ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 20, 2015

WAZIRI UMMY MWALIMU AVAMIA HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO MKOANI TANGA, KUKAGUA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA

IMG-20151220-WA0011
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wahudumu wa afya (jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi) wa dirisha la dawa katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga alipofanya ziara ya kushtukiza mchana wa leo Disemba 20, 2015.
-Atoa wiki mbili wawe wamefunga mashine ya kukusanya mapato kwa njia ya Kielektroniki ili kudhitibiti upotevu wa mapato yanayotokana na wananchi kuchangia huduma za afya.
IMG-20151220-WA0012
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wakina mama anayemhudumia mwanae katika wodi ya watoto Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga alipofanya ziara ya kushtukiza leo mchana Disemba 20, 2015.

IMG-20151220-WA0019
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akimsikiliza mmoja wa akina mama aliyelazwa kwenye wodi ya wazazi wakati wa ziara ya kushtikiza aliyoifanya mchana wa leo Desemba 20, 2015 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga.
IMG-20151220-WA0020
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO), Dkt. Clement Marceli akimwelezea changamoto wanazokabiliana nazo katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani).
IMG-20151220-WA0017
Daktari aliyekuwa kwenye mafunzo, Dkt. Zuberi (Medical Intern) akitoa maelezo ya namna wanavyohudumia wananchi wanaofika hospitalini hapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (kulia) aliyefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga mchana wa leo Desemba 20, 2015 ambapo Waziri huyo alikutana na changamoto utoro wa madktari wa zamu kutokuwepo kwenye kituo chao cha kazi katika Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga.
IMG-20151220-WA0016
IMG-20151220-WA0019
Mratibu wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo, mkoani Tanga kutoka Idara ya Tiba, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Ibrahimu Maduhu (mwenye tai) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu namna wanavyokabiliana na changamoto ya kuzuia vifo vya mama na mtoto katika hospitali hiyo wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Mh. Ummy Mwalimu katika wodi ya wazazi leo mchana Disemba 20, 2015.
IMG-20151220-WA0014
Baadhi ya madaktari waliokuwa mafunzoni wakizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu aliyefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo, mkoani Tanga mchana wa leo Disemba 20, 2015.
IMG-20151220-WA0023
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akipitia orodha ya mahudhurio ya zamu za Madaktari na Wauguzi ambao wengi hawakuwepo kazini wakati wa ziara yake ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga aliyoifanya leo mchana Disemba 20, 2015.

2 comments:

Anonymous said...

Waandishi maalum sasa wanaofuatana na hawa mawaziri wanachokifanya ni kuripoti maagizo na si kukagua na kuangalia hali halisi ya hapo wanapokua.uandishi wa aina hiyo haufai.wanaendekeza pesa na 'promotion' kitu ambacho si cha mfano mzuri.picha zinaonyesha katika hospitali hii wagonjwa wakiwa wamelala chini.hiyo ndiyo ilipaswa iwe issue kuu.jee mheshimiwa waziri ameagiza kuletwa vitanda vya kutosha?jee ameliona hilo? jee analipima vipi?muache blind promotion, fanyeni kazi ya kweli mawaziri wetu.MSIJE MKAGEUKA KUWA 'KITUKO'.

Anonymous said...

Hivi who cares picha ya waziri inapagwa vipi,tunachopaswa kujali ni kama ziara zao,ziwe za kushtukiza au za kupanga zinatatua changamoto zilizopo period! Hata wakipigwa picha kutoka kwenye satellite,we care less tunachotaka ni results.