Wednesday, December 9, 2015

Jussa akanusha taarifa za uvumi wa kifo cha Maalim Seif

ismail-jussa-ladhu

Ismail Jussa akikanusha taarifa za uvumi kuhusu Maalim Seif.

Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chama Cha Wananchi (CUF), Ismail Jussa amekanusha uvumi uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu taarifa za kufariki dunia kwa makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad na kusema wanaofanya hivyo ni watu wenye nia ovu na kiongozi huyo.

Awali kabla Jussa hajatoa taarifa hizo, Kituo cha ITV kilikanusha taarifa hizo za upotoshwaji kupitia mitandao ya kijamii ambazo zilikihusisha, na kuwaomba wananchi kuzipuuza maana si za kweli.

Kupitia ukurasa wao wa Facebook, ITV waliandika hivi: Kumekuwepo wa taarifa za upotoshwaji kupitia mitandao ya kijamii na kuihusisha ITV, tunaomba taarifa hizo zipuuzwe kwa kuwa taarifa hizo si kweli. Taarifa zetu zinakuwa na vyanzo vya kuaminika, ITV haihusiki kwa namna yeyote na taarifa hii. Tunaomba Watanzania wawe makini na Mitandao feki inayozusha matukio na kutoa taarifa zisizo za kweli. Tunaomba vyombo husika kuendelea kuwafuatilia na kuwabaini na kuwaweka hadharani watu kama hawa.
Bofya soma ziadi usome Sehemu ya taarifa hiyo ya upotoshaji.
itv
Habari kwa hisani ya GPL

No comments: