Video ya Matukio ya mwaka 2015 katika Umoja wa Mataifa
2015 – mwaka uliosheheni matukio ya aina yake na picha za kutisha: Maiti ya mtoto mdogo wa kiume akisombwa hadi ufukweni, kiashiria cha janga la wakimbizi Milioni 60: wananchi wa Paris, Beirut na Nairobi wakikmbia mashambulizi ya kigaidi, na nchi zilizosalia magofu kutokana na mapigano yasiyoisha. Matukio ya mwaka 2015, yanakumbusha changamoto ambazo Umoja wa Mataifa umekumbana nazo katika miaka 70 ya tangu kuanzishwa kwake- lakini yanatupatia muhtasari wa mafanikio yatokanayo na ushirikiano.
Fursa ya mashauriano bora kwenye suala la nyuklia la Iran, - ushirikiano wa dunia kukabili Ebola na Umoja wa nchi zote wanachama kwenye kuwekeza kwa kauli moja katika mustakhbali wa sayari ya dunia kwa kupitisha ajenda ya maendeleo endelevu na kutokomeza umaskini, sanjari na mkataba wa kihistoria wa Paris, kuungana katika tabianchi na kuepusha ongezeko zaidi la kiwango cha joto siku za baadaye.
Kuangalia video hii bonyeza hapa
No comments:
Post a Comment