Hali ya kutoeleweka inaendelea
kuibua maswali kwa nini wahudumu wa ndege na watu wengine saba
waliugua wakati ndege ya Shirika la ndege la American Airlines ikiwa
angani ikikatiza Atlantic kuelekea Los Angeles.
Wahudumu wapatao saba na abiria
wawili akiwemo mtu mzima mmoja wa umri wa miaka 60 na mwingine wa
miaka 40 inaaminika walijisikia kupoteza fahamu wakiwa washasafiri
maili 1,600 kati ya safari ya maili 5,500.
Abiria waliochanganyikiwa kwa hofu
walioamba wapate kutibiwa na madaktari ndipo rubani wa ndege ya
shirika la American Airlines, kuamua kutua kwa dharura kwa kurejea
Jijini London katika uwanja wa Haethrow.
No comments:
Post a Comment