
Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa pili unaendelea leo kwa mchezo mmoja kuchezwa mmoja katika uwanja wa Majimaji mjini Songea kati ya JKT Mlale dhidi ya Mighty Elephant.
Kesho Jumatano kutakua na michezo miwili, Kariakoo ya Lindi watawakaribisha Mshikamano FC katika uwanja wa Ilulu – Lindi, Disemba 24 Njombe Mji watakua wenyeji wa Green Warriors katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, na Pamba FC watacheza dhidi ya Alliance uwanja wa CCM Kirumba.
Ijumaa siku ya sikukuu ya Krisamsi Lipuli FC watawakaribisha Kurugenzi katika uwanja wa Wambi Mafinga.
Mzunguko huo wa pili unatarajiwa kumalizika Disemba 29 mwaka huu kwa michezo minne, Wenda FC v Kimondo (Sokoine), Mji Mkuu (CDA) v Singida United (Jamhuri), Mvuvuma v JKT Kanembwa (Tanganyika), Abajalo FC v Villa Squad (Karume)
Timu saba za Ashanti United, Burkinafaso, Geita Gold, Friends Rangers, Madini FCM, Panone na Rhino Rangers zimeshakata tiketi ya kucheza mzunguko wa tatu wa Kombe la FA mwezi Januari 2016, pamoja na timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.
2 comments:
Waangalie wachezaji wetu hapo halafu jiulize jee Tanzania kuna mpira?nasema Tanzania hakuna mpira Ila yapo Mazoezi,tena mengi ya viungo na makocha- viroba,wababaishaji kwa maelfu.yapo matatizo makubwa kadhaa ya Wachezai wetu Kushindwa Kufikia Soka Imara,Lililopevuka,Endelevu,Linalotia Matumaini kama Wenzetu majirani wa Uganda,Kenya,Rwanda,Burundi,Ethiopia,Sudan[sithubutu kutaja Misri] Malawi,Mozambique,Zambia,Namibia [naogopa kutaja Congo].hii ni kwa uchache,yaani hatufai,hatufai ni uchizi mtupu.Kuelemewa kwa mpira wetu [KWA MAONI YANGU YALIYOSHEHENI UTAMBUZI] kunatokana na [NISIKILIZE SANA]:1.MAUMBILE YA WACHEZAJI WETU UFUPI[DWARFTNESS] FUTI 4.5,5 NDIO WENGI[MIMI FUTI 6.4],ULEGEVU MFANO WA UTAPIA MLO,MISULI KUSINYAA,MIGUU KUSHINDWA KUPANUKA WAKATI WA MBIO[FLASH]2.UBONGO KUTITIA-RETARDATION-MAWAZO MAFUPI,HAKUNA UBUNIFU-MBINU,KUHARIBIWA NA BANGI 3.KUJIONA WAMEFIKA,KUDHARAU VIONGOZI, WADAU NA WASHABIKI KWA UJUMLA 4.ZERO TECHNIC ADAPTATION-KUSHINDWA KUWAEEWA MAKOCHA WAWAFUNDISHAPO,WANAKOSA SERIOUSNESS,UTOTO MWINGI,HAWAELEWI WALA KUJIELEWA 5.ELIMU NDOGO SANA YA DARASANI HIVYO MBINU NYINGI MPYA HAWAWEZI KUZIMUDU-MPAKA WAWASIKILIZE WAKALIMANI. 6.KWA UJINGA NA USHAMBA WANAPENDA WANAWAKE-AKIWA NAO WANNE- SITA ANAWATAMBIA WENZIE.7.WANAPENDA[KWA USHAMBA NA PASIPO SABABU KUJIPACHIKA MAJINA YA NYOTA WA ULAYA.8.WAMEJAA WIVU NA CHUKI KWA KILA CHIPUKIZI ANAYEINUKIA[WANATAMANI KUMDHURU, KUMMALIZA].HATUNA MPIRA TANZANIA.NIMESOMA KWA MIAKA MINGI MFUMO WA MAUMBILE YA WATU WA AINA HIYO,NIMECHEZA SANA MPIRA [WA AKILI]VYEO VIKANIPIGA STOP [NILIKUA NAPANDA PAMOJA NA KUSTAHILI LAKINI TOO MUCH],NAIJUA VILIVVYO DUNIA YA SOKA NA WANASOKA.JIULIZE WACHINA WAPO BILLION 3 WANA TIMU GANI YA DARAJA LA DUNIA VIVYO HIVYO INDIA MILLION 850.UMEELEWA? NAITWA PEW P.PANGAWE AU TWENDE KWA TRIPLE 'P'.NIMEKUAMSHA,AMKA.
pew panga wewe ,mkali, kiboko,fimbo nimeamka sasa pew hebu tupe ufumbuzi,hivi kweli upo?tanzania kama tanzania zichukuliwe hatua zipi kuyaleta mapinduzi yenye neema?
Post a Comment