwandishi Bora Chipukizi wa Championi kwa Omary Mdose.
Mhariri wa Gazeti la Uwazi Mizengwe, Hashim Aziz (kushoto) akikabidhi tuzo ya Msanifu Kurasa Bora wa Championi kwa Shafih Hashim. Mhariri Mwandamizi, Mzee Walusanga Ndaki (kushoto) akikabidhi tuzo ya Mwandishi Bora wa Championi kwa Wilbert Molandi.Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli akikabidhi tuzo ya Mpiga Picha Bora wa Championi kwa Richard Bukos. Ofisa Mauzo wa Global, Jordan Ngowi akikabidhi tuzo kwa Mhariri Bora wa Championi Kimauzo, Phillip Nkini. Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) akikabidhi tuzo ya Mhariri Bora kwa John Joseph. Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula (kushoto) akikabidhi picha maalum ya timu ya Championi kwa Abdallah Mrisho.Abdallah Mrisho akitoa neno la shukrani kwa timu ya Championi.Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli (kushoto) akikabidhi Tuzo Maalum ya Sapoti Bora ya Mzazi kwa Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo.
Eric Shigongo akizungumza na wafanyakazi wa Global (hawapo pichani).Wakati wa chakula cha mchana ukawadia. Wafanyakazi wa Global wakifuatilia kwa karibu utoaji tuzo. Picha za pamoja kwa walionyakuwa tuzo hizo.

Picha ya pamoja ya wandishi wa Championi.

PICHA NA RICHARD BUKOS NA MUSSA MATEJA/GPL

No comments: