Mkurugenzi wa kanda ya Kaskazini
kutoka Tigo Bw.George Lugata akimkabidhi Bw.Danson Kaijage kushoto laini mpya
ya 4G LTE katika uzinduzi wa huduma ya 4G LTE, katikati ni Territory Meneja wa
Dodoma,Singida na Kondoa Bw.Innocent Anthony kutoka Tigo jijini Dodoma.
· Ni
baada ya kuanza kutoa huduma hiyo kwa ufanisi jijini Dar es Salaam
Dodoma, Novemba 30 2015. Wateja wa Tigo waishio
Dodoma sasa wanaweza kupata mtandao wa intaneti wenye kasi kubwa zaidi kufuatia
upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4G LTE hadi kufikia jiji hilo lilopo
kaskazini mwa Tanzania Teknolojia ya 4G LTE ina kasi mara tano
zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.
‘’Upanuzi huu umetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana
katika majaribio ya awali ya utoaji huduma ya 4G jijini Dar es
Salaam kuanzia mapema mwaka huu’’, amesema Mkurugenzi wa kanda ya
Kaskazini, George Lugata.
Akizungumza leo
na waandishi wa habari jijini Dodoma, Lugata amesema: "ni kielelezo cha
jinsi ambavyo Tigo imedhamiria kufanikisha kuleta mabadiliko
ya dijitali katika maisha ya watanzania na pia kuwa katika msitari wa
mbele wa kutumia teknolojia ya kisasa na kibunifu nchini Tanzania."
Mtandao wa 4G
LTE una kasi kubwa zaidi katika kuperuzi na kupakua kwa
rahisi kutoka kwenye mtandao wa intaneti na pia katika
kufanya mawasiliano kwa njia ya Skype. Huduma hii pia inaharakisha
urushwaji wa picha za video na ubora hali ya juu na kufanya mikutano kwa njia
ya mtandao.
“Tunapenda
kuwahakikishia wateja wetu waishio Dodoma kwamba sasa wanaweza kufurahia huduma
bora zaidi za mawasiliano kutoka Tigo na Intaneti yenye kasi zaidi,” Lugata
amesema. Dodoma ni moja wapo ya miji mikubwa Tanzania, na pia inajivunia Bunge
la Tanzania na kwa sababu ya kuwa na vyuo viwili vikubwa Tanzania.
Wateja wote wa Tigo
4G LTE watanufaika na promosheni; kila atakapo ongeza salió la shilingi
elfu moja au zaidi, atapata mb 500 bure kama bonasÃ.
Ametaja miji mingine
katika mikoa sita ambapo 4G itaanza kupatikana hivi karibuni kuwa ni, Morogoro,
Moshi, Mwanza na Arusha,Tanga na hapa Dodoma “jambo ambalo linaifanya Tigo kuwa
na mtandao mkubwa wa 4G nchini Tanzania.” Lengo kuu ni kufikisha
huduma ya 4G katika kila kona za nchi ifikapo mwaka ujao, Lugata ameongeza
kusema.
|
No comments:
Post a Comment